..kuna upotoshaji ktk hoja alizitoa Tundu Lissu.
..anachopinga Lissu ni udanganyifu waliofanyiwa na Ccm wakati wa mazungumzo ya maridhiano.
..hata Mbowe alikuja hadharani na kukiri kwamba Ccm wamekataa mapendekezo ya Chadema hivyo mazungumzo yamevunjika.
..wafuasi wa Mbowe wanamshambulia Lissu kwa jambo ambalo Mwenyekiti, mgombea wao, anakubaliana na msimamo wa Lissu.
..nimeshangaa pia msomi kama Dr.Lwaitama na yeye kuingia katika mkumbo wa kupotosha hoja ya Lissu kuhusu maridhiano.
..kama maridhiano yalifanikiwa kwanini makada wa Chadema wameuwawa, na uchunguzi wa matukio yao haufanyiki?
..kama maridhiano yalifanikiwa, kwanini uchaguzi serikali za mitaa ulivurugwa?
Viongozi wote wali wana-yakataa maridhiano baada ya kuwa wameshakaa na kuyakubali, kitu walichosema ni kwamba CCM walikataa kuweka mazungumzo kwenye maandishi, maana yake CCM walikataa mazungumzo yasiwe mkataba wa makubaliano, ingawa wao wote wanakili kuna mambo walikubaliana ingawa hawatuambii ni nini walikubaliana na ni kipi hawakukubaliana.
Kinana aliyekuwa katibu mkuu CCM alisema mazungumzo yalikuwa yanaendelea lakini chadema walijitoa katikati ya mzungumzo.
Wao chadema wakasema ccm ilikataa kuwa committed yani kuyaweka kwenye maandishi na pande zote zinazokubaliana zi sign kama declaration.
CCM haitaki maandishi inataka MAZUNGUMZO bila committment yoyote.
Lakini Lisu na Mbowe ni sehemu ya walioshiriki maridhiano hayo hadi yalipoishia, hayakuwa ya Mbowe peke yake kama tunavyotaka kuaminishwa.
Msingi wa Dr.Lwaitama ni kwamba, mazungumzo yalikuwepo, licha ya kwamba kuna sehemu hayakutekelezeka lakini yalikuwepo, na hayakuwa kati ya Mbowe na ccm, bali ni CDM na CCM.
Na anaendelea kwa kusema, vyama lazima mzungumze mnapokuwa mna hitilafiana, na aka hoji sasa yeye Lisu anaposema hataki mazungumzo, maana yake yeye anataka vita, au atatumia njia gani kukaa na vyama vingine yanapotokea mahitilafiano?
Maanadamano pekee siyo solution ndio maana, Dr,Laitama akasema maridhiano yalikubaliwa na kamati kuu siyo Mbowe, na hayakuwa maridhiano ya Mbowe na CDM,bali CDM na CCM.
Kinachotushangaza Team Lisu wanasema, maridhiano ya Mbowe na CCM yametufikisha wapi?
Yani Lisu anajitoa ufahamu, na kujiona yeye ahusiki, na hata kama hakuhusika, labda tuseme alikuwa mgonjwa.
Lakini yalikuwa ni maamuzi ya kamati kuu, ni chombo cha chama, na siyo Mbowe kama Mbowe.
Kitu ambacho Lisu hataki ku acknowledge.