Baada ya Hayati Magufuli kuombewa Chato, Mwanza nao wanaandaa maombi, binafsi naona haya yanayofanyika baada ya Chato yako kimkakati

Hivi kwann hapa kwetu Tanzania, vibaraka wa, mafisadi pamoja na mafisadi kama January Makamba et al. wanatulazimisha tumuchukie JPM? Angalia huu Uzi wa chinembe ambaye naamini hana hata kaz za kujiajiri au kiajiriwa, anawapinga maelfu ya watu wanaoamini katika falsafa za JPM wasimkumbuke. Ndugu chinembe, naandika jina lako kwa elfu ndogo kuonyesha kuwa nakudharau sana sana. Hivi hao wahuni wenzako wanaokutuma umwandike vibaya JPM, waulize kwanza waliwahi kufanya nn cha maana ili nao wakifa wakumbukwe. Wambie pia,kupewa vyeo vya serikali kwa migongo ya wazee wao,ndio kumeturudisha nyuma kama taifa. Hipo siku nchi itarudi kwa watoto wenye akili sio wao. Hakika JPM alikuwa zaidi ya JK wa Butiama, na amekataa kabisa kufa.
 
Naona leo umemkiri Yesu Kristu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako, Hongera Sana.

ASANTE SANA,SASA WASHAURI NA WENZAKO WAACHE KUPOTEZA MUDA,YESU ANAFUFUA WAFU,WAPELEKE MAOMBI YAO KWA ASKOFU GWAJIMA ILI POMBE AFUFULIWE NA KAZI IENDELEE,SAWA??
 
Kwani shida yako ni nini?swala la maombi ni la watu binafsi na halipaswi kuhusishwa na udini hata kama ataombewa nchi nzima ni haki yao ya kuabudu.
 
Hivi from, Christian perspective, kumuombea mtu aliyekwisha kufa kuna faida gani? Si wanasema ukifa ukiwa hujatubu na kuomba msamaha unaenda motoni au ukiwa tayari unaenda mbinguni...je kuombewa kuna badilisha nini kama Mungu alishafanya maamuzi?
Kwani nyie waislamu hamuombei wafu wenu ?kama hamuombei mtajijua wenyewe mtuache wakristo na utaratibu wetu hayo mengine nenda kasome biblia
 
Sawa
Sasa muache pia mijadala ya kidini sasa dili na imani yako tetea imani yako sio unatetea imani yako kwa kuwaumiza wenzio.
Msitaki kila mtu aamini mnachoamini nyie ila nimependa pale ulipomkili yesu hongera sana
 
wew iko shida upstairs
anaombewa mwingine wew waleta makasiriko
punguza udini tafuta wafu wako nawe uwaombee
 
Hawa watu wanamuombea JPM kuliko hata Nyerere. Nadhani hii imekaa kimkakati ili kupandikiza hisia za udini katika jamii, hasa ukizingatia hawa jamaa huwa hawaridhiki nchi ikiwa na uongozi tofauti.
Mtazamo wako tu huo, ila sema kwakuwa tu kuna wanasiasa wanatamani kushiriki ila imani haziwaruhusu ndiyo maana unaingiza hayo mawazo
 
Eti wanamuombea jpm kuliko Nyerere, acha uongo wako au dhihirisha kwa takwimu. Hatudanganyiki.
Mkuu,

Hata wakimuombea JPM kuliko Nyerere, kwani tatizo liko wapi?

Kuna mashindano ya kuombewa ambayo Nyerere akizidiwa kutakuwa na hatari ya kitaifa?
 
Hivi kuna uwezekano siku moja JPM nae atakuwa anafanyiwa mchakato na kanisa lake wa kutangazwa mtakatifu eh? Maana duniani kuna mambo.
Sio rahis kama unavyodhani, lazima uwe approved na roma
 
Mkuu,

Hata wakimuombea JPM kuliko Nyerere, kwani tatizo liko wapi?

Kuna mashindano ya kuombewa ambayo Nyerere akizidiwa kutakuwa na hatari ya kitaifa?
Hao wamelenga siasa
 
Hao wamelenga siasa
Hata kama wanalenga siasa, inabidi uwe na uthibitisho kabla ya kusema hilo.

Jipenyeze humo uwarekodi upate uthibitisho usiopingika. Ukisema wanalenga siasa, uwe unasema hilo kwa uthibitisho.

Sasa hivi, ukisema wanalenga siasa, hujajitofautisha na mtu mwenye wivu tu anayeona Magufuli anapendwa sana, akaona wivu, akataka kuwanyima watu haki yao ya kumuombea marehemu.


Thibitisha wanalenga siasa. Usiseme tu.

Kusema kila mtu anaweza. Uthibitisho ndiyo kazi.

Mtu mwingine anaweza kusema wewe ndiye unafanya siasa chafu za kuwanyamazisha watu wasimuombee mpendwa wao wanavyotaka.

Unataka kuleta siasa za ku control mpaka imani za watu na jinsi wanavyoombea wafu.
 
Biblia haijaandika kila kitu. Usikremu.
 
Hii Imeenda vizuri kweli kweli
 
ASANTE SANA,SASA WASHAURI NA WENZAKO WAACHE KUPOTEZA MUDA,YESU ANAFUFUA WAFU,WAPELEKE MAOMBI YAO KWA ASKOFU GWAJIMA ILI POMBE AFUFULIWE NA KAZI IENDELEE,SAWA??
Inapendeza sana ulivyomkiri Yesu Kristu ndani ya mwezi mtukufu.
 
Huu nao ni uchawi.
Mbona mnafanya Dua na kuchinja nyama mkitoka kusafisha makaburi ile eid nini sijui.
Wakristo hawalalamiki mnapandikiza udini wakati wa raisi mkristo?
 
Raha iloyopo katika threads za JPM katika ya reply 100 ni 10 tu ndio za wahuni wanaompinga mwamba, 90% wanamwaga maua tu.

Sharout kwenu watu wa Mungu wa nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…