B Dozen, Oscar, Kitenge na Hando wameondoka EFM. Kitenge na Hando watua Wasafi

B Dozen, Oscar, Kitenge na Hando wameondoka EFM. Kitenge na Hando watua Wasafi

Hii sasa vita ya Efm na Wasafi fm imepitiliza.

Maulidi Kitenge amerudi tena Wasafi fm na Gerald Hando kahamia kwa mara ya kwanza ikiwa nadhani baada ya kufungiwa na Majizo kwa miezi mitatu.

Wanasikika kipindi cha Goodmorning kuanzia leo
Kwani huyu Kitenge anategemea hizi radio station au ana mambo yake mengine anayoyajuwa yeye mwenyewe?

Maana safari za ng'ambo ulaya na Marekani Kitenge anaweza kushindana na Kikwete.

Sidhani hizo redio kama ndio ajira rasmi za Kitenge Mimi nadhani ni cover tu.

Huyo Gerald Hando alimatch sana na Masoud Kipanya, Clouds media is where he deserve, huyo mwingine Oscar Oscar Mimi nimemjulia WhatsApp naona memes zake zinasambaa, sijawahi hata kusikia huwa anatangaza kitu gani.
 
Hiki kipindi Cha asubuhi Cha wasafi ni kijiwe Cha watangazaji.Kuna Zembwela ,Zungu, Charles,Maulid kitenge, Ernest kawawa,Gerald hando na Salma Dakota.

Hapo kulogana lazima ndipo unasikia kwenye ridhiki hapakosi chuki na majungu
Jibu liko wazi, hapo maana yake Hakuna meneja wa vipindi na uzalishaji, na kama yupo unaanza na huyo akatafute kazi sehemu nyingine hawezi kazi.
 
Back
Top Bottom