Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Hapana hata kidogo Marekani hawa kutawaliwa na Malkia bali walikuwa watawala na walipigana sambamba na mwingireza kuwaondoa wahindi wekundu, hii ilikuwa hatua ya pili baada ya kuichukua nchi..Sisi tuliupata Uhru wetu kutoka kwa wageni waliotutawala tofauti kabisa na wao ambao walikuwa ndio wageni walioitawala nchi hiyo. Kilichotokea tu ni kwamba hawakutaka tena kurudi kwao wala kutambulika kama waingereza bali WATU wa taifa jipya.

Pili, Walipoitangaza nchi yao na kuweka Azimio hilo ndilo lililojenga katiba na sheria, lengo likiwa kuwa guide wananchi ktk sheria na Political culture. Hivyo utunzi wa katiba hii ni technical kama unavyotumia vitabu vya elimu kujielelimisha haina maana unaiga bali unaelimika. Hakuna kitu kuiga ktk ELIMU bali unapanua fikra zako ktk kuitambua dunia iliyokuzunguka na sii wewe na who U are isipokuwa elimu inatuelimisha kwamba kuna watu kama wewe na ktk mazingira tofauti ambayo tutakuja kabiliana nayo. Na unaposema Mfumo mzima wa Elimu ni wa Muingereza hata sikuelewi maana utaanza hata kusema hata nguo tunazovaa ni za muingereza hivyo hakuna kosa kuwa waingereza - Sijui kama hii ndio maana yako!

Hawa viongozi wetu ni watumwa wa akili na pengine athari za utumwa ndio hizi tunazoziona, haikatazwi kuweka malengo ya kufikia kuendesha magari hayo isipokuwa kinachokatazwa ni ULIMBUKENI, Wamarekani wenyewe wanaita WONNA BE.. kwa maana kwamba wonna be are those who act and live like someone else they aren't!. Hawa wanaishi ktk dunia ya kusadikika ndio kina sisi, Lakini haina maana U can't be that person in terms of his/her success. Na hapa ndipo wengi wanaposhindwa kuelewa kwamba WATU hawawezi kubadilika! lakini wanaweza badilisha utawala na mazingira yao - LIBERTY. Kama unakumbuka niliwahi kukwambia kwa mtoto anayewezka azimio la kuwa daktari akikua hana ujinga wa kuiga pindi anapoenda shule kwa malengo ya kufikia azma hiyo, tofauti na wale wanaojiita madaktari ilihali wamepachikwa ujinga fulani - kina fulani. Kwa jinsi tunavyoendesha nchi yetu leo hii ni ulimbukeni mtupu yaani wonna bees kujivika nguo za Michael Jackson ili dunia ituone tunafanana naye..Hii inatokana na kupoteza dira yetu sisi wenyewe..


Mkandara,

Unaposema tumepoteza dira yetu. Umepoteza na nani? Je ni dira gani hiyo? Au mwenzetu ni magamba? Au CCM. Azimio la Arusha ni document ya TANU na baadaye CCM.

Mimi sifuati chama chochote cha siasa na kwanini unaniingiza kwenye upotevu wa dira ya chama cha siasa? Au mwenzetu bado hupo kwenye mfumo wa chama kimoja?

Naona sasa hata watu wa CHADEMA, CUF, TLP wanalazimishwa? Unazungumza LIBERTY na unakuwa wa kwanza kuikiuka, typical of tyranny of majority.
 
- Kwani lini huko nyuma Viongozi wetu waliwahi kuwajibika under Azimio la Arusha?

W. J. Malecela. You are old enough to know about uwajibikaji during Mwalimu's era.

Kuomba omba nje tulianzia kwenye awamu ya kwanza sio leo tu,

Unaongelea kuomba kwa namna gani? Kweli kama Tanzania under Mwalimu ingekuwa inaomba kwa namna unavyotaka kuniaminisha, Mwalimu angekuwa na guts za kupingana waziwazi na hao "wakubwa"? Mwalimu alitaka kuitoa TZ kwenye Commonwealth kama Uingereza ingekubali Apartheid South Africa kuwa mwanachama. Mifano mingine unaifahamu. Angalia hali ilivyo sasa,taifa halina kauli tena katika anga za kimataifa,kisa kuna "wakubwa" watanuna.

Viongozi wabovu tulionao ni tatizo la wananchi tunaowachagua.

Hapa Le Mutuz,sijakuelewa. Wananchi ndiyo wenye makosa kuchagua viongozi wabovu au? Sio mfumo wa kuchagua viongozi hao ndiyo mbovu,kiasi kwamba viongozi wabovu wanachaguliwa? Suala la rushwa? Kutowajibika kwa vyombo vinavyosimamia chaguzi? Siasa kugeuzwa biashara? Hayo yote yalizingatiwa na azimio katika kuweka haki na usawa ili kupata viongozi bora.

mengine tumeyarithi toka wamu ya kwanza hakuna mapya hapa!

Mkuu,tumeyarithi sawa,sasa hayo "maazimio" yako yamefanya nini kuyaondoa hayo matatizo? Hauoni kama hayo maazimio nayo ni failed theories? Maana sijaona success stories ya hayo unayoyasimamia.

