Oh kumbe Mwafrika wa kwanza maana yake ni Mtanganyika wa kwanza ?
Asante sana
Yamakagashi,
Usinishukuru subiri kwanza nikueleza habari za
Aziz Ali upate kumuelewa:
''
Dossa Aziz alipokwenda Nairobi mwaka wa 1946 alimkuta
Ally Sykes, kijana
maarufu na mwenye shughuli zake pale mjini akijulikana na takriban kila mtu.
Dossa Aziz alikuwa amekwenda Nairobi kufanya usaili wa mafunzo ya urubani.
Kulikuwa na vijana wawili kutoka Tanganyika, wote watoto wa matajiri.
Dossa Aziz alikuwa katika usaili na mtoto wa Mwarabu mmoja tajiri,
Ally Mmanga.
Dossa Aziz alikataliwa kufanyiwa usaili kwa kuwa alikuwa Mwafrika.
Waingereza walidai kuwa Waafrika hawakuwa tayari kufundishwa urubani.
Dossa Aziz alifadhaika sana.
Alimpigia simu baba yake huku akilia na kumpasha habari hizo.
Ili kumliwaza mwanae, baba yake
Dossa,
Aziz Ally, alimtumia fedha anunue gari
kama kifuta machozi.
Gari hili lilikuja kuwa ndiyo chombo cha kwanza cha usafiri kwa TAA, TANU na
Julius Nyerere.''