Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Hivi Kwanini hawakuanza Kwa Kulibinafsisha Bunge halafu baadae Serikali Kuu na Mahakama
Wa Bongo hakuna Kitu tunaweza Fanya, Mkoloni arudi tu
 
Vipi wamekukatia bomba lako la mafuta Nini🀣🀣 maana hatuangalii hasara tuliyokuwa tunaipata Mara mifumo ya Kodi haisomani Mara bomba limeelekezwa kwa mubongo mmojaπŸ˜†
 
Umeona viongozi wa chadema wamekemea huu ubinafishaji wa kijinga?
 
Nchi hii ni ya kipuuzi sijawahikuona tangu nizaliwe hapa Ulimwenguni. Hivi hawa wakoloni weusi (CCM) huwa wanawaza nini lakini?
-----------------------------------------------------------
Bunge DHAIFU la CCM limepitisha azimio la kubinafsisha bandari ya DSM kwa kampuni ya DP World ya Dubai kwa miaka 100 hadi 2123.

#MyTake:
1. Maamuzi haya yamelenga kunufaisha watu wachache na kufuta urithi kwa vizazi vijavyo. Mwaka 2123 hakuna yeyote kati yetu atakayekua hai. Maana yake tumeamua kuwaachia msalaba wajukuu zetu ambao hata hawajazaliwa.

Unadhani Nyerere alishindwa kubinafsisha madini, bandari, mbuga za wanyama? Angeweza but alifikiria vizazi vya baadae. Ila sisi tumeamua kuuza urithi wa vizazi vyetu kwa tamaa ya muda mfupi. Tukikubali huu ujinga wajukuu zetu watapiga viboko makaburi yetu.

2. Kagame aliwahi kutukejeli tumpe bandari ya DSM atupe nusu ya bajeti ya nchi kila mwaka. Tukaona ametudharau. Lakini leo tunajiuza "cheap" kwa waarabu. Hakuna cha nusu wala robo ya bajeti. Kama tumeshindwa kuendesha bandari si bora tungempa Kagame, maana heri mwendawazimu uliyemzoea kuliko kichaa mpya.

3. Kampuni ya DPWorld inatuhumiwa "kupora" bandari nchi mbalimbali kwa kigezo cha uwekezaji. Bandari ya Sarubaya (Indonesia), Batangas (Ufilipino), Palao (Peru), Dakar (Senegal), bandari ya Djibout etc. Huko kote vimebaki vilio. Badala ya kujifunza, tumejipeleka kichwakichwa tukale za uso.

4. Katika kuonesha jinsi bunge lilivyo DHAIFU, limetoa siku 1 tu wananchi kutoa maoni yao. Yani jambo litakaloathiri maisha yetu na vizazi vyetu kwa miaka 100 ijayo litolewe maoni siku 1? Hawa watu wana kichaa? Halafu maoni yatolewe ukumbi wa Msekwa, uliopo bungeni. Ebo.!

Bandari inagusa maisha ya kila mtu, kuanzia mkulima wa Runzewe hadi Mwalimu wa Ludewa. Magari, mafuta, vyakula, nguo, pembejeo vinapita bandarini. Kugusa bandari ni kugusa maisha ya kila mtu. Ingeundwa kamati kukusanya maoni nchi nzima, sio kusema watu wakatoe maoni ukumbi wa Msekwa. Mwananchi wa Namtumbo anafikaje Msekwa?

5. Wananchi kataeni upuuzi huu. Mkinyamaza kwa kuona ni jambo la kisiasa msije kulia baadae. Maana mna "kaupuuzi" ka kunyamaza mkidhani waathirika ni wanasiasa tu. Utadhani bei ya petrol inapanda(ga) kwa wanasiasa tu. Siku yakiwachachia ndo mnaomba kupaziwa sauti. Ukikaa kimya usiombe kupaziwa sauti. Sauti zetu tutapaza kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.

By Malisa GJ
-----------------------------------------------------------
 
Ni kwel atuwez sio uongo sisi warafiii sana tunaiba mpaka vinakera
 
Reactions: AHA
Hiko kiwanda sio mazava cha Morogoro kweli?
 
Hivi hizi taarifa za bandari kubinafsishwa kwa miaka 100 ni official? Nani kazitoa? Wapi na lini? Mbona TPA wanesema huo ni urongo kwani ubia ni miezi 12? Tusaidiane kujua credible source ya miaka 100 kisha tujadili. Vinginevyo tuache kuibua taharuki kwa uzushi. Nawaza tu...πŸ™πŸ™πŸ™
 
Hii akili sio ya mbongo ww unaakil kubwa sana
 
Mama sio mtananyika akimaliza mda wake anarudi mchambawima kwenda kulea wajukuu nyie mtajijua wenyewe na Tanganyika yenu
 
Sidhani kama huyu maza anajitambua,ndio mana vitabu vya dini vinasema baba ndio kichwa cha familia...2025 ccm watajua nguvu ya wananchi,halafu tunamfukuza huyo mwarabu wao
 
Degree, masters hat PHD za kitanzani ni ushuzi mtupu
 
JPM alituingiza mkenge
 
Kwa mtazamo wangu watu wengi wamekuwa wakichangia hii ishu kwa kuangalia zaidi mapato tunayoweza kutapat kama nchi lkn kuna siri kubwa nyuma ya hii ishu na siyo ya kuchangia bila fact. Nadhani ni wajibu wetu kama vijana wa Chama japokuwa sina uhakika kama bado ni kijana sana ila hii ishu tujikite tuangalie hasara kama taifa tutakayoipata kwa usalama wa taifa letu. Naamini ni hatari sana kumkabidhi mtu amiliki lango la bidhaa zote kutoka ughaibuni na sisi tukaa kimya, kufanya hivi ni hatari sana kwa usalama wa taifa na hii ni kwasababu ukiangalia kwa jicho kali unaona nia na dhumuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…