Nani alimchagua kuwa mlinzi wa amani duniani? Au alijichagua mwenyewe?
Kwa taarifa yako Mwamerika ni mvurugaji mkuu wa amani duniani kwa masilahi ya taifa lake. Hayo tunayoyashudia au tuliyashuhudia huko Syria, Libya, Iran, Iraki, Misiri, Palestina, Israel, Afghanistan, Pakistan, North Korea nk - kote ni mkono wa Mwamerika. Lengo lake ni mafuta ya waarabu anataka yaendelee kuwa yake, maliasili za waafrika na wengineo duniani anataka ziendelee kuwa mali yake. Kwenye chaguzi kuu kama hizi duniani kwake huwa ndiyo fursa nzuri ya kupenyeza vibaraka wake. Ndiyo maana bunge la Amerika huwa linazifuatilia kwa karibu. Na Tanzania katuwekea vibaraka wake katika uchaguzi huu, wakisimamiwa na akina Robertson wanaojiita mawakili wa dunia! Lazima tuwe waangalifu. Tarehe 28 Oktoba tuwashikishe adabu.
Mwamerika ni mbabe wa dunia. Kiboko chake ni Mrusi na Mchina.