Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Kama wewe unaogopa kusikia historia ya wazee wa Dar basi Hii ndio historia tunayo itaka.Huwezi kutuzuia
Akili zako kama za wanasiasa wapumbavu hunyima haki na walionyimwa haki wakifhadhibika husema oh watu wanataka kuvunja Amani huku wakijua Uhuru ulitafutwa kwa ajili ya Uhuru na watawala wabovu hawatakiwi... Sasa na wewe ndio kundi hilo... Mimi sijakuzuia kusikia Wala siwezi ila nachopinga ni uongo ndani ya historia ambayo unaongozwa na udini... Na kana kwamba hiyo list ndio ilihangaika pekee na Uhuru .. Na pia atambue kuwa makini kwenye maandiko yake.. Huwa simuelewi kama anatafuta changamoto au hupenda tu kunogesha wasomaji vitu ambavyo huvichomeka...
 
Watanzania tuna safari ndefu sana, kuanzia uelewa wa kila kitu, watu tumeshindwa kusoma na kuelewa, badala yake tumesoma kwa mizuka na kukurupuka ndipo tuliposhindwa Kuelewa
Wewe ndio huelewi na pia huyu mleta Mada naye nadhani ni Mtanzania. Hivyo hoja yako ishapoteza nguvu means naye sehemu alizosoma hakuelewa pia. Hivyo unapingana na kila mmoja humu... Tafute upande mmoja tuwekane sawa.. Mizuka haihusuani na chochote humu... Labda ongea kinachoeleweka maana hoja yako imekaa kimatusi tu kama Sugu dhidi ya Mawaziri Wa Serikali... Ni uchochezi tu unavyofanya... Kama mleta Mada anatambulika ni mdini
 
Punguza Ghadhabu hakuna Ugomvi, Historia ukiamini imekosewa unaleta iliyopatiwa sio Matusi na kashfa na kejeli.

Ni mfano wa Utafiti Kama hukubaliani nao humtukani Mtafiti unaleta wa kwako uliobora zaid na Hilo litakuwa tusi Mujarrab!
Pohamba,
Ahsante sana ndugu yangu kwa maneno na nasaha za busara.

Mimi nilipoona kuwa Chuo Cha Kivukoni kwa maagizo ya CCM
imeandika na historia ya TANU na harakati za kudai uhuru
Tanganyika imeanza na Mwalimu Nyerere na kunalizikia kwa
Mwalimu Nyerere sikuikejeli wala kuwatukana Kivukoni.

Niliamnua kuandika historia ya TANU kama nilivyoifahamu kwa
kutumia staili ya ''biographical approach'' yaani kuandika maisha
ya watu walioasisi harakati za kuutafuta umoja wa Waafrika wa
Tanganyika.

Nyaraka za ukoo wa Sykes zilikuwa msaada mkubwa sana kwangu.


Nyaraka kutoka kwa Kavazi la Mwalimu Nyerere ikionesha nyaraka
kutokanyara za
Ally Sykes. Angalia uongozi wa TAA 1953 pamoja na
MwalimuNyerere yuko
Abdulwahid Sykes, Dome Budohi,John Rupia,
Dossa Aziz na Ally Sykes

Ndiyo leo tupo hapa kitabu kimependwa sana na sasa toleo la
Kiswahil tunakwenda tolea na nne na Kiingereza toleo la tatu.

Ningeamua kutukana nisingefika popote watu wangenidharau na
kunipuuza.

Ingia hapa kuangalia picha:Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE
 
Kahinda,
Hiyo balance usemayo nitaitoa wapi ikiwa hakuna cha kubalance?
hebu hiyo kazi ya ''balancing,'' ifanye wewe ikiwa unaweza.

Inaelekea hujasoma kitabu cha Abdul Sykes ungekutana na Mzee
Rupia
sehemu nyingi sana.

Atakae ithibati ya maneno yangu kuhusu John Rupia aangalie faharasa
ya kitabu changu ashuhudie katajwa mara ngapi.

Nashauri mngechukua muda lau mdogo wa kufanya utafiti kabla ya kuja
barzani kuchangia.

Wala hapa udini katika historia hii niliyoandika yote hayo yametokea.

Labda nikuulize hao walioandika historia ya uhuru na kuwafuta hawa
niliowaandika mimi wao walisukumwa na udini katika kuwafuta?
 
