Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Hamza Aziz alikuja kuwa IGP wa kwanza wa Tanganyika huru.
 
Kumbe Dossa Aziz ni Mtoto wa Aziz Ally? Ilikuaje Mzee Dossa yeye akaelekeza makazi yake Mlandizi Pwani?
 
Hamza Aziz alikuja kuwa IGP wa kwanza wa Tanganyika huru.
Ahaaa You see! Jamani safi sana! I am sure alichaguliwa kutokana na Credit lakini pia huwa kuna lawama Mwalimu Nyerere sijui hakuwakumbuka baadhi ya watu, huenda pia mchango wa baba yake ulisaidia. Lakini botom line, Academic Qualifications tu hazitoshi vijana wajue kuwa Attitude inachangia mnooo pia katika kazi. Ninaamini na huyu Bwana Hamza alikuwa nayo na ilijengwa na baba yake. Kuna la kujifunza hapo! Thanks.
 
Oh kumbe Mwafrika wa kwanza maana yake ni Mtanganyika wa kwanza ?

Asante sana
Hapa hebu nimsaidie maana sijui utakuwa wa mwaka gani. Hapa alikuwa analinganisha makundi ya: Mwafrika, Mzungu, Muhindi na mwarabu.
 
Mwana,
hakuna mahali popote katika maandishi yangu ambako nimeleta
hoja ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kukumbukwa
kwa kupewa vyeo.

Mimi siku zote nimeandika msukumo ukiwa kusahihisha historia.

Labda nifahamishe kuwa wengi katika waliomuunga Nyerere mkono
mathalan Abdul Sykes, Dossa Aziz, Hamza Mwapachu, John Rupia
na wazee kama Mwinjuma Mwinyikambi, Jumbe Tambaza kuwataja
wachache walikuwa watu wa kujiweza sana.

Miaka ya 1950 Dossa Aziz ana malori saba ya mchanga na yeye mwenyewe
ana gari ndogo ya kutembelea na nyingine alimpa Nyerere afanyie kazi za
TANU.

Abdul Sykes anaendesha Mercedes Benz kijana mdogo kabisa.
Mdogo wake Abbas anaendesha Citroen ikisisimua vijana wenzake mji mzima.

Mie mdogo haya yote nimeyaona kwa macho yangu.

Siku moja nazungumza na Balozi Abbas Sykes nikamuuliza kuhusu ile gari
yake.

Nilipata mshtuko.

Alinambia hela ya kununua ile gari alichukua kwa mama yake Bi. Mruguru biti
Mussa.


Wazalendo hawa hawakufanya yote waliyofanya kwa kutaka vyeo baada ya uhuru
kupatikana.

Ninachofanya mimi siku zote ni kuiweka sawa historia za hawa wazee wangu ili
kizazi hiki na vinavyokuja waje kuwajua watu hawa na historia yetu isipotee.

Mtunda yake ni haya kuwa hii leo vijana wa Gerezani wananiandikia wananiuliza
kwa nini Yusuf Makamba apewe mtaa Gerezani ilhali Dossa Aziz aliyefanya
makubwa hajapewa mtaa wowote?

Jibu langu siku zote huwaambia kuwa waiulize serikali ya CCM ni vigezo vipi
vilitumika kumpa Makamba mtaa wakamuacha Dossa?

Mwana,
Kuna la kujifunza hapa.
Thanks.
 
MOhamed naona hukunielewa sikukusema wewe nimesema kuna watu huwa wanatoa Lawama kwa Mwalimu Nyerere wewe ndio umetutoa tonmgotonmgo kuwa pamoja na credit za watoto wa waliochangia uhuru inaonekana waliwaconsider. Sasa sijui wapi nimekupoint wewe labda ni kujishuku tu!
 
Mpaka kupitia Index kwa nini huyataji?!?!?!
 
Can You imagine?!?!?! Double standard!!!!
 
Cha Muhimu ni kuwa nchi hii ilipiganiwa na makabila yote na dini zote. lakini hikli haliondoi ukweli kuwa aliyewaunganisha mpaka tukapata uhuru ni Mwalimu Nyerere. Hebu naomba utuandikie kwa uchambuzi " Analysisi'' Factors zilizo mfanya - Mwalimu mwenye umri mdogo sana, Mtu aliyetokea Bara, Mtu mywenye dini tofauti na Wapigania uhuru ambao umewataja. Alikuwa ana karama gani kuweza kuwaconvince mpaka wakampa uongozi na kweli Uhurtu ukapatikana? Hebu tuandikie na hicho kitabu na utumie reference zako. Kwani kama kupigania uhuri wako wengi tu akiwemo mama mmoja alityesema mimi nilipigania uhuru na sikutaka cheo!
 

Povu linakutoka, huo unaousema ni uongo mpaka sasa hujaja na mbadala wake wa ukweli.

Tunajuwa, ni maradhi ya moyo na kila kukicha huzidi.


Alama Mohamed Said leta historia ya wazee wetu waliosahauliwa na nnaelewa kwanini Duduwasha historia hii inamuwasha mpaka povu linamtoka kwa kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Ni kwa sababu tu hawaoni wazee wake kwenye hii historia na akitazama kumbukumbu zao anakuta hana kabisa pa kuwaweka kwenye historia hii adimu ya Tanganyika.

Duduwasha tupe basi ukweli badala ya huu uongo tunaousoma hapa.

Hapo sasa!
 

Si uandike wewe unayoyajuwa, maana Mohamed Said kayaandika ayajuayo kutokana na wazee wake alipokuwa akikuwa anawaona.

Hivi yote ayasemayo, umekisoma kitabu cha Mohamed Said japo kimoja ukayakosa? Kama jibu ni ndiyo tuandikie basi mbadala na ukizitaka rejea zake zote kaziainisha katika vitabu vyake kitaalam kabisa.

Mbona waandishi wengine wengi tu huenda mpaka kwake kuchukuwa elimu bila khiyana, hata nawe waweza kwenda tu kuchota mengi halafu uje na mbadala.
 
Naomba anijibu muhusika tafadhali!
 
Nakushuru kwa kusahihisha makosa ya kiherufi...

Juu ya rejea sina sababu ya kuzisoma kwakuwa zote ni mkusanyiko wa mawazo yako jambo ambalo mimi nakupinga siku zote.

Umesahihishwa mpaka jina la mtaa si herufi tu.

Huna ulijualo kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…