Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

NATAMANI KUWAOMBA MSAMAHA KINA CHIEF MANGUNGO
____________________
Kuna nyakati huwa Natamani Sisi Watanzania Kuwaomba Msamaha mababu zetu akiwemo Chief Mangungo kwa KUWACHEKA na Kuwa na HASIRA nao kwa kuingia Mkataba wa Ulaghai na Dr. Carl Peters wa Ujerumani ambao ndio uliidhinisha mwanzo wa utawala wa Kikoloni Karne ya 19.

Ni wazi kabisa kizazi chetu cha sasa kila kinaporejea kusoma namna mababu zetu walivyoingizwa Kingi kwenye mikataba ya ulaghai hasa kwa kumrejea Chief Mangungo wa Msowero hucheka na kuona walikuwa wajinga kiasi gani mpaka wakubali?

Lakini mababu hawa kina Chief Mangungo hawakuwa na elimu yoyote, hawakuwa wametembea sehemu mbalimbali yaani hawakuwa na exposure, mababu hawa walidanganywa kwasababu hawakuwa na elimu yoyote ya darasani na hata kutia saini walitumia dole gumba huku wakiwa hawaelewi kilichoandikwa.

Kizazi hikihiki cha baada ya Ukoloni, kizazi chenye elimu, kizazi kinachojua lugha zote rasmi duniani, kizazi cha kidigitali, kinashindwa kujiuliza na kuhoji na kuwacheka viongozi wake ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miaka ya zaidi ya 100 ambayo ndani yake kuna athari za kizazi na kizazi. Mikataba inayokuwa inamnufaisha mwekezaji zaidi na kuwanyonya wazawa.

Mikataba inasainiwa na viongozi waliosoma na kusomeshwa kwa fedha za umma na wana Degree, Masters na PhD, mikataba wanayosaini ni ya kinyonyaji na ya hovyo lakini mikataba inatetewa kwamba wawekezaji hawa wataongeza ajira na kizazi cha Kisomi kinafurahia na kushangilia, hakuna kuhoji, hakuna kuuliza. Ajira zinazoongezwa ni za Malipo ya bora mkono uende kinywani. Ajira zisizo za ukombozi wa kiuchumi.

Nimebahatika kuona mahali kwa macho yangu, Kiwanda ambacho kipo Tanzania eneo kilipo kuna makubaliano ya kimkataba miaka 100 kinazalisha nguo ambazo zinakwenda kuuzwa nje. Nguo zimeandikwa Made in China ila zinatengenezwa hapa kwetu. Kina wafanyakazi zaidi ya 400 (Mia nne) Mishahara wanayolipwa take home Yaani baada ya makato yote ni Sh. 90,000TZS na masaa ya kufanya kazi ni saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumamosi ni mwisho saa nane mchana. Makontena na makontena huingia na kutoka kila wiki. Je, huyu mwekezaji ana Faida gani kwa nchi yetu kama sio unyonyaji ni nini?
Hivi mbele ya kizazi chenye wasomi lukuki viongozi wanathubutu kusaini mkataba wa kuuza bandari ya Dares salaam kwa miaka mia moja?
Je, mkataba kama huu, ulisainiwa na Mangungo? Kwanini tuwacheke wazee wetu ambao hawakuwa na elimu yoyote?

Natamani Kuwaomba msamaha kina Chief Mangungo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.View attachment 2648183
Nadhani next time, utafikiria mara mbili kabla ya kuandika nyuzi za kuwasifia majambazi wa CCM na serikali yao!
 
Haya yatakuwa maajabu ya Karne, yaani majuzi tumegomea $12 billion za Bagamoyo kama awataki mkataba wa miaka 33 tena port wajenge wenyewe.

Halafu leo nchi isaink mkataba wa miaka 100 kwa uwekezaji wa $500m, tena kwa bandari ambazo zipo tayari.

Kama kuna ukweli ata huyo bwana godi atatususa, maana atubebeki ni gunia la misumari.
 
