Baada ya dilema ya muda mrefu sasa yametimia nilichokuwa nakiwaza kimetokea nini kinafuata sijui

Baada ya dilema ya muda mrefu sasa yametimia nilichokuwa nakiwaza kimetokea nini kinafuata sijui

Sasa pesa unayo na unajiuliza nini cha kufanya. Kula na watu wakuhamishe hata kabla hujaenda kureport.
Sitaki kuliweka waz hili ila kama una direction nipe mkuu nipate kujiripua ila iwe ya uhakika nina degree ya utapeli kichwani (jokes)
 
Jamaa liongo mpaka linaboa..
Kwenye issue za maendeleo wengi huwa hatutaki kusikia mafanikio ya mtu hiyo ni nature ya binadamu, kwa kutambua hilo hapo nimeweka uhalisia kutokana na uzito wa tatizo langu ili niweze kusaidika la si hivyo hicho kipengele ningekiruka au ningeeleza vinginevyo, so ni juu yako uamini ama usiamini cha muhimu kwangu naomba ushauri wako mkuu ahsante
 
Kivip mkuu hebu ongezea nyama kidogo
Piga timamu kwanza kituo cha kazi ili pesa ianze kuingia, soma mazingira ujue ukiishi na nai vizuri hapo kazini kwako ya kwako yanakuendea bila bughudha.

Tena ukishathibitishwa kazini unavuta na mkopo wa maana kabisa kukuza biashara zako.
 
Piga timamu kwanza kituo cha kazi ili pesa ianze kuingia, soma mazingira ujue ukiishi na nai vizuri hapo kazini kwako ya kwako yanakuendea bila bughudha.

Tena ukishathibitishwa kazini unavuta na mkopo wa maana kabisa kukuza biashara zako.
Kuthibitishwa kazin inaweza chukua mwaka mzima au miwili kulingana na halmashauri mpaka hapo hali ya kibiashara sijui itakuwaje ndio najiuliza
 
Wakuu nilikuwa na mtanziko wa muda mrefu kuhusu nini ni-priotize katika maisha yangu biashara au ajira au vyote kwa pamoja. Muda wote huo nilikuwa nikifanya biashara ambayo ilinifanikisha kujenga nyumba mbili na kununua viwanja kadhaa mjini (Dar) na mkoani, lakini pia niliweza kutanua wigo kwa kuanzisha vitengo kadhaa mbali na biashara mama

Nilikuwa napiga kazi sana lakini nikiwa najisemea ajira iwe lengo langu la mwisho kama kazi ya kula penshen nikiwa mambo kadhaa ya kibiashara nishayaweka sawa. Sasa nilikuwa kila zikitangazwa ajira (ualimu) nilikuwa nikiomba lakini sitilii maanani kwenye usaili kwa maana nilikuwa na sitaki nataka, sasa bana kuna hizi za october mwaka jana nikafanya hatimae nikapita oral na juzi nikapangiwa kituo aiseeeh moyo ulifanya paah!!

Hasa nikifikiria ni namna gani nitaweza ku-handle biashara na ajira kwa pamoja, hadi sasa sijaenda kuripoti dilema niliyokuwa nayo imenifikia nisijue nini kinafuata mbaya zaidi nimepangwa mbali hukoo na machakani na kuomba uhamisho ni within three years muda ambao nikicheza biashara zangu ambazo nafanyia dar zitakuwa matatani, dilema dilemani nipo gwaa nawaza what next

Unanishauri nini mdau natanguliza shukrani
Hapo ndipo unapohitaji mifumo kwenye biashara yako ili uwe unai-monitor wakati upo kazini
 
Daa yaani uache biashara ambayo umejenga hadi nyumba ukimbilie ajira ya kupata take home laki tano. Labda kama unadanganya ulikuwa huna any pangu pakavu
Wahenga husema usiolijua ni sawa na usiku wa giza, hii ikimaanisha uzoefu wa kwenye ajira sina lakini pia tamaa ya kuongeza wigo wa mapato ilinisukuma pia huku nikiwa najipanga kuajiri watu sasa hili limetokea kabla sijafika tamati

Lakini pia mkuu take home ni 720k sio lk5 labda uwe na deni la helsb
 
Achana hiyo ajira ya porini biashara yako ukimuachia mtu hata huyo mke itakufa na ndoa ya mbali sio ndoa.

Hakuna jipya huko watu wanaacha kazi na hawana hata mia ili waje kujitafuta town wewe ndio unataka kwenda huko. Shauri yako ukienda baada ya muda utajuta.

Kuhama ni ngumu sana hasa kutoka vijijini kuja mjini na hasa kwa mwanaume hata kama ukitimiza miaka 3. Hata ukitoa hela italiwa bure kwa sababu zoezi la kuhams linahusisha watu wengi na ni kwenye mifumo.

Kuwa makini usiende kupata sonona huko bure. Kila la heri.
 
Kwanza mkuu jenga biashara inayojiendesha yenyewe haitegemei uwepo wako utakuwa na uhuru wa kuajiriwa lakn kama pote panakuhitaji chagua biashara
 
Kuna walimu wanaacha kazi waende wakawe huru kwenye harakati zao, wengine wanashindwa kukidhi mahitaji wanaamua kuwa bodaboda kupanga ni kuchagua

Kabisa kaka wengi nawajua wametoka huko vijijini wameacha kazi wanakuja kuwa huru kufanya kazi zao.

Hii ni sawa na ile mwanafunzi anapangiwa kozi kwa sababu tuu anapenda UDSM anaenda kusoma kozi ya ajabu anaacha kozi nzuri chuo kingine. Baada ya kuhitimu anakuja kujilaumu.
 
Back
Top Bottom