Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Hapana hata kidogo Marekani hawa kutawaliwa na Malkia bali walikuwa watawala na walipigana sambamba na mwingireza kuwaondoa wahindi wekundu, hii ilikuwa hatua ya pili baada ya kuichukua nchi..Sisi tuliupata Uhru wetu kutoka kwa wageni waliotutawala tofauti kabisa na wao ambao walikuwa ndio wageni walioitawala nchi hiyo. Kilichotokea tu ni kwamba hawakutaka tena kurudi kwao wala kutambulika kama waingereza bali WATU wa taifa jipya.
Pili, Walipoitangaza nchi yao na kuweka Azimio hilo ndilo lililojenga katiba na sheria, lengo likiwa kuwa guide wananchi ktk sheria na Political culture. Hivyo utunzi wa katiba hii ni technical kama unavyotumia vitabu vya elimu kujielelimisha haina maana unaiga bali unaelimika. Hakuna kitu kuiga ktk ELIMU bali unapanua fikra zako ktk kuitambua dunia iliyokuzunguka na sii wewe na who U are isipokuwa elimu inatuelimisha kwamba kuna watu kama wewe na ktk mazingira tofauti ambayo tutakuja kabiliana nayo. Na unaposema Mfumo mzima wa Elimu ni wa Muingereza hata sikuelewi maana utaanza hata kusema hata nguo tunazovaa ni za muingereza hivyo hakuna kosa kuwa waingereza - Sijui kama hii ndio maana yako!
Hawa viongozi wetu ni watumwa wa akili na pengine athari za utumwa ndio hizi tunazoziona, haikatazwi kuweka malengo ya kufikia kuendesha magari hayo isipokuwa kinachokatazwa ni ULIMBUKENI, Wamarekani wenyewe wanaita WONNA BE.. kwa maana kwamba wonna be are those who act and live like someone else they aren't!. Hawa wanaishi ktk dunia ya kusadikika ndio kina sisi, Lakini haina maana U can't be that person in terms of his/her success. Na hapa ndipo wengi wanaposhindwa kuelewa kwamba WATU hawawezi kubadilika! lakini wanaweza badilisha utawala na mazingira yao - LIBERTY. Kama unakumbuka niliwahi kukwambia kwa mtoto anayewezka azimio la kuwa daktari akikua hana ujinga wa kuiga pindi anapoenda shule kwa malengo ya kufikia azma hiyo, tofauti na wale wanaojiita madaktari ilihali wamepachikwa ujinga fulani - kina fulani. Kwa jinsi tunavyoendesha nchi yetu leo hii ni ulimbukeni mtupu yaani wonna bees kujivika nguo za Michael Jackson ili dunia ituone tunafanana naye..Hii inatokana na kupoteza dira yetu sisi wenyewe..
Mkandara,
Unaposema tumepoteza dira yetu. Umepoteza na nani? Je ni dira gani hiyo? Au mwenzetu ni magamba? Au CCM. Azimio la Arusha ni document ya TANU na baadaye CCM.
Mimi sifuati chama chochote cha siasa na kwanini unaniingiza kwenye upotevu wa dira ya chama cha siasa? Au mwenzetu bado hupo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Naona sasa hata watu wa CHADEMA, CUF, TLP wanalazimishwa? Unazungumza LIBERTY na unakuwa wa kwanza kuikiuka, typical of tyranny of majority.