Ila huyo msagara katuachia laana post colonial generation walaah
 
CCM inauza nchi, vyama vya upinzani na watu wote waingie mtaani maandamano nchi nzima, kama kweli wewe ni mzalendo dawa ni moja maandamano nchi nzima kuukataa huo mkataba
 
Mimi nadhani kabla hatujaanza kulalamika na kutoa maoni kuhusu hili lazima tujue hizo terms zilivyo. Tuache kutoa maoni kwa mihemko. Lete hayo makubaliano hapa mezani tuyaone halafu ndio tuanze kujadili.
 
Rais anako ipeleka nchi anajua yeye. Yaani karne 21 ubinafshishe Bandari Kuu ya Nchi? Kitega uchumi kikuu ya Taifa! Hawa Waswazi shule ili wapita kushuto!!
Leo pia nimeona Mwigulu yupo na ma CEO wa Bank ya mikopo ya Ufaransa. Akope kwa jina la Tz. Pesa ziende kujenga Pemba!! Huu ujinga CCM kuna siku mta jibu!!
Janvsa nmemsikia akimwambia GSM kwamba sasa hivi hawabanwi kwa hiyo hizo ambazo hawabanwi wazipeleke kwenye vilabu vya mpira!

Kwa maneno mengine hapo anamaanisha kuna kodi wanakwepa ila hawabanwi kwahiyo hizo wanazokwepa wapeleke kwenye mpira!

Huyo ndio rais wa nchi
 
Haya yatakuwa maajabu ya Karne, yaani majuzi tumegomea $12 billion za Bagamoyo kama awataki mkataba wa miaka 33 tena port wajenge wenyewe.

Halafu leo nchi isaink mkataba wa miaka 100 kwa uwekezaji wa $500m, tena kwa bandari ambazo zipo tayari.

Kama kuna ukweli ata huyo bwana godi atatususa, maana atubebeki ni gunia la misumari.
Tuone tu hiyo time line...Why how? 100 years for real au huyu mwandishi anatujaza upepo? Aise itakuwa bonge la laana kama hili ni kweli, I wish iwe ni uzushi
 
NATAMANI KUWAOMBA MSAMAHA KINA CHIEF MANGUNGO
____________________
Kuna nyakati huwa Natamani Sisi Watanzania Kuwaomba Msamaha mababu zetu akiwemo Chief Mangungo kwa KUWACHEKA na Kuwa na HASIRA nao kwa kuingia Mkataba wa Ulaghai na Dr. Carl Peters wa Ujerumani ambao ndio uliidhinisha mwanzo wa utawala wa Kikoloni Karne ya 19.

Ni wazi kabisa kizazi chetu cha sasa kila kinaporejea kusoma namna mababu zetu walivyoingizwa Kingi kwenye mikataba ya ulaghai hasa kwa kumrejea Chief Mangungo wa Msowero hucheka na kuona walikuwa wajinga kiasi gani mpaka wakubali?

Lakini mababu hawa kina Chief Mangungo hawakuwa na elimu yoyote, hawakuwa wametembea sehemu mbalimbali yaani hawakuwa na exposure, mababu hawa walidanganywa kwasababu hawakuwa na elimu yoyote ya darasani na hata kutia saini walitumia dole gumba huku wakiwa hawaelewi kilichoandikwa.

Kizazi hikihiki cha baada ya Ukoloni, kizazi chenye elimu, kizazi kinachojua lugha zote rasmi duniani, kizazi cha kidigitali, kinashindwa kujiuliza na kuhoji na kuwacheka viongozi wake ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miaka ya zaidi ya 100 ambayo ndani yake kuna athari za kizazi na kizazi. Mikataba inayokuwa inamnufaisha mwekezaji zaidi na kuwanyonya wazawa.

