Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Wanamajlis,
Katika mambo yanayonishangaza katika historia ya TANU kama nilivyoiandika ni jinsi inavyopandisha ghadhabu kwa baadhi ya watu.

Nimeeleza hapo juu chanzo cha khitilafu katika kuandika historia ya TANU.
Kiasi nahisi imewatisha baadhi yetu.
 
Duduwasha,
Sioni tena lile bandiko lako la matusi.
Ikiwa umelifuta basi umefanya jambo jema.

Ahsante sana.
 
Hii ni open forum kila member anachangia,hakuna anayedandia hapa,kifupi huna la maana lolote unalochangia hapa zaidi ya kupost maneno machafu ambayo ndio maisha yako, siku nyingine unapokua hujui jambo ni bora ukapita kimya tu kuliko ulivyojiaibisha kwenye hii mada kwa kujionyesha wazi kabisa kua Kichwani u mweupe na huna ujualo!
 
Mkuu wangu Mohamed, unavyoandika, you sound like Nyerere hakutaka mchango wa hawa aliowakuta wakiongoza TAA kabla yake utambulike. Ukiisikiliza hotuba ya Nyerere kwa wale aliowaita wazee wa Dar es salaam wakati anaaga baada ya kuchaguliwa Mwinyi, inafuta kabisa mengi unayoyaandika.

Kuna kitu hujakiweka wazi.
 
..Mi nadhani hapa amemzungumzia zaidi Aziz Ally...na sykes. Kupogania uhuru ni sehemu mambo waliyofanya...hakuna udini hapo
 
Hahaaaa ahsante ingawa hujajibu swali langu!

Majina yote yana asili ya Uingereza, nashangaa anaposema aliletwa na Wajerumani kupigana na Wareno - binafsi sijawahi kusikia kwamba wajerumani waliwahi kupigana na Wareno, ninacho fahamu ni kuhusu wanajeshi kutoka Africa kusini chini ya General Jan Smuts walisaidiana na wanajeshi wa Uingereza nafikiri na Wabelijiji kumung'oa Mjerumani kutoka kuloni lake la Tanganyika.
 
..Una kashfa sana mzee...punguza chuki ya dhahiri.Hata ww nadhani hujaelewa huyu mzee mo anazungumzia nini...mimi kwa uelewa wangu kazungumzia umaarufu,kazi,sehemu(daresalaam).na shida kwako ni dini hakuna kingine mkuu si ndiyo??kwa hiyo ulitaka aziz ally awe mkatoliki kama wewe na mimi ndio uwe positive na hii historia...Aziz hakuwa mwanasiasa alikuwa mfanyabiashara (contractor) na ndivyo alivyoandika mwandishi kwa hiyo yeye kusaidia sehemu ya uhuru kwa harakati za daresalaam haikuwa issue kubwa mpaka awekwe kwenye historia...ukisema hivyo kwamba wapigania uhuru wapo wameandikwa kwenye vitabu unatoka nje ya historia hii.unachofanya ni kumshambulia makusudi mzee mo.said na hupendi kusikia waislamu wamefanya kitu kizuri...ndivyo nilivyokuelewa samahani japo ndiyo ukweli...By the way mimi ni mkatoliki naitwa Franklin.....
 
lete na historia ya vituo hivi,kwa matias,kwa mfipa,kwa ali maua,kwa mtogole.
 
Aziz ali mtu,mdigo mtu wa Moa kwa wadigo ndo wa kwanza kumilik gari Africa
 
..Mi nadhani hapa amemzungumzia zaidi Aziz Ally...na sykes. Kupogania uhuru ni sehemu mambo waliyofanya...hakuna udini hapo

Well said mkuu, Moh anazungumza aliyo yaona na kusikia - mambo mengi/harakati zilianzia hapa Dar kila mtu analijua hilo sasa kama Watanganyika majasiri wakati huo majority walikuwa ni Waislaam, je, mnataka hilo lisisemwe - mbona baadae walikuja wakristo na wapagani mfano: Paul Rupia, Dk.Mtahangarwa, Dk.Kyaruzi nk.

