B Dozen, Oscar, Kitenge na Hando wameondoka EFM. Kitenge na Hando watua Wasafi

B Dozen, Oscar, Kitenge na Hando wameondoka EFM. Kitenge na Hando watua Wasafi

Kitenge ana "Lishangazi" lake US.... inawezekana na yenyewe ni cover up tu
Kwani huyu Kitenge anategemea hizi radio station au ana mambo yake mengine anayoyajuwa yeye mwenyewe?

Maana safari za ng'ambo ulaya na Marekani Kitenge anaweza kushindana na Kikwete.

Sidhani hizo redio kama ndio ajira rasmi za Kitenge Mimi nadhani ni cover tu.

Huyo Gerald Hando alimatch sana na Masoud Kipanya, Clouds media is where he deserve, huyo mwingine Oscar Oscar Mimi nimemjulia WhatsApp naona memes zake zinasambaa, sijawahi hata kusikia huwa anatangaza kitu gani.
 
Habari za uhakika nilizonazo ni kwamba B Dozen ameondoka EFM na kutaka kurudi Clouds. Hata hivyo hawajareach agreement na Clouds, at the same time Wasafi wanamnyatia.

Oscar Oscar ameondoka EFM, Amejiunga na Wasafi kwa signing fee ya shilingi milioni 100. Mshahara wake kwa mwezi ni shilingi milioni 6.5.

Gerald Hando naye amejiunga na Wasafi akitokea EFM.

Maulid Kitenge yuko kwenye hati hati. Diamond anataka kumpa milioni 200 na Range Rover. Wako hatua nzuri hasa ukizingatia kwamba Hando na Oscar ambao ni marafiki zake wakubwa wameshaaenda EFM.

Ni test ngumu kwa Majizzo, akivuka salama hapa EFM haitashuka hata siku 1.
 
Kwani huyu Kitenge anategemea hizi radio station au ana mambo yake mengine anayoyajuwa yeye mwenyewe?

Maana safari za ng'ambo ulaya na Marekani Kitenge anaweza kushindana na Kikwete.

Sidhani hizo redio kama ndio ajira rasmi za Kitenge Mimi nadhani ni cover tu.

Huyo Gerald Hando alimatch sana na Masoud Kipanya, Clouds media is where he deserve, huyo mwingine Oscar Oscar Mimi nimemjulia WhatsApp naona memes zake zinasambaa, sijawahi hata kusikia huwa anatangaza kitu gani.
Hando, Kipanya na Fina Mango ilikua 🔥🔥🔥. Hando alikuwa anakuambia mtu tatu kama bilioni 3.
 
😂🤣 aisee hii mbona kali, nilishawahi ishi nyumba moja na mtangazaji wa TBC, ni yale yale tu.
Nimeshawahi kuwa karibu na watu wa media. Kiukweli maisha yao ni magumu sana. Mwaka 2012 kuna redio moja sitaitaja ilikuwa inalipa 150k kwa watangazaji wao wengi. Ila nao watu wa media ni kama misukule... yaani kukaa nyuma ya MIC kwao inawapa raha za ajabu hata usipowapa mishahara kwao poa tu.

Ule umaarufu uchwara unawazuzua. Kwenye media angalau wanawake ndo wako poa kwasababu wana mambo yao mengine. Waandishi, watangazaji na wasanii ni watu wenye maisha magumu.
 
Nimeshawahi kuwa karibu na watu wa media. Kiukweli maisha yao ni magumu sana. Mwaka 2012 kuna redio moja sitaitaja ilikuwa inalipa 150k kwa watangazaji wao wengi. Ila nao watu wa media ni kama misukule... yaani kukaa nyuma ya MIC kwao inawapa raha za ajabu hata usipowapa mishahara kwao poa tu. Ule umaarufu uchwara unawazuzua. Kwenye media angalau wanawake ndo wako poa kwasababu wana mambo yao mengine. Waandishi, watangazaji na wasanii ni watu wenye maisha magumu.
Kwa wenye majina makubwa na umaarufu wana ahueni kidogo ila wengi ni kawaida sana.
 
Kama profesa hafikishi hiyo hela basi hali ni mbaya.
Wewe unadhani Maprofesa wangelipwa vizuri wangeng'ang'ania siasa ya kazi gani? K.ushindana na darasa la saba kina Bajaj?

Hivi hujiulizi ni kwa nini Lipumba project za wazungu alikuwa anakwenda kufanya na anaicha CUF na anakaa muda mrefu Ulaya, lakini sasa hivi yupo radhi alale Buguruni kuliko kumuondowa CUF?
 
Back
Top Bottom