. Lakini muhimu ni kwamba hatuwezi kulirudia Azimio la Arusha tena maana limetuletea maafa makubwa sana!

William.

Maafa yapi Willie? Maafa kwa misingi ipi? What is the basis for such a sweeping statement?
 
Unaongelea kuomba kwa namna gani? Kweli kama Tanzania under Mwalimu ingekuwa inaomba kwa namna unavyotaka kuniaminisha, Mwalimu angekuwa na guts za kupingana waziwazi na hao "wakubwa"? Mwalimu alitaka kuitoa TZ kwenye Commonwealth kama Uingereza ingekubali Apartheid South Africa kuwa mwanachama. Mifano mingine unaifahamu. Angalia hali ilivyo sasa,taifa halina kauli tena katika anga za kimataifa,kisa kuna "wakubwa" watanuna.?

Nzi,

Kwa data zilizopo, Tanzania ilikuwa inaongoza (au miongoni mwa nchi zinazoongoza) kwa kupokea misaada kwa nchi za kiafrika zilizopo chini ya jangwa la Sahara. Hilo halina ubishi.

Tofauti na viongozi wangine wa kiafrika, mwalimu aliitumia misaada kwa nia nzuri. Kwa upande mwingine alifanya viongozi wetu wasiwajibike katika kujenga capabilities za kujitegemea ambazo ni msingi ya Azimio la Arusha.
 
- Bob wacha haya mambo ya kitoto, kama umeishiwa hoja haina tatizo kukaa pembeni kuliko kukoseana heshima hivi wakati mimi na wewe ni close people, I mean ate the end of the day hii ni siasa yaani kwa sababu wewe hukubaliana hoja na mimi ndio unakuwa umechanganyikiwa nianze kukutafuta?

Vipi bob mbona unashuka sana mkuu? kama huna hoja kwani ni lazima uchangie mkuu?

William.
Niliyasema yanauma sana na nilitaka sana ufahamu hivyo maana sikutegemea kusikia vitu hivi toka kwako hata kidogo..Wewe ni Azimio la Arusha lililokukuza hadi umefikia leo kugombea ubunge leo unaliponda bro, kusema kweli ikifikia mimi kuanza kuropoka vitu vya ajabu kama hivi inabidi unitafute haijalishi niko ktk hai gani maana uzima wa mwili hauna maana yoyote ikiwa naanza kuchanganyikiwa...

Trust me, unachoandika hata hakieleweki, mara upinge miiko wakati unaitaka sheria, mara sijui mambo ya UN na Jefferson yaani hata sikuelewi elewi vile..Utanisamehe lakini sintokuacha japokuwa hupendi nayoandika.
 
- Mkuu Jasusi, heshima yako sana America kuna sheria, hakuna miiko ya uongozi you know better huko taifa huongozwa kwa sheria, matatizo ya Clinton na Monica yalitatuliwa na sheria sio miiiko ya uongozi, hapana!

- Kenya wamekwua mabepari kwa muda mrefu kuliko sisi, ndio maana wana viwanda vingi kuliko sisi na pesa yao ni kubwa kuliko yetu, na pia Watalii wanawajali wao kuliko sisi, yaaani haya hata bila shule yanaeleweka sana kuwa ni matunda ya ubepari!

William.

[SIZE=+1]Code of Ethics for U.S. Government Service
[/SIZE]

[SIZE=-1]Adopted July 11, 1958 [/SIZE]

Resolved by the House of Representatives {the Senate concurring}, That it is the sense of the Congress that the following Code of Ethics should be adhered to by all Government employees, including officeholders. CODE OF ETHICS FOR GOVERNMENT SERVICE

Any person in Government service should:

1. Put loyalty to the highest moral principals and to country above loyalty to Government persons, party, or department.
2. Uphold the Constitution, laws, and legal regulations of the United States and of all governments therein and never be a party to their evasion.
3. Give a full day's labor for a full day's pay; giving to the performance of his duties his earnest effort and best thought.
4. Seek to find and employ more efficient and economical ways of getting tasks accomplished.
5. Never discriminate unfairly by the dispensing of special favors or privileges to anyone, whether for remuneration or not; and never accept for himself or his family, favors or benefits under circumstances which might be construed by reasonable persons as influencing the performance of his governmental duties.
6. Make no private promises of any kind binding upon the duties of office, since a Government employee has no private word which can be binding on public duty.
7. Engage in no business with the Government, either directly or indirectly which is inconsistent with the conscientious performance of his governmental duties.
8. Never use any information coming to him confidentially in the performance of governmental duties as a means for making private profit.
9. Expose corruption wherever discovered.
10. Uphold these principles, ever conscious that public office is a public trust.

[Source: U.S. House of Representatives Ethics Committee
]
 
Mkandara,

Unaposema tumepoteza dira yetu. Umepoteza na nani? Je ni dira gani hiyo? Au mwenzetu ni magamba? Au CCM. Azimio la Arusha ni document ya TANU na baadaye CCM.

Mimi sifuati chama chochote cha siasa na kwanini unaniingiza kwenye upotevu wa dira ya chama cha siasa? Au mwenzetu bado hupo kwenye mfumo wa chama kimoja?

