Uchaguzi 2020 Baada ya Dkt. Kigwangalla kujibizana na Mo Dewji Twitter. Dkt. Bashiru amshukia Kigwangalla, amtaka am-tweet Dkt. Magufuli

Uchaguzi 2020 Baada ya Dkt. Kigwangalla kujibizana na Mo Dewji Twitter. Dkt. Bashiru amshukia Kigwangalla, amtaka am-tweet Dkt. Magufuli

tunapangiana hadi cha kuongea ?, mwisho wa siku watapangia watu wapi pa kuweka nukta na koma, au wapi pa kucheka na kununa....
 
Dr Bashiru amemuagiza waziri Kigwangala kuacha mara moja kutupiana maneno na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa simba Mohammed Dewj.

Amemtaka badala ya kujibishana mambo ya mpira, hizo nguvu azitumie kumpigia kampeini mwenyekiti wa ccm ili ashinde.

Hakika huu ni uingiliaji wa mambo binafsi ya mtu, maana kupenda soka ni mambo binafsi. Sasa wamefikia hatua ya kupangiana nini cha kupenda.

Hakika ccm sasa ipo icu.

Tanzania bila ccm inawezekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jidanganye
 
alilolifanya Bashiru leo inaonesha jinsi gani chama mapinduzi kimekomaa kimaadili najinsi wanvyoheshimu madaraka ya kila mmoja wao kwenye uongozi wa chama hicho
mimi ninawapongeza wanachama wa chama hicho wote hasa kwa HK mwenyewe baada ya kutoka hadharani kwenye mtandao wa twitter na kukiri kupokea maelekezo hayo na kuyatii licha ya umaarufu wake
that is great
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla kumzungumzia Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Magufuli badala ya kuendelea na malumbano yake yanayohusu mpira dhidi ya Mmiliki wa Simba SC, Mohammed Dewji

Dkt. Bashiru amaema“Naona Hamis Kigwangalla yupo mitandaoni kujibizana na Mohammed Dewji mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi. Nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda.”

Ameongeza, “Siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM"

Dkt. Kigwangalla na Mo Dewji walianza kujibishana mtandaoni baada ya Kigwangalla kuhoji namna alivyopatikana CEO mpya wa Simba ambaye anaelewa kuwa PA wa Mo Dewji

Katika kujibu hoja hiyo Mo aliendelea hadi kumuomba msamaha Waziri Kigwangalla kutokana na mkopo wa pikipiki kutofanikiwa (hali iliyotafrisiwa kuwa Mo anadhani Kigwangalla anafanya hivyo kutokana na kunyimwa mkopo)

Hata hivyo, Kigwangalla aliendelea na kusema mkopo hauhusianj bali tu yeye anahoji kama Mwanachama wa Klabu ya Simba. Aliweka bayana barua pepe aliyoombea mkopo wa pikipiki na pia alionesha tweet zake za nyuma ambazo pia alikuwa a ahoji mambo kadhaa ndani ya Simba

Tunasonga mbele kwa kishindo, tunaiishi falsafa ya kujisahisha.
 

Attachments

  • IMG-20200906-WA0087.jpg
    IMG-20200906-WA0087.jpg
    108.3 KB · Views: 1
Angemuonya moja moja kama unavyojaribu kuliweka mm nisingekuwa na nongwa. Lkn Bashiru kasema Kigwangalla amtafutie kura mwenyekiti wake.
sahihi lakini bado ingeendelea kuleta mjadala kwa wapenzi wa twitter kwa vile HK angeonekana kuukimbia mjadala
ili isilete maneno ilimpendeza kutoa maelekezo kwa kuwa ni kazi yake kufanya hivo muda wowote na mahali popote ili kudumisha mazingira mazuri kwa wanchama na chama kwa ujumla, wakati huo kumbuka kuwa mo ni mwanachama wake pia kwahiyo hayo yalikuwa ni maelekezo kwa wote
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Bashiru Ally mchana wa leo ametoa maelekezo kwa wagombea wa Ubunge kubaki katika maeneo yao ya jimbo na kufuata maelekezo na taratibu zilizopangwa na Kamati za Siasa za Wilaya husika. Katibu Mkuu amewataka wabunge kuzingatia ratiba za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ratiba za Kamati za Siasa za Wilaya kuungana na Viongozi wengine kuwatafutia Kura wagombea Udiwani pamoja na kumuombea Kura mgombea Urais wa CCM Ndugu John Pombe Magufuli.

Sambamba na maelekezo hayo, amewataka wabunge kutumia mitandao ya kijamii katika kutafuta kura za Chama Cha Mapinduzi kwa kufafanua ilani yetu ya Chama kwa mwaka 2020- 2025 kwa kuwaeleza wananchi kipi kimetekelezwa na kipi tunatarajia kukitekeleza pamoja na kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura siku ya tarehe 28 Oktoba 2020.

Nidhamu ya Chama inatuongoza kusikiliza maelekezo ya Viongozi wetu na bila kinyongo kuyatii na kujisahihisha.

Tunasema tumesikia na tumetii...!

View attachment 1560618View attachment 1560618View attachment 1560620

Siku zote wanasema mitandaoni hakuna wapiga kura, leo wanageuka tena na kujikata mitama na kuwataka wagombea kuomba kura mitandaoni. Kweli siku ya kufa nyani, miti yote huteleza
 
Siku zote wanasema mitandaoni hakuna wapiga kura, leo wanageuka tena na kujikata mitama na kuwataka wagombea kuomba kura mitandaoni. Kweli siku ya kufa nyani, miti yote huteleza
Acha kujitoa fahamu, kuna sehemu katibu Mkuu amesema watu waombe kura mitandaoni?
 
Back
Top Bottom