Wanaojiita Team Lisu hawana tofauti na Team WEMA, yani wao kila hoja inayopingana na Lisu wanapinga, kwa sababu kwao wao hoja za Lisu ni kama Msahafu/biblia hawataki akosolewe, aambiwe ukweli.
Team Lisu wanasema Mbowe dikteta, Mwizi, na kila kitakachowajia akilini wakati huo. Hapa wao tayari wamesha hitimisha na wanasema anamtetea Mbowe. Kisa ni kwamba majibu hayakuwapendeza wao. Sasa wameanza kusema Lwaitama ni Team Mbowe.
Hawajali aliongea katika muktadha upi, ana alikuwa anaongea nini na nani.
Lisu ni mwanasheria mzuri, na anaelewa maridhiano ni nini?
Walipoitwa kuyafanya angepitia agenda, na kukishauri chama, yeye ni makamu mwenyekiti wa chama, ni mtu mwenye turufu ya maamuzi.
Na kama alishuri atuletee, alishauri nini kikao gani na wajumbe waliafikiana vipi hadi kukubali kukaa na CCM, na tukaambiwa wameafikiana vitu fulani fulani kwenye maridhiano yao.
Lakini wao ni kupiga kilele, na kukataa kila kitu kilichoamuliwa na chama, unaweza kusema ni wageni chamani, na hawakuwepo kila kitu kilipoamuliwa.
Hawamtaki Mbowe, lakini wasikilize hoja kisha waje na maswali. Hawataki badala yake wao ni kuponda tu.
Lisu tangu amekuwa makamu mwenyekiti, alifanya nini, na alipungukiwa nini kinacho wafanya muamini akiwa mwenyekiti, atatekeleza alichoshindwa kwa sababu ya nafasi yake kuwa makamu mwenyekiti?