Baada utawala wa Syria kuanguka Israel wamekimbilia kuchukua maeneo katika miji mitano katika milima ya Golan ya Syria wanazidi kuongeza mgogoro


Ritz, hivi bado wewe ni mgeni wa historia ya mashariki ya kati? Kila vita Mwarabu anapoaanzisha huwa ndio anapoteza ardhi...Ilikuwa hivyo 1948, 1967, 1973....na Inarudia tena sasa hivi......! Nilimwambia jamaa fulani humu jamvini, Hamas hawatapata hata futi moja vumbi itakapotulia! Hamas wamesababisha Syria ianguke, sasa inanyang'anywa ardhi....Iran inafunga virago vyake middle east....basi tabu tupu.
 
Tarehe 7/10/2023 alibezwa, alisimangwa, alisutwa, alikejeliwa sana, sasa ame prove wrong. Anapigana direct and indirect kote, Syria, Lebanon, Iran, Ghaza, Yemen. Sisi tusuburi watwangane tuone mbabe.
 
Ritz Badilisha nick name yako ujiite Aljazeera mchochezi
 
Unajua hao jamaa wana support ya na naji nyuma yao ? Fund and mafunzo? Mipango?

Hawapo wenyewe, ni collective decision
 
Askari wa Assad waliambiwa wasipigane na waziri wa jeshi lao pamoja na Chief of Staff wao. Je ni Assad ndio aliwambia au wao ndio walimgeuka.
Hapo Russia na Iran hawakuwa na namna yoyote ya kusaidia. Utasaidia vp nchi ambayo jeshi mwenyeji halitaki kupigana au limsaliti
 
Acha uongo basi..
  • Miji mitatu kati ya hii iko ndani ya eneo la buffer lililosimamiwa na UN la
    1974, eneo ambalo
    Israeli ilitekwa kinyume cha sheria katika vita vya 1973 na
    kulazimishwa kurejea
    Syria:
Wew bado una comment tu humu? Si ulitudanganya Urusi na Iran hawawezi kuiachia Syria ichukuliwe na waaasi. Bado unataka tukuamini tu na mihemuko yako ya kidini?
 
Mkuu ; Usihangaike. Vita vya panzi ni furaha ya kunguru. Naona mjomba Neta kajiokotea pande la ardhi. Halafu ujue halitokaa lirudishwe kwa mwenye nalo. Si unamjua Myahudi?

Na ukizingatia alishawah kulimiliki wakamlazimisha alirudishe sasa hivi hawatalirudisha kwa kisingizio cha usalama
 
Kwanza hapa Mohammad kuonyesha sio mtume wa Mungu alitunga uongo maana hamna sehemu wayahudi wanasema Ezra ni mwana wa Mungu.
 
Kuna watu vita ndio biashara yao
Watahakikisha wanaendelea kupigana
 
Haya ni mambo yaliyopo katika unabii. Ni lazima yatokee. Iran, Urusi na wengine ni Lazima waanguke ili wale wafalme wanaoanzisha mambo ya ajabu waweze kupita na kufanikisha mambo yao duniani kote. Kila mtu awe na uhuru wa kuchagua anasimama upande gani.

12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
Ufunuo wa Yohana 16:12

13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Ufunuo wa Yohana 16:13

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Ufunuo wa Yohana 16:14

15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Ufunuo wa Yohana 16:15

16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.
Ufunuo wa Yohana 16:16
 
Misri Saudi Arabia mpaka Iran uko potential pa Isreal so mjomba anaanza kujitanua sasa
 
Hapo Russia na Iran hawakuwa na namna yoyote ya kusaidia. Utasaidia vp nchi ambayo jeshi mwenyeji halitaki kupigana au limsaliti
Assad this time alitakiwa aseme na yeye anaingia front line ili kuwapa morali wajeshi wake.. ila akasema naongeza mshahara 50% , wakamuona mngese kweli yaani uhai wao uharibifu wa maisha na mali for himself dadeki wakawa wanapisha tu jamaa wanabeba silaha na kusonga without a single shot.. Iran akajifanya kuleta ndege yenye shehena ya silaha militants wakampigua simu Netanyahu na Neta bila hiyana akamuambia Iran ukitua unakutana na mlipuko ardhini.. Ayatollah akageuza ikawa too late akajibu 4th time habari ni ile ile.. Game ikawa over
 
Kwani vikosi vya Iran viko wapi? Si visaidie kuzuia haya mashambulizi,au si Hezbollah wapo na wana nguvu si waende Syria kupigana na Israel ambao wanazidi kujitwalia maeneo huko Syria. Na tulikubaliana wote humu kuwa Israel kaomba cease fire Lebanon baada ya kuzidiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…