Haya mambo ya kumkandia Moh. eti yuko biased binafsi nashindwa kuelewa hoja za namna hiyo - tatizo kubwa hapa watu wengi utamani Nyerere ndiye ahusishwe kwa kila kitu - wakati yeye alikaribishwa tu na kukriminiwa na Waislaam, waislaam hao hao ndiyo walipedekeza Nyerere aingoze Chama kutokana na Usomi wake, lakini hilo halina maana kwamba wapigania uhuru wengi wa wakati huo walikuwa wasomi sana au nini sijui, waislaam wengeweza kudai uhuru wa Tanganyika bila ya kumshirikisha Nyerere. Haya mambo ya kuchukulia mtu mmoja kama Alpha na Omega hayafahi hata kidogo, kuna,watu wengi tu wakichangia sana katika harakati za kudai uhuru lakini awatajwi kwenye vitabu vya historia ya Taifa letu na ukichunguza sana utakuta ni wale waliopishana kiswahili na Nyerere! Sikatai Nyerere alijitahidi sana pamoja na wenzake kutufikisha tulipo kitu kilicho kuwa kinanishangaza katika mojawapo ya hulka yake ni kuendekeza vinyongo - sikumbuki kama aliwahi kuhudhulia mazishi ya wanaharakati wenzake mfano: Prof. Abdallahaman Babu, Zuberi Mtemvu, Kasela Bantu, Oscar Kambona, Bibi Titi na wengine wengi tu - kitu hiki kilinishangaza sana.
 
Gagnija,
Kitu gani sitaki weka wazi?
Niulize na ikiwa ninalo jibu nitaliweka hapa jamvini.
 
..Mi nadhani hapa amemzungumzia zaidi Aziz Ally...na sykes. Kupogania uhuru ni sehemu mambo waliyofanya...hakuna udini hapo
Tonic Jr,
Mimi naandika yale niyajuayo.
Ikiwa wewe unaona ipo kasoro basi rekebisha.

Hapa ni mahali sote tunasomeshana.
 
Bukyanagandi,
Nilichosema ni Wazulu walipigana na Wareno Mozambique.

Rudia kusoma upya tafadhali.
 
..Watanzania siyo watu tunaopenda kutafuta ,kupokea ,kukubali na kurudisha kitu kama kilivyo..lazima kisemwe kipitishwe ktk dini,kiletwe kwenye kanda na makabila yake na ndipo upatikane ubaya wa kusemana lakini siyo kufumbua au kuelimishana...hii historia ya huyu mzee ni sahihi...uislam ilikuwa ni lazima uwe na nguvu maeneo(daresalaam) ambayo ameyazungumzia mzee Mo na ndiyo makazi ya kina Aziz..watu wanataka wasikie historia wanavyopenda wao ziwe kwa sababu wanaamini wao ni bora kuliko wengine au wao wanastahili yote hayo..wanasahau kwama siku zote ukitaka kwenda mbali lazima uambatane na mwenzako lakini ukitaka kwenda haraka nenda peke yako...Uhuru haikuwa safari fupi wala ya haraka Uamue uende peke yako.....ni safari ya muungano wa watu na mawazo yao na uwezo wao maana safari haikuwa fupi
 
Tonic Jr,
Mimi naandika yale niyajuayo.
Ikiwa wewe unaona ipo kasoro basi rekebisha.

Hapa ni mahali sote tunasomeshana.
..Mzee hiyo quote yangu napingana na wanaosema umeongelea udini.isome vizuri
 
Hawaweki historia hii kwenye vitabu, sababu ya kuhofia udini mtajua asili ya nchi yenu, imetokana na dini gani ndo maana wakawaachia nyerere, nyerere ni MTU mdogo sana kwenye Uhuru wa Tanzania, yaani tukiwafufua wazee Leo watalia kuona nyerere mnamuita baba wa taifa, ni hayo tu
 
Gagnija,
Ile hotuba ya Mwalimu Nyerere anaaga na kuwataja wazee wa Dar es Salaam
kila ninapoisikia hunijaza simanzi nyingi sana.

Nasikitika kwa kuwa wale wazee wote wana majina yao na kila mmoja wao
alikuwa na mchango wake katika kupigania uhuru.

Iweje hakuweza kuwataja kwa majina yao angalau wawili watatu hivi?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…