B Dozen, Oscar, Kitenge na Hando wameondoka EFM. Kitenge na Hando watua Wasafi

B Dozen, Oscar, Kitenge na Hando wameondoka EFM. Kitenge na Hando watua Wasafi

  • Kwa hiyo, unataka kusema Vice chancellor na DVC wa Udsm, Mzumbe,udom,muhas,hwapati hizo?
  • maprofesa wakuu wa Vyuo kama IFM,NIT,CBE,TIA unataka kusema hawafiki 6m?
Hao sio "maprofesa wengi" katika vyuo kama ulivyoainisha kabla.

Hela yoyote ya ziada watakayolipwa hao uliowataja kutokana na vyeo vyao ni kutokana na hiyo administrative appointment na sio uprofesa wao na hizo nafasi hazizidi 3 kwa chuo (VC, DVC Academic, na DVC Administrative)
maprofesa wengi vyuoni ni academic members tu wa department na mshahara wao haufiki huko !
 
Kwani huyu Kitenge anategemea hizi radio station au ana mambo yake mengine anayoyajuwa yeye mwenyewe?

Maana safari za ng'ambo ulaya na Marekani Kitenge anaweza kushindana na Kikwete.

Sidhani hizo redio kama ndio ajira rasmi za Kitenge Mimi nadhani ni cover tu.

Huyo Gerald Hando alimatch sana na Masoud Kipanya, Clouds media is where he deserve, huyo mwingine Oscar Oscar Mimi nimemjulia WhatsApp naona memes zake zinasambaa, sijawahi hata kusikia huwa anatangaza kitu gani.
Mimi pia namuonaga tu kwenye memes[emoji81][emoji81]
 
Hao sio "maprofesa wengi" katika vyuo kama ulivyoainisha kabla.

Hela yoyote ya ziada watakayolipwa hao uliowataja kutokana na vyeo vyao ni kutokana na hiyo administrative appointment na sio uprofesa wao na hizo nafasi hazizidi 3 kwa chuo (VC, DVC Academic, na DVC Administrative)
maprofesa wengi vyuoni ni academic members tu wa department na mshahara wao haufiki huko !
Kwa hiyo unataka kusema professor analipwa 3m?
 
Wazee wamepiga 24 Hours notice !
Inakubalika kisheria, unamlipa muajili cash, au kama tarehe imefika hupokei mshahara unatowa notice simple kabisa.

Lakini ukitumia style hii hakikisha hutorudi tena hapo yakikushinda huko uendapo.

Ustaarabu mzuri ni wa kutowa notice ya mwezi mmoja.

Mmewashuhudia hapa TZ high Profile figure Senzo na Barbara walitowa notice kabisa Simba na Yanga na walijurikana kabisa wanaondoka lini haikuwa surprise kuondoka kwao.
 
Walichokosea ni kuleta siasa mwenye media, kumsimamisha Gerald Hando ulikuwa ni upumbavu mtupu.

Ninachojuwa kuhusu Kitenge sidhani kama anaishi kwa kutegemea hizo media, ndio maana anahama anavyojisikia lakini siyo swala la maslahi, huyo jamaa ana mambo yake mengine kabisa.
Kijiwe chetu cha Kahawa kinasema MAULID ni Shushushu🤣
 
Wakati tunajadili mishahara ya hawa watu tusisahau yafuatayo especially kwa hizi Urban Radios.

1. Approach vs Approached: Miaka ya nyuma nilikuwa nafanyia taasisi moja ya kifedha.

Sasa sijui ilikuwa ni uhaba wa Competitive Bankers au vipi lakini miaka ile haikuwa ajabu Staff wa Bank X kuwa approached na Bank Y kwamba ukafanye kazi kwao!

Ukishakuwa approached namna hii, unaahidiwa mambo mazuri including MSHAHARA NA BENEFITS.

So, kwenye media hapa Bongo, kuna layer fulani ya Watangazaji ambao mara nyingi wanakuwa approached na media zingine! Watu kama akina Kitenge, Edo Kumwembe, and the like huwa wanakuwa approached kujiunga na media fulani.

Hao wanalipwa vizuri sana!

2. Hao Watangazaji wanakuwa approached kwa sababu wana uwezo wa Kuvutia Advertisers kutokana na influence yao.

Kutokana na hilo, hao watu ni Mtaji Mzuri sana kwa redio. Aidha, kutokana na influence yao pia wanakuwa na fursa ya kuwa na connection na watu mbalimbali.

Connection hizi sio tu zinawasaidia kuleta deal mpya za matangazo kwenye redio bali pia ku-lobby pale ambapo hazipo.

Namba 2 hapo juu inawafanya wawe ni Ng'ombe Mzalisha Maziwa, na hivyo kuendelea kuwa na soko kubwa kwenye soko la ajira za Urban Radio.

3. Hizi media huwa zinatoa kamisheni kwa wale wanaofanikisha kuleta matangazo!

Sasa kwa sifa niliyotaja #2 hapo juu, unakuta mara nyingi wanakuwa miongoni mwa Staff wanaotandika kamisheni za kutosha!

NOTE: Usidhani watangazaji wote wapo sawa! Kama huna sifa nilizotaja hapo juu, na kwahiyo unategemea sana mshahara, basi Utangazji ni Kazi Iliyojaa Njaa!!

Aidha, sio kila mtangazi unayemsikia kwenye redio au kumuona kwenye tv ni Mwajiriwa!

Wapo wengi tu ambao wanapiga deiwaka kwa matarajio sooner or later ama watapata replacement hapo hapo au wataonekana na media zingine na hatimae akalamba ajira!

So, usimuone X aliye Wasafi au EFM analia njaa ndo ukadhani hapo Wasafi au EFM kuna njaa kali kihivyo... unaweza kukuta anapiga Deiwaka tu au ndo wale wasioleta cha ziada kwenye redio!
 
Habari za uhakika nilizonazo ni kwamba B Dozen ameondoka EFM na kutaka kurudi Clouds. Hata hivyo hawajareach agreement na Clouds, at the same time Wasafi wanamnyatia.

Oscar Oscar ameondoka EFM, Amejiunga na Wasafi kwa signing fee ya shilingi milioni 100. Mshahara wake kwa mwezi ni shilingi milioni 6.5.

Gerald Hando naye amejiunga na Wasafi akitokea EFM.

Maulid Kitenge yuko kwenye hati hati. Diamond anataka kumpa milioni 200 na Range Rover. Wako hatua nzuri hasa ukizingatia kwamba Hando na Oscar ambao ni marafiki zake wakubwa wameshaaenda EFM.

Ni test ngumu kwa Majizzo, akivuka salama hapa EFM haitashuka hata siku 1.
Hizi signing fees ni ulongo 🤣🤣🤣
 
Kitu pekee hamjatizama ambacho nimekiona ni kiini macho kwa watizamaji na wasikilizaji wa hivyo vituo ,mabos wanakaa mezani wanawaza wafanye nini ili wasikilizaji na watizamaji waongezeke , wazungumziwe zadi wawe top kwenye biashara yao , njia wanayoiona ndio hii ,, na wamefanikiwa mana fb ,jf ,insta na mitandao mingine mingi wanawazungumzia wasafi na efm tangu jana usiku , wafuasi wao watataka kujua zaidi wanaenda kuendesha vipindi gani huko , mabos wanapiga hela ndefu wanagonga cheers maisha yanasonga fresh ,kisha tunawaita freemason kwa akili yao kubwa
 
Back
Top Bottom