Watu kama wew wanahitajika sana nchi hii,yaan had kichefuchefu
Mara fulan bin fulan alikucha akiwa na miak 5 tayar akiw MUISLAM
What kind of hell is this!!!..
Dukeson,
Ongesoma swali lililoulizwa ungeelwa jibu lililotolewa.
Ghadabu inaondoka fikra makini.

Nimewaeleza Wazulu waliokuja Tanganyika mwishoni 1800.

Hawa walitokea Mozambique na fikra za wengi ni kuwa hawa
hawakuwa Waislam.

Ndipo nikaweka historia zao na kueleza kuwa walikuja Tanganyika
tayari Waislam.

Hili ndilo lililokukera kusikia kuna Mzulu anaitwa Ally Katini au
Hassan Machakaomo au Schneider Abdillah Plantan au
Mashado Ramadhani Plantan au Kleist Abdallah Sykes na
hawa wote walishiriki katika siasa za African Association na TANU
toka 1929.

Chuo Cha Kivukoni walikuwa hawayajui haya wao wameiona TANU
1954.
 
Mzee Mohamed Said nakushauri usiendeleze mabishano na hao wajukuu zako wasioelewa historia
Mapovu,
Ahsante kwa ushauri.
Hawa kwa umri wangu ni wanangu si wajukuu.

Mimi siko katika ubishi na yeyote niko hapa jamvini
nadarsisha.
 
Maana naona umaarufu wake huyu aziz ally ni kujenga misikiti tu.
 
Lakini huoni kama imesahulika kiasi fulani historia ya shuleni haiwataji kabisa me nadhani wangepewa heshima kama familia ya nyerere ingekuwa vizuri zaidi, na hii yote ni kutokana hawana mhamasishaji katika sector hyo
Kleist Sykes Jr ameshawahi kuwa diwan na Meya wa Dsm
 
Hapa nitakuwa nimekuelewa MOHAMMED SAID,ahsant kwa kunielewesha!!..
 
Mr Mohamed, tunaskia pia John Rupia alikuwa contractor na alisaidia kupigania uhuru. Je unamzungumziaje huyu mzee Rupia?
Itongo,
Mzee Rupia hakuwa mjenzi wa majumba bali yeye alikuwa na ''quary''
ya kokoto na pia akiuza mchanga vyote hivi ni vitu katika ujenzi wa
majumba na barabara na akitumia malori yake mwenyewe kwa kazi
hiyo.

Kuhusu mchango wake katika TANU ni mkubwa sana.

Nyerere alipojiuzulu ualimu alikuja Dar es Salaam na kukaa nyumbani
kwa Abdul Sykes.

Hii ilikuwa 1955 Abbas Sykes wakati ule kijana mdogo hivyo akahamishwa
chuma chake kumpisha Nyerere.

Nyerere baada ya muda alitafutiwa nyumba na Mzee Rupia Magomeni
Majumba Sita akahama kwa Abdul Stanley na Sikukuu Street akahamia
nyumba hii alotafutiwa na Mzee Rupia.


Hapa ndipo ilipokuwa nyumba aliyokuwa akiishi Nyerere alotafutiwa na Mzee Rupia.

Kuanzia TAA hadi TANU kulikuwa na wafadhili wakubwa wanne: John
Rupia
, Abdul na Ally Sykes na Dossa Aziz.

Ukitaka kujua mengi ya Mzee Rupia soma kitabu cha Abdul Sykes.
 
Na dosa aziz wana undugu na uyu aziz ally?
 
Mohamed Said unasema historia imewafuta kivipi?? Mbona mimi nimesoma historia na hawa watu wote unaowataja hapa wamo pia?? Mie ninachokipinga kwako ni umebase sana kwenye udini as if hao wengine wapagani na wakristo walikua magoi goi katika kutafuta huo uhuru. Kumbuka kua humo pia kuna wahindi na waarabu walikuwamo sijakuona ukiwataja kabisa dont say huwafahamu.
Angalizo: mimi ni muislamu ila udini noo kwangu.sisi ni watanzania na afrika ni moja.
 
Oh kumbe Mwafrika wa kwanza maana yake ni Mtanganyika wa kwanza ?

Asante sana
We nawe msumbufu!
Neno muafrica ktk hii context ni sahihi Zaidi kuliko mtanganyika!
Wakati wa miaka hiyo ya kugombea uhuru walipita watu wa mataifa mengi ktk Tanganyika ikiwemo wazulu, wanyasa, waganda, wazanzibar etc na wote hao waliishi kama wakazi rasmi ktk mji!
kwa hiyo to qualify kwa weusi wake basi neno Africa liko sahihi Zaidi kuliko Tanganyika!
 