Naona sasa hata watu wa CHADEMA, CUF, TLP wanalazimishwa? Unazungumza LIBERTY na unakuwa wa kwanza kuikiuka, typical of tyranny of majority.

Ukitazama Azimio la Arusha kama ni sera ya TANU/CCM, ina maana unaanzisha mjadala mpya kabisa kwa maana kwamba mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ulihitaji kwenda sambamba na kitu kipya kabisa nje ya azimio la arusha? Je unataka kutuaminisha kwamba mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na Azimio la Zanzibar mwaka 1992 did not happen by coincidence? Kwa sababu ni dhahiri kwamba tangia kufutwa kwa azimio la arusha, hakuna sera yoyote ya kitaifa ambayo inatokana na self - determination juu ya wapi tunataka kwenda na tufanye nini kufika huko, kinachoendelea tangia kipindi hicho ni utekelezaji wa sera za soko huria kiholela huku WorldBank, IMF waki determine our future. Inawezekana sijaeleweka vyema lakini ni kutokana na kuchanganywa kidogo na hoja yako inayoashiria Azimio la Arusha should remain as a partisan issue. The bottom line is - Ukoloni ulitugawanya, Azimio la arusha pamoja na mapungufu yake likalenga kuturudisha kundini bila ya kujali dini, kabila, au tofauti za kisiasa, at least for a little while. Otherwise kama nchi ilikuwa imegawanyika kisiasa wakati wa harakati za ukombozi, uhuru usinge patikana kwani mkoloni ange capitalize on divide and rule principle.

Je ni wapi kuna ushahidi kwamba wananchi walilazimishwa ujamaa? na kwanini waukatae wakati ule wakati hivyo ndivyo wali ishi kabla ya ujio wa mkoloni? kwani ujamaa simply means undugu/familyhood tofauti na wachache wanavyojaribu kuharibu maana yake halisi. Leo hii kuna mwanachama wa TLP, CHADEMA n.k kweli ambae akieleweshwa maana ya ujamaa atapingana nao? hata wafaransa kwenye uchaguzi mkuu juzi wamechagua chama cha kijamaa, na ni dhahiri kitashinda kwenye second run-off. Tujiulize, kwanini? Jibu nikwamba now wapo in crunch times, of which sisi tumekuwa for decades. Hata marekani kwa mfano, tunashuhudia jinsi gani wananchi wanavyo adopt into undugu wakati wa matatizo ya kiuchumi, natural disasters, man-made disasters n.k.

Ubepari na soko huria ni vitu vizuri na havina mbadala wa asilimia mia, lakini ni muhimu tukavifuata hatua kwa hatua using a bottow-up approach, sio top-bottom kama sasa. Ujamaa wa kidemokrasia ni moja ya best options for us Tanzania kwani una heshimu na kuvumilia ubepari as long as ubepari una heshimu na kuvumilia ujamaa. Ndio maana Sweden walitusaidia sana wakati wa ujamaa kuliko taifa lolote.
 
[SIZE=+1]Code of Ethics for U.S. Government Service [/SIZE]

[TD="bgcolor: #cc0000, colspan: 2"]
[/TD]
[SIZE=-1]Adopted July 11, 1958 [/SIZE]
Resolved by the House of Representatives {the Senate concurring}, That it is the sense of the Congress that the following Code of Ethics should be adhered to by all Government employees, including officeholders. CODE OF ETHICS FOR GOVERNMENT SERVICE

[Source: U.S. House of Representatives Ethics Committee
]
Kobello,
Umefunga mjadala juu ya miiko. Kumbe Marekani wana miiko. Ni mleta mada tu ndiye alikuwa halijui hilo.
 
Mkandara,

Unaposema tumepoteza dira yetu. Umepoteza na nani? Je ni dira gani hiyo? Au mwenzetu ni magamba? Au CCM. Azimio la Arusha ni document ya TANU na baadaye CCM.

Mimi sifuati chama chochote cha siasa na kwanini unaniingiza kwenye upotevu wa dira ya chama cha siasa? Au mwenzetu bado hupo kwenye mfumo wa chama kimoja?

Naona sasa hata watu wa CHADEMA, CUF, TLP wanalazimishwa? Unazungumza LIBERTY na unakuwa wa kwanza kuikiuka, typical of tyranny of majority.
Mkuu wangu kwani Jefferson alipoandika Declaration of Independence hakuwa na chama? Je, walikuwa democratic au labda soma hapa Na Je, mabadiliko yoyote yalibadilisha declaration of Independnce?
Mbona hata sikuelewi elewi vile, maana tulikuwa na chama kimoja hii haina maana Azimio lile halingeweza kufikiwa kaa tungekuwa na vyama vingine.. Kumbuka tu Azimio litu lililenga kuwabadilisha watu sio vitu mnachotazama nyie ni kubadilisha vitu ili watu wafaidike na hiyo concept ndio inapingana na Azimio lile. Makosa ya kiutendaji hayawezi kuondoa ukweli wa dhamira ya Azimio la Arusha na hata wewe leo unapinga Technicality tu..lakini bado unaamini vitu vyote vilivyoorodheshwa..

