Pre GE2025 Baada ya Hotuba ya Lissu, Mbowe, Dr Azavel naye azungumzia nguvu ya pesa, vigezo vya mgombea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nifah, Please give your views on the issues raised by Lwaitama. Umechukua njia ya ad hominem kujibu hoja zake.
 
Hivi unaweza kutupatia mabadiliko ya uongozi wa vyama cha conservative na Labour upoje, ili kuhalalisha Mtu akaye miongo miwili au zaidi
 
Huna point
 
Nacho shangaa hadi sasaa ni kua, mbowe hasemi nini atafanya kwa hii miaka mitano ambacho hakuweza fanya kwa miaka 20😳😳😳😳.

Pilli akigoma tena kuondoka baada ya miaka mitano watamteteaje tena?,ikumbukwe huko nyuma zama za zito kabwe aliomba aaichiwe muhula mmoja tuu kisha angeondoka, ila hadi sasaa yupoooo
 
Lissu alisikika akisema kuwa wao (CDM) walitoa matakwa (masharti yao) ili maridhiano na CCM yafanyike. Kwamba haki zao zote za kikatiba zirejeshwe: ikiwa ni pamoja na mikutano ya kisiasa kuruhusiwa, kufutwa kwa kesi za kubambikiwa na kuachiwa kwa watu wao wote walio mahabusu na magerezani kinyume cha sheria na katiba, n.k. I guess I’m right.

Swali. Je, hayo YOTE yalifanyika kabla CDM hawajaingia kwenye mazungumzo ya maridhiano au la? Kama hayakufanyika, kuna guarantee yoyote waliyopewa CDM kuwa yatatekelezwa - along the way - hivyo wasiwe na shaka, mazungumzo yafanyike tu?

Kauli ya Lissu inaonyesha viongozi wakuu wa CHADEMA hawakuwa na uelewa mmoja kuhusu malengo (objectives/targets) na matokeo tarajiwa (deliverables) ya maridhiano - ambayo ni mambo ya msingi kabisa. Ni jambo la kushangaza sana kwa watu tuliofikiri wana akili zenye upeo wa juu kama Mbowe na Lissu.

Kwa vyovyote vile sasa ni dhahiri kabisa kuwa ama wote wawili (Mbowe/Lissu) au mmoja wao amefhamiria kubomoa ROHO ya CHADEMA kimoja. Ama kwa kutojua au kwa makusudi kabisa wote au mmoja wao anatumikia vyema ajenda ya muda mrefu ya chama tawala ya kuangamiza nguvu ya upinzani nchini.

Mbowe kwa upande wake taswira yake imeshachafuliwa sana kiasi kwamba akishinda uchaguzi na kubaki mwenyekiti, basi kuna uwezekano wanachama na wananchi wengi wataacha kusimama na hicho chama.

Lissu kwa matamshi yake anaijenga na kuikuza taswira yake binafsi kwa kuichafua CHADEMA kama chama ambacho “kimewatapeli” wananchi kwa muda mrefu kikijidai cha kidemokrasia kumbe kinashirikiana na dola kufanya ufisadi na baadhi ya maovu kwa wadau wake! Akishinda uchaguzi basi atakuwa mwenyekiti wa chama duni sana na atajikuta ana kazi nzito ya kukijenga upya na kurejesha imani ya wananchi ambayo ndiyo “jeuri” ya muda mrefu ya CHADEMA single-handedly!
 
Profesa Lwaitama ni moja kati ya wasomi wasio na principles!Kuwa msomi usiyejulikana unaamini nini na unasimamia nini na kwamba you are ready to die on your course hakuna tofauti na kuwa mhuni wa mtaani!Hakuna profesa hapo
 
..mimi kwa upande wangu niliona maridhiano yale yalikuwa na walakini kwasababu yalikosa msuluhishi wa kuyasimamia. pamoja na hayo niliwaamini viongozi kwamba wana nia njema, lakini baada ya kuvunjika tumejua kwamba kulikuwa na ulaghai.
Neno ulaghai ni kali sana. Lissu anatuambia kuwa Heche alikuwa upande wake na wote tuliona kuwa Heche alihusika kikamilifu. Tunaambiwa ( nadhani hili hata Lissu alilithibitisha) kuwa Kamati Kuu ilikuwa inapewa taarifa kuhusu kila hatua. Tatizo lililotokea ni kuwa baada ya majadiliano kukwama upande wa Lissu ukataka kumtupia lawama zote Mwenyekiti wao. Kwangu mimi hapo ndipo mbegu ya mapinduzi ikapandwa. Hauwezi kusema, with a straight face, kuwa CDM ilipoteza muda wake kwa kuingia katika yale mazungumzo.
Kwa bahati mbaya Lissu hasemi wazi mpango wake wa kulazimisha mabadiliko. To his credit, alimnyamazisha ha Kigogo24 aliposema kuwa inabidi CDM ifikirie kuingi misituni. Lakini kama hataki violence, anataka nini?