Mikataba inasainiwa na viongozi waliosoma na kusomeshwa kwa fedha za umma na wana Degree, Masters na PhD, mikataba wanayosaini ni ya kinyonyaji na ya hovyo lakini mikataba inatetewa kwamba wawekezaji hawa wataongeza ajira na kizazi cha Kisomi kinafurahia na kushangilia, hakuna kuhoji, hakuna kuuliza. Ajira zinazoongezwa ni za Malipo ya bora mkono uende kinywani. Ajira zisizo za ukombozi wa kiuchumi.

Nimebahatika kuona mahali kwa macho yangu, Kiwanda ambacho kipo Tanzania eneo kilipo kuna makubaliano ya kimkataba miaka 100 kinazalisha nguo ambazo zinakwenda kuuzwa nje. Nguo zimeandikwa Made in China ila zinatengenezwa hapa kwetu. Kina wafanyakazi zaidi ya 400 (Mia nne) Mishahara wanayolipwa take home Yaani baada ya makato yote ni Sh. 90,000TZS na masaa ya kufanya kazi ni saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumamosi ni mwisho saa nane mchana. Makontena na makontena huingia na kutoka kila wiki. Je, huyu mwekezaji ana Faida gani kwa nchi yetu kama sio unyonyaji ni nini?
Hivi mbele ya kizazi chenye wasomi lukuki viongozi wanathubutu kusaini mkataba wa kuuza bandari ya Dares salaam kwa miaka mia moja?
Je, mkataba kama huu, ulisainiwa na Mangungo? Kwanini tuwacheke wazee wetu ambao hawakuwa na elimu yoyote?

Natamani Kuwaomba msamaha kina Chief Mangungo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.View attachment 2648183
Hakika machozi yamenitoka
 
Wewe kila mara unatumia akili zako chache kuiponda chadema na wapinzani unasahau kua nchi inachangamoto kibao zakushughulikia likiwepo lakuondoa ujinga kwa viongozi wanaopata dhamana yakuongoza.Endelea kuinanga chadema uku nchi ikiangamia.Huo ni mfano tu umejijibu mwenyewe.Sasa jiulize yako mengine mangapi.
 
Hivi wewe mporipori huwa unapata muda wa kuwaza na kufanya mambo yako kweli? Kila siku uko hapa kuropokaropoka vitu ambavyo havina maana na kupotosha ukweli!

Acha serikali iongoze nchi kwa weledi na kifuata standard za waliofanikiwa. Wewe ishi kwenye hizo nadharia zako za kijima.
Nimekosa tusi muafaka linalokufaa
 
NATAMANI KUWAOMBA MSAMAHA KINA CHIEF MANGUNGO
____________________
Kuna nyakati huwa Natamani Sisi Watanzania Kuwaomba Msamaha mababu zetu akiwemo Chief Mangungo kwa KUWACHEKA na Kuwa na HASIRA nao kwa kuingia Mkataba wa Ulaghai na Dr. Carl Peters wa Ujerumani ambao ndio uliidhinisha mwanzo wa utawala wa Kikoloni Karne ya 19.

Ni wazi kabisa kizazi chetu cha sasa kila kinaporejea kusoma namna mababu zetu walivyoingizwa Kingi kwenye mikataba ya ulaghai hasa kwa kumrejea Chief Mangungo wa Msowero hucheka na kuona walikuwa wajinga kiasi gani mpaka wakubali?

Lakini mababu hawa kina Chief Mangungo hawakuwa na elimu yoyote, hawakuwa wametembea sehemu mbalimbali yaani hawakuwa na exposure, mababu hawa walidanganywa kwasababu hawakuwa na elimu yoyote ya darasani na hata kutia saini walitumia dole gumba huku wakiwa hawaelewi kilichoandikwa.

Kizazi hikihiki cha baada ya Ukoloni, kizazi chenye elimu, kizazi kinachojua lugha zote rasmi duniani, kizazi cha kidigitali, kinashindwa kujiuliza na kuhoji na kuwacheka viongozi wake ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miaka ya zaidi ya 100 ambayo ndani yake kuna athari za kizazi na kizazi. Mikataba inayokuwa inamnufaisha mwekezaji zaidi na kuwanyonya wazawa.