Yesu wakati anaondoka alikuwa na wafuasi chini ya 20, leo hii tuna waumini zaidi ya billioni nne na hata kama ni asilimia 20 tu ndio wanasali na kufuata mafundisho yake haina maana he failed. Wewe ndiye ulofail kutoweza kuokoka wakati maandishi yapo kukuelekeza.

Nakuomba kalisome tena Azimio la Arusha na pengine sukutua na mawaidha ya mwalimu bofya halafu tutaendelea kutazama wapi tulikosea lakini sintokubali kabisa kwamba malengo ya azimio lile yalikuwa na makosa, unless wewe ni kizazi kipya mlokuta kina Mengi na Lowassa matajiri.
 
Ukitazama Azimio la Arusha kama ni sera ya TANU/CCM, ina maana unaanzisha mjadala mpya kabisa kwa maana kwamba mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ulihitaji kwenda sambamba na kitu kipya kabisa nje ya azimio la arusha? Je unataka kutuaminisha kwamba mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na Azimio la Zanzibar mwaka 1992 did not happen by coincidence? Kwa sababu ni dhahiri kwamba tangia kufutwa kwa azimio la arusha, hakuna sera yoyote ya kitaifa ambayo inatokana na self - determination juu ya wapi tunataka kwenda na tufanye nini kufika huko, kinachoendelea tangia kipindi hicho ni utekelezaji wa sera za soko huria kiholela huku WorldBank, IMF waki determine out future. Inawezekana sijaeleweka vyema lakini ni kutokana na kuchanganywa kidogo na hoja yako inayoashiria Azimio la Arusha should remain as a partisan issue.


Azimio la Zanzibar na vyama vingi didn't happen by coincidence. Wakati wa mfumo wa chama kimoja, wasomi wengi na watu wenye professional zao za maana hawakujiingiza sana kwenye nafasi za kisiasa.

Na vilevile kulikuwana watu ambao walifanya kazi kwenye mashirika kimataifa au kwenye ofisi za ubalozi ambao wajiwekezea nyumba au miradi. Kulikuwa na wafanyabiashara. Vilevile kulikuwa na wataalamu walioanzisha shughuli zao binafsi. Watu hawa wasingebaki CCM.

Kwa mfano. Salimu Ahmed Salimu alikaa nje miaka mingi. Je pesa alizozipata nje kihalali alitakiwa azifanyie nini? Kwa mujibu wa Azimio la Arusha, akizitumia pesa hizo kuwekeza tayari atakuwa amevunja masharti ya uongozi.

Vilevile wakati viongozi wengi walikuwa na mali zilizokuwepo kwenye majina ya ndugu zao. Hivyo vyama vingi vingewafanya watu wajiunge na vyama vingine bila kupata matatizo yoyote yale kwani kanuni za Azimio la Arusha zilikuwa sio sheria za nchi.

Self determination is illusive quest na huwezi kuipata kwa maazimio na maandamano. Kwa nchi masikini kama Tanzania, self determination ni suala la kutumia taaluma na nidhamu ya juu sana.
 
- Again sina shida ya kusoma Azimio ambalo nimembishwa kwa nguvu maisha yangu yote ya utotoni hapa bongo, Jefferson Declaration ilikuwa inagusia sana kuondolewa utumwa kumbuka Jefferson alikuwa na fuatilia sana siasa za kukataa utumwa za France ambazo alijua kuwa zipo njiani kwenda US with the fact kwamba mazungumzo ya UN yalikuwepo tayari. Lincoln alipoamua kutekeleza maazimio ya Jefferson, ikatokea a Civil War lakini in the end mawazo ya Jefferson yakashinda utumwa ukaisha,

- Sisi wananchi wakahamishwa kwenye miji yao kwa nguvu kutekeleza maazimio ya Arusha, matokeo wengi wao wakapoteza maisha yao lakini results mpaka leo hakuna!

- Sihitaji u-intelect wa kusoma Azimio maana it was designed kupumbaza na usiulize faida wala hasara zake, ama sivyo unawekwa rumande, kweli ulitegemea mimi niisome hiyo kitu ambayo imetufikisha hapa taifa letu hatujijui tunatoka wapi wala tunakokwenda, pleasee!

William.

Hapana, Jefferson hawezi kupewa sifa zozote kwa juhudi za kuondoa utumwa. Yeye alijikita zaidi kwa maslahi ya wazungu. Kumbuka ni wewe hapa umetufahamisha kwamba alipokuwa anatunga declaration alikuwa na watumwa. Wakati huo weusi hawakuwa full humans kwa macho ya wazungu. Ni kweli aliguswa na kanuni za Ufaransa za liberte et egalite, uhuru na usawa lakini hii haiku apply kwa weusi. Na Lincoln, alipopigana kulinda muungano alikuwa hatekelezi maazimio ya Jefferson. It was simply common sense. The south wanted to break away to continue with slavery na walikuwa na jeshi lao na nchi isingeweza kuendelea kukiwa na confederates na jeshi la taifa ( northerners.) Umerudia tena kuwa kuna wananchi waliopoteza maisha yao katika uhamiaji wa vijijini lakini hujatuambia ni akina nani na wapi. Bila kutoa ushahidi tutakuona kwamba wewe ni muongo na mtu mwenye chuki tu juu ya azimio. Kama azimio limetupumbaza, kwa nini tunalalamikia madudu wanayofanya akina Kikwete na Mkapa? Kwa sababu azimio lilitupa matumaini ya liberte et egalite.
Leo Tanzania egalite hakuna. Kuna tabaka la watawala ambalo naona kila mtu analikimbilia kwa kuwania ubunge ili waweze kuitafuna nchi. Hapana azimio lilitufungua macho na ndiyo sababu tunawapigia kelele wale ambao leo wameua azimio ili waitafune nchi yetu mchana kweupe. Kama wewe hujui unakotoka na unakokwenda, speak for yourself. Sisi wengine tumeshaona the promised land na tumaanini, we will get there.
 
