Azimio No. 181 la Umoja wa Mataifa lilitengeneza matokeo ya leo kati Palestina na Israel.

Azimio No. 181 la Umoja wa Mataifa lilitengeneza matokeo ya leo kati Palestina na Israel.

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Baada ya kufatilia kwa utulivu issue ya migogoro isiyoisha kati ga Palestina na Israel, nimejilidhusha pasi na shakha kuwa Umoja wa Maitafa chini ya azimio lake la mwaka 1947 la kuigawa Palestina ya Uingereza na kutoa nchi mbili yaani ya Wayahudi na Waarabu ndiyo ilikuja kutengeneza tatizo zaidi katika eneo la mashariki ya kati.

Inakadiliwa ardhi yote ya Palestina ya Uingereza kabla ya haijamegwa ilikuwa na ukubwa wa Kilometer za mraba elfu 26,000, Azimio No. 181 la mwaka 1947 ambalo lilipendekeza ardhi ya kiparestina ya Uingereza ikatwe mapande mawili yaani kwaajili ya wakazi wa kiarabu na nyingine wakazi wa Kiyahudi ndilo lilikuja kuzaa mzozo zaidi, na mpaka sasa hakuna majibu ya uhakika kwanini jumuiya hii iliamua kufanya hivi.

Inakadiliwa Wayahudi mwaka 1947 waliokuwa wanaishi huko Palestina mara baada ya kuanza harakati za kisiasa 1917 za kizayuni kurudi wanakoamini ni kwao mara baada ya kuishi Ulaya takribani miaka 400 walikuwa laki 6 (600,000).

Eneo walilopewa Wayahudi kuunda nchi yao lilikuwa takribani KM za mraba elfu 14.

Mwaka huu 1947 jamii ya kiarabu ikiyoishi hapo Palestina kabla haijakatwa ilikuwa takribani watu Milion 1 na laki 7 (1,700,000+) yaani mara 3 ya population ya kiyahudi.

Eneo walilopewa Wapalestina (Waarabu) la kuanzisha nchi yao lilikuwa takribani KM za mraba elfu 10.

Eneo la Jerusalem Umoja wa Mataifa lilipendekeza lisiwe na mwenyewe bali litakuwa chini ya umoja wa maifa.

Mashakha yangu!

Walitumia vigezo gani kuipa Israel eneo kubwa zaidi ikiwa alikuwa na Raia wachache na kuwapa eneo dogo Wapalestina ambao walikuwa na raia wengi?

Mwenye majibu aje anifundishe tafadhali.
mapcard-palestina-1946-today.jpg
 
Back
Top Bottom