Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Kitendo cha kamanda SIRO Kumuacha Makonda akitamalaki na vyeti Feki hapa Dasalaam inaonyesha kiongozi wa kanda Maalum anapwaya.

Makonda aliwahi kuhoji utendajikazi wa kamanda Siro kuwa haukizi viwango. nimeanza kuamini,kelele zetu zote hizi na inteligensia zake ameshindwa kufungua jarada la uchunguzi dhidi ya Daudi Bashite! only in Tanzania.

forgery is a criminal offence in the eyes of the law Kamanda Siro!
Mkuu forgery haipo katika makosa ya kufanya "fyokofyoko" unamlaumu bure kamanda Sirro
 
Hii nchi tushajazwa woga! Ukijifanya shujaa unaweza kosa kibarua aisee! Huyo Mange alieanzisha sakata la Bashite yuko US huko anakula bata na hela za child support... Sasa wewe na kibarua chako ukurupuke tu kumuiga gwajima anaelishwa na kanisa kama haujaishia kurudi kijijini kulima.
"Wisdom is profitable to direct"
 
Waandike habari za Daudi halafu waishie kutajiwa nyeti za wazazi wao? Kwanini mamlaka yenye uteuzi au tume ya maadili isimuhoji juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake.
 
Gwajima si amesha fanya na majibu aliyaweka wazi kila mtu alisikia
 
Tofauti haipo mkuu. Uko sahihi. Hata hivyo haya mambo hapo zamani yalikuwa ya kawaida sana. Watu wengi hawakupenda shule kwa kuwa waliamini maisha si shule. Watu waliopenda shule waliappeal na kutumia majina ya watu. So, kwangu hakuna kesi kiivyo. Kama mtu anaperform aachwe maana vyeti is not an issue. Kuna watu wana vyeti but they have no brain. Let vijana wafanye kazi na tuache majungu.
We unaongea nini? Kuna ndugu zetu wamefukuzwa kazi bado mwaka mmoja wastaafu na wamekosa haki zao zote.... Leo out wee unasema kinachofanya kazi sio cheti?
 
Daudi bashite [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuna siku Sirro naye ataonyesha hasira zake baada ya kuambiwa analipwa milioni tano tano na wauza shisha. Mtu mzima hakurupuki kulipa kisasi. Siku akimwona Daudi kaingia kwenye anga zake ndio mtajua kuwa maneno yale ya kusingiziwa kupokea mlungula wa shisha yalimuumiza sana mtu mzima!
 
Mwigulu hakufeli bali aliacha shule kwenda kuchunga mbuzi, kisha akarudi shule kwa jina hilo, alisoma yeye mwenyewe, akafaulu, akasoma shule ya vipaji Ilboru, akatoka na Div one kali, akaenda chuo kikuu akatoka na 1st Class akaajiriwa BOT.

Daudi Albert Bashite alisoma kijijini akafeli, akaenda kurudia mjini, akafeli, akapiga dili kuchukua nafasi ya mtu aliyepasi hivyo akasoma shule ya serikali kwa jina jingine, akapata Div 0. Ndipo mrembo Christina akampa cheti cha kaka yake Paul Christian alichowasilisha kusomea chuo.

Makonda amefoji jina na kufoji cheti, Mwigulu amesomea jina la mtu mwingine.
Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli
Paskali
Acha uongo Paschal,Mwigulu hakupata Division One kali Ilboru alipata Division One ya kawaida ya kawaida ndo maana 1998 aka-join Mazengo High School.Wenye Division One kali walikuwa wanaenda Mzumbe,Ilboru,Tabora Boys na Kibaha. Hata pale Mazengo alitoka na Division Two ya point 10 akiwa na E ya Uchumi (alisoma EGM -ECONOMICS alipata E,Geography alipata C na Mathematics alipata B) ,ambao ni ushindi wa kawaida kabisa miongoni mwa ma-"bookworms"!
Hata pale Mlimani First Degree hakupata First Class bali alipata Upper Second! Tatizo ni VI.LA.ZA walioshindwa kuelewa pale alipofikia nafasi ya Mchumi daraja la kwanza (Senior Economist) pale BOT wakajua Mchumi daraja la Kwanza ni First Class,hiyo ndo tatizo la elimu ya Tanzania ya kukariri mambo! Hivyo Paschal Mayala fanya research yako kama unabisha haya!
 
Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.
Mwambie aliyemuajiri amutimuwe huyo mbowe maana unampenda sana.
 
Nakumbuka matokeo ya Ole sendeka, ya ziro yalisambazwa vp ya makonda
 
Analindwa na FJ maana ndio anaemtumia na ni home boy sasa anaona aibu afanyeje? Anataka kulazimisha hajui effect yake kumbeba na kashfa nzito kama hiyo!!!! Atafute sababu amtoe!!
 
Wana Jamvi nimekuwa nikiangalia na kuona MAWE anayotupiwa RC Makonda kuhusu madai yanayohusu uhalali wa MAJINA na ELIMU yake.

Ninapoandika hivi sisemi Makonda hana mapungufu katika maamuzi na utendaji wake hasa wa juzi juzi, hata hivyo tukiangalia upande mwingine wa SARAFU yaonekana kuna ZAIDI ya CHETI, bali ni kutaka huyu RC afukuzwe kazi, ili WENGINE WAFURAHI.

Kwanza kabisa PROFILE ya Makonda ILIVUJWA maksudi kwa sababu ya watu walio na SABABU zao mbaya ili aonekane mbele ya Mwajiri wake ambaye ni rais kwamba yeye ni MHALIFU mkuu.

Na hivyo KUJARIBU kum influence mwajiri wake indirectly kutumia BLACKMAIL ili AMFUKUZE kazi.

Jambo hili limeendelea kwa muda sasa. Swali langu wanajamvi. Kabla ya kumtupia mawe turudi NYUMA.Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa na issue kama hii, mbona ya Makonda kila mtu ANAMTUPIA MAWE?

Ni vizuri tusiwe na DOUBLE STANDARD katika kutoa haki bali tuwe FAIR/na USAWA. bila WIVU, UBAGUZI , na FITINA. Kama Waziri Mwigulu Nchemba HAKUJIUZURU basi TUMWACHE Makonda afanye kazi. Yeye si mkamilifu mara nyingi AMEJIKWAA je hilo ndo tumpe mob justice wampige mawe. ASIYE na DHAMBI na awe wa Kwanza kutupa JIWE!
halafu huwa siwapendi watu kama nyie ndo mnafanya taifa linaangamia hv unafurahia makonda kutumia cheti cha mtu hawezi kufanya kaz kwa weledi sababu ni mbumbumbu halafu ww li mtu lizima hebu kuwa na akili shule ni muhimu ktk utendaji ukimsemea mwigulu huyo hajawahi kufeli alitumia jina la mtu kusoma cheti ni chake
lkn makonda ametumia cheti cha mtu kichwan empty
 
Back
Top Bottom