Ahaaa You see! Jamani safi sana! I am sure alichaguliwa kutokana na Credit lakini pia huwa kuna lawama Mwalimu Nyerere sijui hakuwakumbuka baadhi ya watu, huenda pia mchango wa baba yake ulisaidia. Lakini botom line, Academic Qualifications tu hazitoshi vijana wajue kuwa Attitude inachangia mnooo pia katika kazi. Ninaamini na huyu Bwana Hamza alikuwa nayo na ilijengwa na baba yake. Kuna la kujifunza hapo! Thanks.
Mwana,
hakuna mahali popote katika maandishi yangu ambako nimeleta
hoja ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kukumbukwa
kwa kupewa vyeo.
Mimi siku zote nimeandika msukumo ukiwa kusahihisha historia.
Labda nifahamishe kuwa wengi katika waliomuunga
Nyerere mkono
mathalan
Abdul Sykes, Dossa Aziz, Hamza Mwapachu, John Rupia
na wazee kama
Mwinjuma Mwinyikambi, Jumbe Tambaza kuwataja
wachache walikuwa watu wa kujiweza sana.
Miaka ya 1950
Dossa Aziz ana malori saba ya mchanga na yeye mwenyewe
ana gari ndogo ya kutembelea na nyingine alimpa
Nyerere afanyie kazi za
TANU.
Abdul Sykes anaendesha Mercedes Benz kijana mdogo kabisa.
Mdogo wake
Abbas anaendesha Citroen ikisisimua vijana wenzake mji mzima.
Mie mdogo haya yote nimeyaona kwa macho yangu.
Siku moja nazungumza na
Balozi Abbas Sykes nikamuuliza kuhusu ile gari
yake.
Nilipata mshtuko.
Alinambia hela ya kununua ile gari alichukua kwa mama yake
Bi. Mruguru biti
Mussa.
Wazalendo hawa hawakufanya yote waliyofanya kwa kutaka vyeo baada ya uhuru
kupatikana.
Ninachofanya mimi siku zote ni kuiweka sawa historia za hawa wazee wangu ili
kizazi hiki na vinavyokuja waje kuwajua watu hawa na historia yetu isipotee.
Mtunda yake ni haya kuwa hii leo vijana wa Gerezani wananiandikia wananiuliza
kwa nini
Yusuf Makamba apewe mtaa Gerezani ilhali
Dossa Aziz aliyefanya
makubwa hajapewa mtaa wowote?
Jibu langu siku zote huwaambia kuwa waiulize serikali ya CCM ni vigezo vipi
vilitumika kumpa
Makamba mtaa wakamuacha
Dossa?
Mwana,
Kuna la kujifunza hapa.
Thanks.