Mkuu wangu kwani Jefferson alipoandika Declaration of Independence hakuwa na chama? Je, walikuwa democratic pia labda soma hapa Mbona hata sikuelewi elewi vile, maana tulikuwa na chama kimoja hii haina maana Azimio lile halingeweza kufikiwa kaa tungekuwa na vyama vingine.. Kumbuka tu Azimio litu lililenga kuwabadilisha watun na sio vitu mnachotazama nyie ni kubadilisha vitu ili watu wafaidike na hiyo concept ndio inapingana na Azimio lile. Makosa ya kiutendaji hayawezi kuondoa ukweli wa dhamira ya Azimio la Arusha na hata wewe leo unapinga Technicality tu..lakini bado unaamini vitu vyote vilivyoorodheshwa..

Yesiu wakati anaondoka alikuwa na wafuasi chini ya 20 leo hii tuna waumini zaidi ya billioni nne na hata kama ni asilimia 20 tu ndio wanasali na kufuata mafundisho yake haina maana he failed. Wewe ndiye ulofail kutoweza kuokoka wakati maandishi yapo ya kukuelekeza.

Nakuomba kalisome tena Azimio la Arusha na pengine ksukutua na mawaidha ya mwalimu bofya halafu tutaendelea kutazama wapi tulikosea lakini sintokubali kabisa kwamba malengo ya azimio lile yalikuwa na makosa, unless wewe ni kizazi kipya mlokuta kina Mengi na Lowassa matajiri.

Mkandara,

Kulikuwa hakuna political parties wakati declaration linaandikwa. Lakini alikuwa ni mwanzilishi wa political party. Baada ya uhuru kulikuwa na kundi linalotaka federal government kuwa na nguvu kubwa kuliko majimbo. Na kuna waliotaka majimbo yawe na uhuru.

Yeye alikuwa kwenye kundi la majimbo. Na mpinzani wake wa kifalsafa Alexander Hamilton alikuwa kwenye federalist. Na soma mabadilishano yao ya barua na jinsi gani walivyoheshimu michango ya wenye mawazo tofauti.

Sio hapa kulikataa Azimio la Arusha, tayari makombora ya matusi yanakufuata. Bado tupo nyuma sana kwenye age of renaissance.
 
Kobello,
Umefunga mjadala juu ya miiko. Kumbe Marekani wana miiko. Ni mleta mada tu ndiye alikuwa halijui hilo.

Jasusi,

Kama nilivyoeleza mwanzo. Katiba ya nchi haitakiwi kuwa na code of ethics. Kwa sababu zinabadilika badilika. Code of ethics ziwe kwenye sheria za nchi au kanuni za kazi za sehemu husika. Pamoja na hayo bado kuna watu wanaotaka mabadiliko ya kikatiba yajumlishe kanuni za uongozi zilizo kwenye Azimio la Arusha.

Kama zinatakiwa basi zipitishwe bungeni na kujadiliwa kama miswada mingine. Na sio kukurupuka tu. Mwishowe wasukuma watachomoa utamaduni na jadi zao na kutaka ziwe code of ethics.
 
Jasusi,

Kama nilivyoeleza mwanzo. Katiba ya nchi haitakiwi kuwa na code of ethics. Kwa sababu zinabadilika badilika. Code of ethics ziwe kwenye sheria za nchi au kanuni za kazi za sehemu husika. Pamoja na hayo bado kuna watu wanaotaka mabadiliko ya kikatiba yajumlishe kanuni za uongozi zilizo kwenye Azimio la Arusha.

Kama zinatakiwa basi zipitishwe bungeni na kujadiliwa kama miswada mingine. Na sio kukurupuka tu. Mwishowe wasukuma watachomoa utamaduni na jadi zao na kutaka ziwe code of ethics.

Hii topic nimeingia nikiwa nimechelewa sana, kwa hiyo itanichukua muda kidogo ku-catch up. Ila siyo kweli kuwa katiba haitakiwi kuwa na code of ethics eti kwa vile zinabadilika kila wakati kwani hata Katiba ina amendments nyingi. Kwa hiyo kubadilika kwa code of ethics kunaweza kuwa reflected kwenye hizo amendments.
 