Hizo njia ndio umefundishwa shuleni kwenu? Acheni ujinga na upumbavu hakika ulifail mitihani kama unaamini ulichofundishwa shuleni kwenu aina tatu za kujibu maswali... Mtu muongo akinaswa huishia kutukana naona umekazia kumtetea mpotoshaji
Mbona reactions zako ni beyond kusahihisha ukweli!
Umetumia lugha za matusi/kukera mno!
Kama mleta mada amekosea kitu, historia hujengwa kwa kusahihisha, kwa kuwa kila mmoja wetu hapa atakuwa anaandika masimulizi, then yale yanayokubaliwa na wengi ndio huwa assumed kama maelezo sahihi Zaidi!
wewe, huji na version yako, umekuja na matusi tu!
Kama Mohamed Said asipoleta uzi wa historia hapa JF hakuna mwingine anayeleta, sasa masimulizi ya Tanganyika yatajulikana vipi!
Sidhani kama kuna anayeweza kuukataa mchango Julius, Rupia au Okello! lakini pia ni ukweli wenyewe lazima wachangie ktk ukombozi, hebu fikiria tu Julius kutoka Butiama aliishi mtaa gani hapa Dar Es Salaam, unadhani angewezaje kupambana na wazungu ktk mitaa ambayo hata chochoro hajui, Rupia alikadhalika!
Naona wote mnaongea kitu kimoja ktk spectrum 2 tofauti, ambapo hamna haja ya kutukana bali kuongezea nyama ktk historia zinazoletwa!
 
Mauza,
Zungumza jambo unalolijua na kama wewe wewe ni Muislam
kama unavyosema utakuwa unajua kuwa Allah kaonya mtu
kulisema jambo ambalo hana ujuzi nalo.

Nakuona umelishikilia sana hili la udini wakati mimi nimeandika
kitabu cha historia hii na kimefanyiwa mapitio na mabingwa wa
historia ya Afrika kama John Iliffe, Jonathon Glassman na
James Brennan na hakuna hata mmoja kauona huo udini unaodai
wewe.

Catalogue ya Library of Congress inakieleza kitabu kama, ''Political
History.''

Mimi nimefanya utafiti na si wa kitabu hiki tu nimeandika ''paper,''
na huo udini unaoutaja wewe nimekutananao kwingi lakini si kwa
Waislam.

Fanya rejea kwa P Van Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi
(2002).

Fanya rejea hizo kisha rejea hapa jamvini utuambia kipi umekiona.

Ikiwa unawajua Wapagani, Waarabu na Wahindi katika historia ya
TANU tupe habari zao ili tujifunze lakini mimi nimewataja wote
waliokuwapo ulingoni wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika.

Ila nitakufahamisha kuwa wasio Waafrika walifunguliwa milango
kujiunga na TANU 1958 katika sakata la Kura Tatu.

Ila ndugu yangu nakuonya kwani wengi wamesababisha kuangamizwa
kwa wenzao kwa kusema wasiyoyajua.

Iko siku nitakupa kisa cha Rajab Diwani na Selemani Kitundu hadi
leo wametangulia mbele ya haki lakini madhila waliyoacha nyuma bado
yanakumbukwa.

Ndipo nilipokupa indhar mwanzo kabisa kuwa usiseme jambo usilolijua
kwa kutafuta sifa ukidhani utaonekana, ''Muislam mwema.''

Historia ya uhuru wa Tanganyika ina wengi mfano wa wewe na wote
wamemaliza maisha yao kwa majuto.

Nahitimisha kwa pale ulipozungumza, ''Afrika ni Moja.''

Nakufahamisha kuwa Ali Juma Ponda na Hassan Suleiman wakiwa
viongozi wa African Association 1945 walipata kuandika waraka muhimu
kwa Watanganyika wenzao wakiwaeleza kuhusu umoja wa Afrika.


Kushoto wa kwanza ni Ali Juma Ponda

Watafiti wa Chuo Cha Kivukoni hawakuwataja hawa popote katika kitabu
chao cha Historia ya TANU.

Labda hawakuwa wanawajua.
 
Kwa hiyo Kleist Sykes ni jina la asili ya Kizulu?
Na vipi kuhusu Dully?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…