Baada ya dilema ya muda mrefu sasa yametimia nilichokuwa nakiwaza kimetokea nini kinafuata sijui

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Wakuu nilikuwa na mtanziko wa muda mrefu kuhusu nini ni-priotize katika maisha yangu biashara au ajira au vyote kwa pamoja. Muda wote huo nilikuwa nikifanya biashara ambayo ilinifanikisha kujenga nyumba mbili na kununua viwanja kadhaa mjini (Dar) na mkoani, lakini pia niliweza kutanua wigo kwa kuanzisha vitengo kadhaa mbali na biashara mama

Nilikuwa napiga kazi sana lakini nikiwa najisemea ajira iwe lengo langu la mwisho kama kazi ya kula penshen nikiwa mambo kadhaa ya kibiashara nishayaweka sawa. Sasa nilikuwa kila zikitangazwa ajira (ualimu) nilikuwa nikiomba lakini sitilii maanani kwenye usaili kwa maana nilikuwa na sitaki nataka, sasa bana kuna hizi za october mwaka jana nikafanya hatimae nikapita oral na juzi nikapangiwa kituo aiseeeh moyo ulifanya paah!!

Hasa nikifikiria ni namna gani nitaweza ku-handle biashara na ajira kwa pamoja, hadi sasa sijaenda kuripoti dilema niliyokuwa nayo imenifikia nisijue nini kinafuata mbaya zaidi nimepangwa mbali hukoo na machakani na kuomba uhamisho ni within three years muda ambao nikicheza biashara zangu ambazo nafanyia dar zitakuwa matatani, dilema dilemani nipo gwaa nawaza what next

Unanishauri nini mdau natanguliza shukrani
 
Sijui nani aliwaambia maisha ni ajira za serikali tu, ungeajiriwa bila hizo biashara usingefanikiwa kujenga nyumba Zuri na viwanja kwa salary ya 500k, kwasababu inaonekana unapenda kuajiriwa regardless ya hatua yako kiuchumi nenda kareport then siku hizi wanaonga wanaondoka, Range ni 2m_3m hii haiitiaji ufike miaka 3.
 
Kama una mwanamke unamwamini kichwani yupo vizuri mpe hilo jukumu, halafu wewe uwe unaenda mara moja moja
Mke ninae na yupo vizur tena sana lakini purukushan za wateja na mtoto na kufungasha mzigo ni ngumu kwake muda wote yeye kazi yake ilikuwa kuuza tu mahesabu na mambo mengine nilikuw nikifanya mie sasa bora ingekuwa nimepangwa karibu ni mbali huko hata mtandao ni shida
 
Sijui nani aliwaambia maisha ni ajira za serikali, ungeajiriwa bila hizo biashara usingefanikiwa kujenga nyumba Zuri na viwanja kwa salary ya 500k, kwasababu inaonekana unapenda kuajiriwa regardless ya hatua yako kiuchumi nenda kareport then siku hizi wanaonga wanaondoka, Range ni 2m_3m hii haiitiaji ufike miaka 3.
Nipe direction mkuu ila iwe kwa nia nzuri karibu
 
Mimi sina direction zozote, lakini nimeona watu wakiacha kazi wasimamie harakati zao, nimeona watu wakiacha kazi wakajitafute nje ya ajira, nimeona watu wakipata pesa nje ya kuajiriwa na hawataki kusikia chochote kurudi kwenye ajira. Wewe huoni walimu wakitoka jioni wanaenda kuendesha bodaboda? Kwahiyo chagua fungu lako.
 
Mke ninae na yupo vizur tena sana lakini purukushan za wateja na mtoto na kufungasha mzigo ni ngumu kwake muda wote yeye kazi yake ilikuwa kuuza tu mahesabu na mambo mengine nilikuw nikifanya mie sasa bora ingekuwa nimepangwa karibu ni mbali huko hata mtandao ni shida
Kama sio chai, basi usiende huko kwenye hiyo ajira. Take off ya Biashara iko mlangoni kwako. Ukienda huko Biashara itakufa tu hiyo.
 
Mimi sina direction zozote, lakini nimeona watu wakiacha kazi wasimamie harakati zao, nimeona watu wakiacha kazi wakajitafute nje ya ajira, nimeona watu wakipata pesa nje ya kuajiriwa na hawataki kusikia chochote kurudi kwenye ajira. Wewe huoni walimu wakitoka jioni wanaenda kuendesha bodaboda? Kwahiyo chagua fungu lako.
Mkuu kuna sehem hapo juu umeandika kiwang cha mlango wa kutokea kabla ya 3yrs nilihitaj nijarib hiyo mbinu kabla maamuz ya kutoenda kuripot sijayatekeleza kama una uzoefu karibu ila uwe na nia njema
 
Wakuu nilikuwa na mtanziko wa muda mrefu kuhusu nini ni-priotize katika maisha yangu biashara au ajira au vyote kwa pamoja. Muda wote huo nilikuwa nikifanya biashara ambayo ilinifanikisha kujenga nyumba mbili na kununua viwanja kadhaa mjini (Dar) na mkoani, lakini pia niliweza kutanua wigo kwa kuanzisha vitengo kadhaa mbali na biashara mama

Nilikuwa napiga kazi sana lakini nikiwa najisemea ajira iwe lengo langu la mwisho kama kazi ya kula penshen nikiwa mambo kadhaa ya kibiashara nishayaweka sawa. Sasa nilikuwa kila zikitangazwa ajira (ualimu) nilikuwa nikiomba lakini sitilii maanani kwenye usaili kwa maana nilikuwa na sitaki nataka, sasa bana kuna hizi za october mwaka jana nikafanya hatimae nikapita oral na juzi nikapangiwa kituo aiseeeh moyo ulifanya paah!!

Hasa nikifikiria ni namna gani nitaweza ku-handle biashara na ajira kwa pamoja, hadi sasa sijaenda kuripoti dilema niliyokuwa nayo imenifikia nisijue nini kinafuata mbaya zaidi nimepangwa mbali hukoo na machakani na kuomba uhamisho ni within three years muda ambao nikicheza biashara zangu ambazo nafanyia dar zitakuwa matatani, dilema dilemani nipo gwaa nawaza what next

Unanishauri nini mdau natanguliza shukrani
Sasa pesa unayo na unajiuliza nini cha kufanya. Kula na watu wakuhamishe hata kabla hujaenda kureport.
 
Mkuu kuna sehem hapo juu umeandika kiwang cha mlango wa kutokea kabla ya 3yrs nilihitaj nijarib hiyo mbinu kabla maamuz ya kutoenda kuripot sijayatekeleza kama una uzoefu karibu ila uwe na nia njema
Yap nenda kafanye ivyo, hautakaa hata miezi 6 kama ukipata connection sahii, watu wanapitia mlango wa nyuma, faida ya serikalini kama ukifanikiwa na ukarudi kwenye shughuli zako ni uwezo wa kukopa, unakopa unaendelea kuinvest, unaweza kufanya mambo yako bila kusumbuliwa kwasababu hata mkuu wa shule na yeye ni njaa tu.
 
Back
Top Bottom