Amandla...
 
Hivi unaweza kutupatia mabadiliko ya uongozi wa vyama cha conservative na Labour upoje, ili kuhalalisha Mtu akaye miongo miwili au zaidi
Havina ukomo wa kutumukia nafasi ya uongozi wa chama. Tony Blair wa Labour alitumikia kwa zaidi ya miaka 12 ( Charles Attlee alitumikia kwa miaka 20) na Liz Truss wa Conservative kwa siku 50.

Amandla...
 
..kuchanganya kofia ni kosa linalotugharimu pakubwa hapa Tanzania.

..Afrika Kusini wametenganisha kofia na ndio maana chama kinaweza kuwadhibiti Maraisi wao kila wanapokengeuka
Mwenye nguvu Afrika Kusini ni Rais na sio Mwenyekiti wa Chama. Wanaoweza kumdhibiti Rais ni National Working Committee ya Chama sio Mwenyekiti peke yake. Hawana power centres mbili. Hata Marekani Mwenyekiti wa Chama hana nguvu kama Rais. Kwetu sisi ni tofauti. Mamlaka ya Mwenyekiti wa chama ni makubwa mno.

Amandla...
 
Wengi wapo na Lisu moyoni na machoni wapo na mbowe kwa lengo la kula pesa zake anazogawa kama njugu, sasa ni kula pesa za mbowe lakini piga kura kwa Lisu, hii kampeni ni nzuri sana kwani imesaidia mbowe kusambaza pesa ambazo alikuwa akila mwenyewe kifisadi
 
Mbowe ndani ya chama ni Dikiteta mkubwa huwezi kumpinga na hutumia nguvu ya pesa anayoiba kuwadhoofisha wote wanaompimga, hata Lisu angekuwa katia nia mapema ya kuwania uenyekiti asingekuwa mzima leo, watia nia wote Mbowe aliwachakaza mapema
 
Mbowe ni mwizi kama wezi wengine atasalia kuwa mwenyekiti kwa uchakachuaji na wizi wa kura tu kinyume na hapo mbowe ni bye bye, Mbowe huiba pesa za chama Kisha kisitakatisha kwa kujidai alikikopesha chama ni madeni feki ya kuharalisha wizi wake, kuleni pesa za mbowe kwa bidii angalau mzifaidi wengi aje kujutia matendo yake ambayo bila uchaguzi huu yasingejulikana sasa
 



CCM ina uvumilivu mkubwa wa ndani kwa ndani japo wanahujumiana na kushughulikiana kwa kiwango kikubwa sana lakini kinachowapa uvumilivu ni ukomo wa uongozi wa chama na serikali .

Kundi la wazalendo ndani ya CCM linapoona mafisadi wanatamalaki na kiongozi wao wanavumilia kwa sababu miaka kumi iliopita wazalendo wataingia madarakani na kuweka timu yao ,japo kundi la mafisadi hua linatoka kwa shingo upande. Sasa Chadema tatizo ni kuwa kundi la mafisadi limekaa miaka 22 kwenye kiti .

Ni wazi kuwa Wananchi wa kawaida wa wanapenda kuona sura mpya kwenye uongozi lakini mafisadi na viongozi wa wanapenda mtu anayewafaa wao tuu ndio akalie kiti milele.

Mbowe hata akishinda na kuwa mwenyekiti hawezi kamwe kupata heshima aliyokua ameipata . Hakuna Mtu wa kawaida au msomi au mazalendo wa kweli atakayemwalini .Atabaki kuwa chaguo la mafisadi . Mafisadi Watamshangilia sana lakini Chadema hata pakiwa na uchaguzi wa uwazi na wa haki hawezi kupata kura zaidi ya milioni moja.
 
Hoja za kuzungumuzwa zilowekwa mezani kama sikosei zilikuwa hoja kumi na moja baadhi zilifanyiwa kazi immediately mfano kufuta kesi zote za kisaiasa kurejeshwa mikitano ya kisaiasa,kurudishwa kwa Mali za wafanyabiashara zilizokwapuliwa wakati wa utawala wamagu,baadhi ya hoja ambazo hazikufikia muafaka ni pamoja katiba mpya, tume uhuru ya uchaguzi
 
Duh kweli jina lako linaakisi ulivyo minyoo kwenye akili yako
 
Tangu ajiunge huko muda mrefu tu alikuwa kimya! Leo tu ndiyo afunuliwe kusema haya, kweli au ni bendera fuata upepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…