Baada ya dilema ya muda mrefu sasa yametimia nilichokuwa nakiwaza kimetokea nini kinafuata sijui

Mkuu sioni haja ya wewe kwenda porini wakati una biashara zinazofanya vizuri hapo mjini. By the way hakuna tajiri ambaye ameajiriwa. Za kuambiwa changanya na zako.
 
Kama nitafuata huu ushauri nitaomba rikizo bila malipo kwanza nisome mchezo kabla sijaamua kuumpa mkulugenz pesa za bure
 
Kwanza mkuu jenga biashara inayojiendesha yenyewe haitegemei uwepo wako utakuwa na uhuru wa kuajiriwa lakn kama pote panakuhitaji chagua biashara
Haya ndio yalikuwa malengo yangu sema ajira imewahi kunifikia kabla sijaset mipango vizuri
 
Kama una kiu ya ajira kareport kituo cha kazi ulichopangiwa, taarifa zako za kiutumishi zikishakaa sawa anza kuangalia namna ya kuhamia Dsm chap.
Hapo kwenye kuhama ndio kipengele but ngoja nione ahsante mkuu kwa ushauri
 
Kama nitafuata huu ushauri nitaomba rikizo bila malipo kwanza nisome mchezo kabla sijaamua kuumpa mkulugenz pesa za bure

Likizo bila malipo umeshakuwa umtumishi halali wa pale. Ni mpaka uthibitishwe kazini kitu kitakacho chukua zaidi ya mwaka na nusu hiyo biashara itakuwa bado hai kweli. Na hata ukithibitishwa unaweza kukubaliwa hiyo likizo au usikubaliwe na ukikubaliwa wakati wa kurudi wataangalia kama wanakuhitaji au laa je kama washapata mwingine sio wanakuacha.

Mimi na mashaka na hiyo biashara yako unayosema kama ingekuwa kweli ni kubwa sidhani kama ungetamani kwenda kuwa mwalimu huko vijijini uache biashara nzuri ipotee.
 
Haya ndio yalikuwa malengo yangu sema ajira imewahi kunifikia kabla sijaset mipango vizuri

Hata kama una mifumo bila kuwepo na wewe mara kwa mara itakwama tuu. Watu wana tamper mifumo lakini pia kuna mambo mengi nje ya mifumo kama haupo huwezi kuyaona na yatapelekea biashara kufa.
 
Mimi na mashaka na hiyo biashara yako unayosema kama ingekuwa kweli ni kubwa sidhani kama ungetamani kwenda kuwa mwalimu huko vijijini uache biashara nzuri ipotee.
Sijajua humu ili uwe na biashara unatakiwa uwe na biashara ya aina gani na yenye mtaji kiasi gani. Ila kwangu mimi biashara niliyoijenga kwa miaka 7 sasa ni kubwa kuliko hizo ambazo mnataka nyie hata kama ni yakuuza mitumba
 
Dah hilo nalo neno, ahsante kwa ushauri mkuu let me calculate the risk
 
Hapo kwenye kuhama ndio kipengele but ngoja nione ahsante mkuu kwa ushauri
Kama umezoea life la mjini, kijijini utaacha ndala mkuu.
Kitakachofuata hapo utabobea kwenye utoro maana utakuwa haukauki kwa mkeo na kwenye biashara yako.
 
Kama umezoea life la mjini, kijijini utaacha ndala mkuu.
Kitakachofuata hapo utabobea kwenye utoro maana utakuwa haukauki kwa mkeo na kwenye biashara yako.
Sio kirahisi hivyo Dar to machakani huko ni mwendo wa siku mbili yaani masaa 28 na nauli ya kwenda
 
Unaomba ushauri wa aina gani kama jibu tayari unalo? Do what benefits you the most, ajira zipo tu, lakini kwenye kujiajiri unajipangia income yako mwenyewe kutokana na your level of investment.
 
Hiki ndo kipindi usipokuwa makini unapotea, na utatumia miaka mingi kidogo kukaa sawa, kuwa makini Sana, Ushauri wangu amini Sana Ile akili ya mwanzo au wazo la Kwanza kabisa lile ndo sahihi
 
Unaomba ushauri wa aina gani kama jibu tayari unalo? Do what benefits you the most, ajira zipo tu, lakini kwenye kujiajiri unajipangia income yako mwenyewe kutokana na your level of investment.
Kuna watu wameajiriwa huku niwafanya biashara ndio naomba kwao ushauri pia
 
Hiki ndo kipindi usipokuwa makini unapotea, na utatumia miaka mingi kidogo kukaa sawa, kuwa makini Sana, Ushauri wangu amini Sana Ile akili ya mwanzo au wazo la Kwanza kabisa lile ndo sahihi
Ni kweli ngoja nione with time kila kitu kitakaa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…