Mikataba inasainiwa na viongozi waliosoma na kusomeshwa kwa fedha za umma na wana Degree, Masters na PhD, mikataba wanayosaini ni ya kinyonyaji na ya hovyo lakini mikataba inatetewa kwamba wawekezaji hawa wataongeza ajira na kizazi cha Kisomi kinafurahia na kushangilia, hakuna kuhoji, hakuna kuuliza. Ajira zinazoongezwa ni za Malipo ya bora mkono uende kinywani. Ajira zisizo za ukombozi wa kiuchumi.

Nimebahatika kuona mahali kwa macho yangu, Kiwanda ambacho kipo Tanzania eneo kilipo kuna makubaliano ya kimkataba miaka 100 kinazalisha nguo ambazo zinakwenda kuuzwa nje. Nguo zimeandikwa Made in China ila zinatengenezwa hapa kwetu. Kina wafanyakazi zaidi ya 400 (Mia nne) Mishahara wanayolipwa take home Yaani baada ya makato yote ni Sh. 90,000TZS na masaa ya kufanya kazi ni saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumamosi ni mwisho saa nane mchana. Makontena na makontena huingia na kutoka kila wiki. Je, huyu mwekezaji ana Faida gani kwa nchi yetu kama sio unyonyaji ni nini?
Hivi mbele ya kizazi chenye wasomi lukuki viongozi wanathubutu kusaini mkataba wa kuuza bandari ya Dares salaam kwa miaka mia moja?
Je, mkataba kama huu, ulisainiwa na Mangungo? Kwanini tuwacheke wazee wetu ambao hawakuwa na elimu yoyote?

Natamani Kuwaomba msamaha kina Chief Mangungo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.View attachment 2648183

BANDARI YA BAGAMOYO INAJENGWA,MAGUFULI ALISEMA HAYA, WALIKULA MABILIONI YA WACHINA AWAMU YA NNE.​

Miimi nina mtazamo tofauti na wengi. Hiyo Bandari ikodishwe tu waje Watu wenye akili walete ufanisi.
Wakimaliza waje wabinafsishe na Custom ya border ya Tunduma. Lori moja linatumia karibia dakika 20 mpaka nusu saa kupita kwenye scaner wakati kuna malori zaidi ya 500 kwenye foleni. Hakuna ubunifu ni uzembe tu. Waje tu Watu wenye akili wawekeze tu.
 
Ni wakati sasa wa kuwaomba radhi mababu zetu akiwemo Chief Mangungo wa Msovelo kwa kuwacheka walivyosaini mkataba wa Ulaghai na Dr. Carl Peters aka mkono wa damu wa Ujerumani ambao ndio uliidhinisha mwanzo wa utawala wa kikoloni karne ya 19.

Mimi Mwande na Mndewa tunamuomba radhi babu yetu Chief Mangungo wa Msovelo na Kingo Kisebengo hawakuwa na elimu yoyote, hawakuwa wametembea sehemu mbalimbali duniani kupata exposure, mababu hawa walidanganywa kwa sababu hawakuwa na elimu yoyote ya darasani na hata kutia saini walitumia dole gumba huku wakiwa hawaelewi kilichoandikwa zaidi ya kuona tabasamu la Carl Peters aka Mkono wa damu.

Digirii zetu, Masters zetu,na PhD zetu tunaweka mfukoni,wale mababu zetu walikuwa zaidi ya digrii, Masters na PhD, wale walikuwa wanafalsafa na tunajua hawakufanya vile bila faida ila hawakuwa na elimu yoyote, tendwa na mtu usiye mjua lakini sio unaye mjua na anakuja utaumia sana, huenda hatuna akili za kujiongoza kwa hiyo acha watuongoze pengine tuta tambua thamani ya kujiongoza.
 
Naona waliokunywa maji ya bendera wanashtuka, hawaamini. Imeisha hiyo!
 
Back
Top Bottom