Azam wameigharimu sana Yanga kuelekea mchezo wao na Mamelodi

Pacome aliumia kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya mechi, ila mwalimu aliamua kumwanzisha kutokana na umuhimu wa mechi.

Kwa mchezo ulivyokuwa, nadhani mwalimu alitaka kumaliza mechi mapema kisha ampumzishe kabla hajajitonesha.

Ila makosa ya Mzize yakagharimu timu. Kwani kabla ya kufunga lile goli alipoteza nafasi mbili za wazi kabisa zilizoundwa na Pacome.

Ova
 
Mkuu embu kuwa serious basi, swala la kuchezesha wachezaji wanaokaa benchi hutegemea na aina ya mpinzani unayeenda kucheza nae. Ucheze na Azam halafu upange wachezaji wanaokaa benchi kweli upo serious?
Hata kocha wa Yanga mara nyingi kawapanga wanaokaa benchi ila hutegemea na aina ya mpinzani anayecheza nae.

Hao Mamelod unajua hiyo timu iliyocheza nayo ipo daraja la ngapi?
Mamelod wamecheza na timu ya daraja la kwanza hivyo kwao haikuwa mechi ngumu na ndio maana wameweka wanaokaa benchi.
 
Walikua wanacheza Nedbank Cup hawa Mamelodi wametolewa kombe moja tayari kwa hiyo sasa hivi wanakaza sana..
Yanga wachezaji wa kucheza mechi ya Azam kwa beki za kina Fred na kibabage wanacheza vizuri tu kiungo yule dogo Shaha Mzanzibar anacheza vizuri tu kuliko mechi zote wachezaji hao hao ikitokea majeruhi kidogo tu kwa kuwa wachezaji hawapati nafasi kocha anaumiza kichwa gemu ya points tatu na mtoano ni tofauti ilitakiwa aangalie kule huku akiwalinda wachezaji sasa ajawalinda Wachezaji na kapoteza points...
 

Kama first eleven ya Yanga inasumbuana na Azam, hao wakina Shaha wataweza nini au unataka wafungwe nyingi? Imefanyika rotation dhidi ya Ihefu tu Yanga ikapoteza mechi ndio uje ucheze na Azam kwa timu ya kikosi cha pili?
 
Yanga hatuna presha kikosi chetu ni kipana mno.Madunduka yapo hoi presha imewajaa kama yanacheza menyewe.So far our target was group stage hata tukifungwa mia kuna shida gani?
 
Imetugharimu sana.
 
Pacome alikuwa benchi kwenye mechi ya Ivory coast na Benin Jumamosi, maana yake yuko fiti.
 
Ila watacheza.. wakiwa na majeruhi hivyo hivyo. Report ya dr hjwa haisikilizwi yanga maana jata mechi na cr belouzidad pacome alifosi na dr akakubali..
 
Hii mechi haikuwa na ulazima kabisa yaani.

Alafu TFF hao hao na serekali wanakuja na hoja ya uzalendo! Unataka watu wawe wazalendo huku unaipangia Yanga mechi ngumu few days kabla! Like serious?

Stupid kabisa yaani
Yanga wana kikosi kipana
 
Yanga hatuna presha kikosi chetu ni kipana mno.Madunduka yapo hoi presha imewajaa kama yanacheza menyewe.So far our target was group stage hata tukifungwa mia kuna shida gani?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] poleee kwa maumivuuu
 
Wakati timu zinajiaanda na Mechi round ya tano, Yanga walicheza back to back ndo wakakutana na CR Belouzdad.
Wakati Simba wanaomba recovery kwa wachezaji wao, Yanga wao wajiona wanaweza kwenda na move ileile kucheza kila baada ya siku 3, Tena mechi ngumu. Ujuaji utawagharimu.
 
Shida ni nini Yanga si wana kikosi kipana tulishaelewana..
 
Mechi ilikuwa bado two weeks.
 
Halafu Pacome alishambuliwa kwa makusudi tu, na yule aliyemshambulia wala hakupewa hata yellow card.
 
Pacome na Aucho wanaweza kucheza, tatizo Yao aliyeumia Nyama za paja, huwa zinachelewa kupona, coz huchanika ndani kwa ndani.
 
Kwa 2 big matches mkuu? Wiki 2 chache sana
Afisa HabarI wenu aliwahi kusema nyie siyo wa kudekadeka kama wale jamaa wa upande wa pili baada ya simba kuomba mechi yao na mtibwa isogezwe ili ajiandae vizuri kwa ajili ya kwenda kuwakabiri asec .

Tena akaongeza kwa kusema ,mna kikosi kipana mnaweza kucheza mechi 2 kwa siku Moja na zote mkashinda. Sasa haya malalamiko wanetu yanatoka wapi tena?
 
Wewe jamaa kweli ni utopolo. Hivi kama kweli kocha yupo serious na huyo mchezaji kwa nini amemruhusu kwenda national team wakati ni majeruhi.
Usiitafutie Azam sababu.
 
Acha ujinga , ratiba ya ligi kuu inakuwepo kabla ya hizo nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…