Mahali wanapokosea sana wakubwa ni Kulinda maslahi ya mafisadi ndani ya CCM kwa kuua upinzani .Wakidhani kuwa wanakijenga Chama.
Kikwete alifanikiwa sana sana kuanza kukijenga Chama cha Mapinduzi kwa kuamua Hata kuunda katiba mpya ambayo ingejenga Taifa badala ya Chama kilichopora mamlaka na uwezo na nguvu za Mungu duniani na kukifanya kuwa Chama cha Kutengeneza miungu watu na kuwaabudu na kuwatukuza badala ya Mungu.
Nasema Kikwete alifanikiwa kuanza kukijenga Chama Cha mapinduzi sio kwa kukipa ushindi wa asilimia 100 Bali kujenga Taifa lenye vyama viwili vyenye nguvu yaani Chama cha Haki na Chama cha dhulma. Yaani ukiona kuwa unapenda dhulma Bali kule na ukiona kuwa unapenda haki njoo huku.
Kikwete alifanikiwa mpaka kuwatimua wale waliokataliwa na jamii kwa kuanzisha kauli mbiu ya kujivua gamba.
Chini ya JK Katibu mkuu wa Chama aliwakosoa wazi mawaziri waliofanya vibaya kwa Kuwaita mizogo. Leo hii Katibu Mwenezi na Katibu wake mkuu wanashindwa hata kukemea usfisadi mpaka Mwenyekiti ambaye ni Rais Mwenyewe abebe mzigo wa lawama kwa kukemea ufisadi na kuwatimua baada ya kuona mashinikizo toka mpaka nje ya nchi.
Nasema JK alifanikiwa kuanza kukijenga Chama sio kwa kutumia Bunduki na dhulma kukipa ushindi wa 100% Bali kwa kukiandaa kisaikolojia kuelejea kwenye siasa za ushindani wa Haki ,Uhuru na uwazi baada ya Kuundwa kwa Tume huru na katiba mpya.
Tulifikia pazuri mana CCM alifanikiwa kusimamia ujenzi wa Demokrasia kwa watanzania kukaa na kukosoana kama binadamu waliostarabika bila kuparurana na kuuana huku wakikaa meza moja kwenye TV na kushikana mikono kipindi kinapoisha na kurudi nyumbani kulala kwa amani.
Leo hii tumerudisha wale mafisadi na magamba yote yaliyokuwa yanagombania madaraka ndani ya Chama na Serikali.
Tumejenga Taifa lenye dhulma mbaya zaidi mana ni dhulma juu ya nafsi za watu na uongozi. Ukabila unakua kwa kasi. Chuki inakua kwa kasi. Mawazo ya magamba sasa ni kupata uoongozi bila jasho zaidi ya kupongeza na kuunga mkono juhudi.
Hakuna tena viongozi wa chini wenye kukaa na kutafakari namna ya kutatua changamoto zinazowazunguka zaidi ya kujipanga kupora fomu za wagombea wa Chama vingine na kupitia bila kupingwa.
Nani asiyetaka vyeo na uongozi unaopatikana kirahisi ndani ya CCM huku vikiwa na mafao na fursa kibao.
Chadema imeporomoka baada ya kuwakaribisha mafisadi na magamba. CCM italimaliza na kuliporomosha Taifa baada ya kuwarejesha mafisadi na magamba na hatimaye Chama hicho kikongwe kitaondoshwa na wenye nchi wenyewe bila kujali vyama Bali wataibuka wazalendo wa kweli kama upepo wa kisulisuli na kuipeperushia mbali.
CCM na uongozi wake wa sasa wamesahau kuwa mbinu wanayoitumia kuwapa watu madaraka na uongozi kwa kuwadhulumu wapiga kura itasababisha kila MTU kukimbilia humo na kuanza kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe. Kwa sasa wanajifanya wana umoja lakini umoja wao ni wa muda tuu kwa lengo la kuua upinzani. Upinzani ukifa watarudi kwenye kupigania matumbo yao kupitia uongozi. Nani asiyetaka maisha bora. Kijana gani asiyetaka kutamba kuwa Yeye anakula raha kuliko MTU yeyote.
Kujenga Mfumo wa Chama kimoja karne hii ni ngumu mno mno mno.
Baba wa Taifa aliliona hili mika 30 iliyopiata.
Vipofu hawaoni wanadhani kurudisha nchi kwenye Chama kimoja ni kupitisha kwa nguvu wenyeviti wa mitaa , madiwani na wabunge wasio na sifa za kupata kura toka kwa wananchi wanaowaongoza. Kumbe wanajenga na kuandaa watu watakaokuja kuwa sugu wa kumwaga ugali na kusema tukose wote tulale njaa wote.
Naona tunataka kutambika.
Kwa heri baba wa Taifa.
Sent using
Jamii Forums mobile app