Niyasema yanauma sana na nilitaka sana ufahamu hivyo maana sikutegemea kusikia vitu hivi toka kwako hata kidogo..Wewe ni Azimio la Arusha lililokukuza hadi umefikia leo kugombea ubunge leo unaliponda bro, kusema kweli ikifikia mimi kuanza kuropoka vitu vya ajabu kama hivi inabidi unitafute haijalishi niko ktk hai gani maana uzima wa mwili hauna maana yoyote ikiwa naanza kuchanganyikiwa... Trust me, unachoandika hata hakieleweki, mara upinge miiko wakati unaitaka sheria, mara sijui mambo ya UN na Jefferson yaani hata sikuelewi elewi vile..Utanisamehe lakini sintokuacha japokuwa hupendi nayoandika.

- Bob kila ninachokisema unakielewa isipokuwa kwa vile sikubaliani na mawazo yako basi ninakwua nimechanganyikiwa, ndio maana mimi huwa ninakuwa muangalifu sana na marafiki uchwara, Bob mimi kuwa rafiki na wewe sio lazima tukubaline kila kitu, Mwenyekiti Mao alisema ukiona watu wawili wanakubaliana kwa kila kitu kwa wakati wote ujue either mmoja wao ni mgonjwa au wote wawili wagonjwa, ninafurahi kwamba hapa umenionyesha what kind of friend you are unategm,ea usichotaka wewe na mimi pia nifuate mkumbo, unachoataka as well hapana siko kihivyo bro!

- Azimio ni kweli limenisomesha, lakini haina maana halina mapungufu, na kwamba siruhusiwi kuyasema wazi, unanikumbusha zile enzi ukiuliza tu kuhusu Azimio unafukuzwa nchi au unakuwa mhaini, kumbe wenye that kind of thinking mlikuwa wengi sana, sasa tupo huru tunauliza bado unajaribu kulazimisha kwa nguvu tu kwamba Azimio was great, Bob nitakwambia tatizo kubwa la ulevi huwa ni vigumu sana mlevi kukubali amelewa, infact ataita wengine kwua ndio walevi, so is kuchanganyikiwa ni rahisi sana kwa aliyechanganyikiwa kuona wengine ndio, wakati ukweli ni kwamba ni yeye ndiye mwenye kuchanganyikiwa. So is kuropoka nayo ni rahisi sana kuwahisi wengine wanaropoka na hasa kama hawakubaliani na mawazo yako tu!

- Kuhusu Jefferson, nimesema very clear kwamba Declaration aliyoitoa, ilijali sana kuwepo kwa mazungumzo ya UN kule NYC, na pia by origin Jefferson asili yake ilikuwa ni France, ambako kulikuwa na vugu vugu kubwa la kukataa utumwa, DEclaration aliyoiandika ilijali hayo na pia hata alipofariki, huku nyuma ilikuwa bado inatekelezeka na nido maana Lincoln akaweza kuitekeleza lakini kwa kupitia The American Civil War, ambapo wananchi wengi sana walimwaga damu, sasa sisi katika kutekeleza Azimio, wananchi wengi walipoteza maisha wakati wa kuhamishwa, lakini matokeo yamekuwa zero! WHY? Ni kwa sababu Azimio lilikuwa halitekelezeki na mpaka leo huwezi kulitekeleza!

- Sipo hapa kusameheana na mtu yoyote, na I could careless isipokuwa nipo hapa kukata ishus muhimu kwa taifa, whatever you write ni haki yako na mimi pia ni haki yangu, tupingane kwa hoja, lakini kuingiliana binafsi ni kukosa hoja, ninarudia tena kwamba Azimio la Arusha ndio chanzo cha umasikini wetu, na ndio chanzo cha matatizo yetu kiuchumi, sasa tuachane nalo tusonge mbele na Ubepari kama tulionao sasa!

William.
 
Hii topic nimeingia nikiwa nimechelewa sana, kwa hiyo itanichukua muda kidogo ku-catch up. Ila siyo kweli kuwa katiba haitakiwi kuwa na code of ethics eti kwa vile zinabadilika kila wakati kwani hata Katiba ina amendments nyingi. Kwa hiyo kubadilika kwa code of ethics kunaweza kuwa reflected kwenye hizo amendments.

- Mwalimu Kichuguu, be careful unapo-deal na watu wenye akili timamua maana unaweza kuwa unasema usichokisema, honestly hakuna aliyekuuliza kama ulikuwepo au hukuwepo, muhimu ni una hoja gani on the ishu!

- Taifa linatakiwa kuendeshwa na Katiba tu ya jamhuri, anything else lile taifa litaingia matatizo tu kama yetu, tunawauliza hizo miiiko ya uongozi Tanzania iliwahi kumbana kiongozi gani wa juu?

William.
 
