AzamTv wametudanganya kuhusu kuonesha michuano ya Euro

Azam wana ubabishaji mwingi sana. Walituonesha kale kamechi kamoja tu siku ya ufunguzi; wakapotea mazima. Ukifungua hiyo ZBC2 yao muda mwingi unakutana na Masheikh wao wanatoa mawaidha!!

Hovyo kabisa!
 
Mwaka ambao Azam aliomba tena haki ya kurusha ligi pia DStv alikuwepo, ila tatizo la DStv n alitaka kurusha mechi kubwa tuu za simba na Yanga tuu hapo ndipo kosa lake lilipo wakati mwenzake Azam anarusha hadi mechi za kajamba nani
Sasa kuna shida gani akirusha mechi za simba na yanga tu, na kuna ulazima gani wa kurusha mechi ndogo ambazo hazina watazamaji wengi, au sheria ndio zinataka hivyo kwamba ukichagua ligi fulani basi ni lazima urushe mechi zote za hiyo ligi
 
Sasa kuna shida gani akirusha mechi za simba na yanga tu, na kuna ulazima gani wa kurusha mechi ndogo ambazo hazina watazamaji wengi, au sheria ndio zinataka hivyo kwamba ukichagua ligi fulani basi ni lazima urushe mechi zote za hiyo ligi
Itakuwa Azam kamwaga mpunga mrefu + uzawa 😁,
Mbona dstv wanarusha ligi ya Zambia lakin sio HD,, hatar za kajamba nani za Zambia zinaoneshwa sembuse za kwetu!
Tena mkataba wa alioingia aZam ni mrefu na wanauboresha kila mara,,
Na vitasa kama kawa 😁,

Mzee kama vp funga zote dstv na Azam, alafu unakuwa unaamua ulipie ipi kulingana na burudani
 
Ni vyema Azam akaendelea kuonesha ligi yetu ya NBC,, unaipata HD,,

Dstv hatar ligi ya South Africa hawaitendei haki ,, lakin EPL si wanajiunga na Sky sport ndio tunapata HD murua
EPL kule kuna makampuni kama matano hv ndio wanafanya production, kuna sky sport, IMG - huyu ndio main production studio wa EPL, kuna BT na nyingine nimezisahau, hao wamegawana idadi ya mechi ila kwa bongo ndio hvy Azam anafanya mechi zote pekee yake.

KWA HAPA BONGO NAMKUBALI AZAM TV TOFAUTI NA DSTV KWA SABABU ZIFUATAZO.

Azam ameifikisha ligi mbali mno, ndio mana kuna wachezaji wa kawaida huko Afrika Magharibi wanatamani kuja kupata ukubwa huku Tanzania kupitia simba na Yanga baada ya hapo wakishakuwa wakubwa wakimbie ligi.

Hapa Afrika nadhani n nchi kama tano tuu ndio wanaonyesha mechi zote za ligi kuu live akiwemo Azam, kwa ligi ya bongo Dstv alitaka mechi za Simba na Yanga tuu.

Klabu, TFF na makampuni ya kibiashara yangekosa pesa kutoka dstv mana wao wangekuwa hawaonyeshi baadhi ya mechi, tofaut na Azam anarusha mechi zote hivyo watu wanapata pesa.


Eh nimechoka kuandika ila wakuu, Azam anazingua kwenye hizo ligi nyngn ila kwa ligi ya bongo aisee tumpe maua yao hata kama production ya mechi ndogo anafanya kama vile wanalazimishwa πŸ˜‚
 
Sasa kuna shida gani akirusha mechi za simba na yanga tu, na kuna ulazima gani wa kurusha mechi ndogo ambazo hazina watazamaji wengi, au sheria ndio zinataka hivyo kwamba ukichagua ligi fulani basi ni lazima urushe mechi zote za hiyo ligi
Mh mkuu, em tufanye ww ndio unatoa kibali.

Anakuja Azam anatoa 50B anaonyesha mechi zote.
Anakuja dstv anatoa 50B anaonyesha mechi za Simba na Yanga tuu.

Wewe utampa kibali nani?
 
Azam kamwaga pesa mzee wangu, hata team wakionyeshwa utendaji kazi utakavyokuwa kwenye ligi kati ya Azam na dstv na wakiulizwa wanamtaka nani kati yao watasema wanamtaka Azam πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…