Hapana, Jefferson hawezi kupewa sifa zozote kwa juhudi za kuondoa utumwa. Yeye alijikita zaidi kwa maslahi ya wazungu. Kumbuka ni wewe hapa umetufahamisha kwamba alipokuwa anatunga declaration alikuwa na watumwa. Wakati huo weusi hawakuwa full humans kwa macho ya wazungu. Ni kweli aliguswa na kanuni za Ufaransa za liberte et egalite, uhuru na usawa lakini hii haiku apply kwa weusi. Na Lincoln, alipopigana kulinda muungano alikuwa hatekelezi maazimio ya Jefferson. It was simply common sense. The south wanted to break away to continue with slavery na walikuwa na jeshi lao na nchi isingeweza kuendelea kukiwa na confederates na jeshi la taifa ( northerners.) Umerudia tena kuwa kuna wananchi waliopoteza maisha yao katika uhamiaji wa vijijini lakini hujatuambia ni akina nani na wapi. Bila kutoa ushahidi tutakuona kwamba wewe ni muongo na mtu mwenye chuki tu juu ya azimio. Kama azimio limetupumbaza, kwa nini tunalalamikia madudu wanayofanya akina Kikwete na Mkapa? Kwa sababu azimio lilitupa matumaini ya liberte et egalite.
Leo Tanzania egalite hakuna. Kuna tabaka la watawala ambalo naona kila mtu analikimbilia kwa kuwania ubunge ili waweze kuitafuna nchi. Hapana azimio lilitufungua macho na ndiyo sababu tunawapigia kelele wale ambao leo wameua azimio ili waitafune nchi yetu mchana kweupe. Kama wewe hujui unakotoka na unakokwenda, speak for yourself. Sisi wengine tumeshaona the promised land na tumaanini, we will get there.

1. Kwenye Declaration Jefferson aliongea sana kuhusu utumwa kwamba ni dhambi, Lincoln amekubali sana kwenye speech zake nyingi kwamba alikuwa inspired by Jefferson Declaration, katika kuuumaliza utumwa US.

2. Unasema aliguswa na France kutaka kutokomeza utumwa Duniani, lakini haiku-apply kwa weusi? Sasa ni wapi Wazungu walikuwa watumwa mkuu? Kwamba Jefferson ndio aliokuwa aakiwalilia? Kumbuka aliyeleta mambo ya Jefferson ni wewe mwenyewe sio mimi, maana siamini Azimio la Arusha lina anything to do na Jefferson, Declaration ni vitu viwili tofauti wala havifanani!, kwa sababu Declaration ilikuwa inatekelezeka, wakati Azimio halitekelezeki!

3. Unasema maamuzi ya Lincoln yalikuwa ni common sense, sasa ikawaje South wakawa hawana hiyo common sense? South simply hawakutaka kuona utumwa unaisha kwa sababu za kicuhumi zaidi, Northeast ilikuwa imejaa wageni wengi toka nje ya US ambao waliona utumwa umepitwa na wakati, ndio maana katika kutekeleza maanuzi mengi ambayo yalisemwa mapema na Jefferson, ikazuka Vita ya wenyewe kwa wenyewe, which is ok katika kutekeleza agenda za taifa, kitu ambacho sisi ilitushinda, hata China ilibidi wananchi wengi wapoteze masiha kwenye kutekeleza maamuzi magumu!

4. Sio siri kwamba wananchi wengi walipoteza masiha yao wakati wa Operations za Azimio za kuwahamisha kutoka kwenye miji yao na kuwapeleka kwenye vijiji vipya vya ujamaa, unaweza kukataa lakini ukweli upo wazi na unaeleweka, sina shida ya kusema uongo kwa kusingizia vifo vya wananchi ambavyo havikutokea that is very low for you think I would ever do such a thing, kama umeamua kwa sababu unapenda sana Azimio sasa hutaki kukubali kwamba kuna wananchi walikufa kwenye kuhamishwa hamishwa bila mpangilio na maamuzi ya Azimio la Arusha, it is up to you! Lakini records zipo wazi na walioshuduia wapo pia!

5. Mnalalamikia madudu ya wengine tu lakini ya awamu ya kwanza ambapo wengi wenu mlikuwa na masilahi sana hamtaki iguswe, mnalalamikia madudu kwa kulilia kurudia thoeries zilizoshindwa ndio wengine tunawashangaa sana kwamba vipi leo mwaka 2012 mtu kulilia thoery za Azimio ambazo ndio hasa zimelidumaza hili taifa? Kuona madudu ya wengine na kulilia old solutions ni tatizo zaidi kuliko tatizo la Azimio by it self, kwa sababu unakwua unaji-contradict kwamba huna idea kabisa na what is what!

6. Kuogembea ubunge ni haki ya kila wananchi wa Tanzania, anaruhusiwa kugombea kupitia Upinzani au CCM. Sasa dhana ya unayoisema kwamba wanagombea kwenda kula, inatokea wapi? Unsema kutafuta nafasi ya uwakilishi wa wananchi kwa taifa ni kutafuta kutafuna nchi? I mean au ukigombea CCM tu, lakini sio ukigombea kupitia Upinzani?

7. Taifa zima hatujui tunakotoka na wala tunakokwenda ndio maana tunalumbana hapa kujaribu kupata ukweli wa njia tuliyomo, sasa mnatokea watu kama wewe ambao mmenufaika weee na awamu ya kwanza ya madudu haya ya Azimio na kwa vile mlo umeisha mnataka kutudanganya kwamba Azimio lilikuwa sawa, sawa my fooot ni Azimio ndilo limetuletea matabaka nchi hii, toka enzi zile Azimio lilikuwa maneno matupu, kazi kuwaonea Viongozi waliolikataa, huku waliokulikubali kwa maneno tu wakineemeka, ndio maana Viongozi wenye akili sana wakaona dawa ni ku-level the field ili kila kiongozi naye anufaike na wananchi pia, sasa mnaanza kulia lia mnlia nini wakati mmenfuiaka nalo weee na awamu ya kwanza, hakumjua kwamba kuna siku itafika mwisho wananchi wataamuka na kutaka usawa? Ninasema time ni sasa, twende mbele na ubepari, wote tuwe sawa!

8. Well, if you can get there na Azimio good luck, lakini sisi wengine hasa mimi nimeshituka sana kwamba Azimio was nothing but a myth, na ndilo hasa limetufikisha hapa tulipo, tumekwama sasa mnakuja watu kama nyinyi ambao mnajua you cannot farewell kwenye Ubepari mnaanza kutulazimisha tukubali theories zilizoshindwa, hapana MUNGU AWABARIKI SANA WALIOLIUWA AZIMIO MAANA IT WAS A WASTE!

William.
 
Je ni wapi kuna ushahidi kwamba wananchi walilazimishwa ujamaa? na kwanini waukatae wakati ule wakati hivyo ndivyo wali ishi kabla ya ujio wa mkoloni? kwani ujamaa simply means undugu/familyhood tofauti na wachache wanavyojaribu kuharibu maana yake halisi. Leo hii kuna mwanachama wa TLP, CHADEMA n.k kweli ambae akieleweshwa maana ya ujamaa atapingana nao?

- Duh!

William.
 
Hii topic nimeingia nikiwa nimechelewa sana, kwa hiyo itanichukua muda kidogo ku-catch up. Ila siyo kweli kuwa katiba haitakiwi kuwa na code of ethics eti kwa vile zinabadilika kila wakati kwani hata Katiba ina amendments nyingi. Kwa hiyo kubadilika kwa code of ethics kunaweza kuwa reflected kwenye hizo amendments.


Mkuu Kichuguu,

Ni kweli katiba inaweza kuwa na code of ethics, na kufanyiwa amendments. Lakini sifa ya katiba ni kuwa kitabu kifupi chenye kuwezesha watu wote kukielewa haki zao na muundo wa shughuliza za kiserikali.

Sifa nyingine ya katiba ni lazima iwe ni sheria kuu ya nchi. Sheria zingine za nchi zinakuwa extension ya katiba. Hivyo code of ethics unaziweka kwenye sheria ya nchi.

Kwa mfano sheria inaweza kupitishwa kuwa rais anapopiga kampeni ya kuchaguliwa tena asitumie vyombo vya dola kumsaidia. Ukiiweka kwenye vifungu vya sheria za nchi, hakutakuwa na haja ya kufanya amendment yoyote hile.

Vilevile katiba ni lazima iwe neutral document kwa kiasi kikubwa. Unaporuhusu kila kitu kiwe kwenye katiba, utaruhusu tyranny of majority kama inavyotokea Tanzania. CCM wana wabunge wengi na wana rais. Hivyo wanaweza kubadilisha vitu kukidhi mahitaji yao.
 
Hizo rekodi unazosema zipo za vifo vya watu waliokufa kutokana na Azimio la Arusha ziweke hapa JF. Here we dare talk openly. Kama huna basi ni uwongo.

Tunalumbana hapa si kwa sababu hatujui tunakotoka na tunakokwenda. Tunalumbana hapa kwa sababu the likes of you mmeamua makusudi kutupotosha tusimulike madhambi yanayofanywa na serikali za post Arusha declaration na sera mbovu za Mkapa/ Kikwete.

Tanzania leo ina matatizo makubwa kwa sababu uongozi wa sasa hauna dira, hauna ruuya (vision) na umekithiri kwa wizi mtupu. Kama hicho ni kitu cha kushabikia, nakusikitikia sana na ndoto zako za uongozi kwa sababu inavyoonekana hautakuwa tofauti na hawa unaowashabikia.

I am out!
 
Mkuu Kichuguu,

Ni kweli katiba inaweza kuwa na code of ethics, na kufanyiwa amendments. Lakini sifa ya katiba ni kuwa kitabu kifupi chenye kuwezesha watu wote kukielewa haki zao na muundo wa shughuliza za kiserikali.

Sifa nyingine ya katiba ni lazima iwe ni sheria kuu ya nchi. Sheria zingine za nchi zinakuwa extension ya katiba. Hivyo code of ethics unaziweka kwenye sheria ya nchi.

Kwa mfano sheria inaweza kupitishwa kuwa rais anapopiga kampeni ya kuchaguliwa tena asitumie vyombo vya dola kumsaidia. Ukiiweka kwenye vifungu vya sheria za nchi, hakutakuwa na haja ya kufanya amendment yoyote hile.

Vilevile katiba ni lazima iwe neutral document kwa kiasi kikubwa. Unaporuhusu kila kitu kiwe kwenye katiba, utaruhusu tyranny of majority kama inavyotokea Tanzania. CCM wana wabunge wengi na wana rais. Hivyo wanaweza kubadilisha vitu kukidhi mahitaji yao.
Katiba yetu inatakiwa ifuate MISINGI YA AZIMIO LA aRUSHA.
au hujui hilo?
 
Back
Top Bottom