Baada ya Kashfa ya Trump, Ulaya kwa kauli moja wamuambia Zelensky your not Alone you never walk alone alipo wapo ulipo tupo simamia nchi yako

Baada ya Kashfa ya Trump, Ulaya kwa kauli moja wamuambia Zelensky your not Alone you never walk alone alipo wapo ulipo tupo simamia nchi yako

Sasa mkuu hawawezi kuruhusu Urusi ishinde wakati mkapa sasa ina beba maeneo karibia kila siku pamoja na misaada yao yote.
Sasa jiulize pamoja na misaada yao ikuwemo ile ya Marekani bado Urusi alikuwa anasonga mbele je Marekani akikata musaada?
Alafu usije kujidanganya ya kwamba nchi za Ulaya zinaipenda Ukraine bali zimekasirishwa na hatua ya Trump kuwageuka na kutaka kupora utajiri ya Ukraine peke yake na wao kuambulia kapa hilo ndo lina watoa mapovu, lakini Marekani angewashirikisha nao katika huo uporaji unaotakwa kufanywa na Marekani hizi kelele usinge kuwa unazisikia.
Na Ulaya wameshtuka hawana mgao baada ya kutengwa kwenye mazungunzo ya awali kule Saudi Arabia.
Hata hiyo wanayotaka kutoa kwa jina la misaada watakuja kudai. Wameona hawana namna nzuri ya kudai mnofu ulionona bila ya kuongeza misaada.
Ulaya imechoka kiuchumi, angalia chaguzi Kila mara - wananchi wanechafukwa.
 
Usalama wa Ukraine ndio Usalama wa bara lote la Ulaya, hususani Ulaya Magharibi.

Ukraine ikishindwa Vita maana yake ni kwamba Ulaya yote kabisa itakuwa imetekwa na Urusi. Hili litakuwa jambo baya sana tena ni jambo la hatari kubwa sana kupita kiasi kwa maisha ya Watu wote kabisa wa bara la Ulaya.

Kwa hali kama hiyo, ni Bora Watu wa Ulaya waingie katika Vita ya Tatu ya dunia kuliko kuruhusu Urusi ishinde Vita hiyo.

Kwanza kabisa, lengo Kuu mojawapo la kuanzishwa kwa NATO ilikuwa ni kupambana na Udikteta wa Watawala wababe wa Urusi.

Urusi ikishinda Vita hii, bado ataendelea kuteka maeneo mengine zaidi na zaidi hadi Ulaya yote kabisa iwe chini ya Utawala wa Urusi, Putin hataishia kuiteka Ukraine peke yake.
Nikutoe was was yukreini ya urusi
 
Unatakiwa kufahamu kwamba Watawala wengi sana wa Urusi ni kama vile Mashetani, wana Itikadi kali Sana za Ufashiati, kuua Watu kwao hawaoni kuwa ni tatizo. Kama umeshawahi kufika nchini Urusi au hata kuwahi kuishi na jamii za Watu kutoka Urusi nafikiri utakuwa unanielewa vizuri Sana.
Kwa kifupi ni kwamba Wananchi wengi Sana wa nchi hiyo ya Urusi wengi wao hawaridhiki kabisa na hali ya mambo jinsi yalivyo nchini mwao kutokana na kuwepo kwa Mazingira ya Utawala wa Kidikteta uliojikita mizizi katika nyanja zote kabisa za maisha ya Watu katika nchi hiyo. Hakuna kabisa Mazingira huru na ya Kidemokrasia, Wananchi wengi Sana wa Nchi hiyo wenye Vipato vya kutosha wamekuwa wakihama na kwenda kuishi katika nchi zingine, hususani kwenda katika nchi za Ulaya Magharibi.
Rejea kisa Cha Rais wa nchi hiyo ya Urusi ya zamani (USSR) Mikhail Gorbachev kufanya Uamuzi mgumu Sana wa kuisambaratisha nchi hiyo ya USSR ili kuwapunguzia Watu/Wananchi wengi zaidi kutoka kwenye janga kubwa sana la mateso kutoka kwa Utawala dhalimu chini ya KGB.
Nadhani utakuwa umekosea ulipo andika urusi unatakiwa uandike USA maana sifa zote ulizoandika zimeendana usa na sio urusi
 
Yani wewe unajua kuliko Trump yani wewe wa kumuonya trump Huna hata ujembe wa nyumba kumi kumi
Hapo mkuu sijajifanya najua kuliko Trump, sema watanzania wengi hatuwezi kureson na kutoa maoni yetu wapi nimekosea mkuu?
 
Hata wakati Marekani na ulaya wanaivamia Iraki mlitoa kauli kama hizi mpaka leo Bush Jr na wenzie wanadunda tu. Kauli hizi huwa hazina maana yoyote zaidi ni kuchukua hatua
Tofautisha uvamisi wa US kwa Iraq kumbuka US alimvamia Iraq ili kulinda masilahi yake na washirika wake. Sasa wewe unahisi Russia akiichukua Ukraine US atakuwa salama?
 
Lakin kama ukrain iilkuwa moja ya constituent za ussr hapo urusi ana haki kwa % flan. Ila huyo trumpet kamfanyia umafia zele asee.
 
Falitilia mkataba wa BUDAPEST KAMA UNATAKA KUJUA UNGESE WA PUTIN

Zelensky kwa namna Ukraine ilivyokuwa nzuri, viwanda vizuri, wananchi wasomi na wanaojituma alafu akaingiza nchi vitani dhidi ya Urusi ambayo mataifa zaidi ya 30 yenye viwanda vizito vya kijeshi yameungana kuikabili miongo mingi na bado inabaki imara huoni Zelensky anapaswa kunyongwa sio tu kudharauliwa?
Alichofanya zelensky ni kuitoa sadaka nchi na wananchi wake sababu.
Inajulikana hata waliomshauri aichokoze Urusi wenyewe wanaiogopa ndio maana waliitumia Ukraine wakijua asili ya waUkraine ni Urusi, hivyo Urusi ingetetereka kwa kupambana na ndugu yake..

Jitahidini msome kwa kuelewa sio kwa kushabikia.
Una point makini
 
Februari 28, 2025 Wakuu wa Umoja wa Ulaya wanamwambia Zelensky kwamba "hauko peke yako" baada ya kukashifiwa na Trump katika Ikulu ya White House

Wakuu wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Antonio Costa wanamhakikishia kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky uungwaji mkono usioyumba wa Ulaya baada ya mzozo wake wa ajabu na kiongozi wa Marekani Donald Trump, wakimwambia: "Kamwe hauko peke yako." "Iweni hodari, kuwa jasiri, msiwe na woga," wameandika tume ya Ulaya na marais wa baraza katika taarifa ya pamoja kwenye mitandao ya kijamii, wakimwambia Zelensky: "Tutaendelea kufanya kazi nanyi kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu."

you’ll never walk alone.”
February 28, 2025

EU chiefs tell Zelensky ‘you are never alone’ after he is berated by Trump at White House

EU chiefs Ursula von der Leyen and Antonio Costa assure Ukrainian leader Volodymyr Zelensky of Europe’s unwavering support after his extraordinary clash with US leader Donald Trump, telling him: “You are never alone.”

“Be strong, be brave, be fearless,” write the European commission and council presidents in a joint statement on social media, telling Zelensky: “We will continue working with you for a just and lasting peace.”
Easier said than done, bila US they can't manage Russia. Militarily Russia is by far stronger than the whole of Europe combined, na kwa sasa Ukraine watapelekewa moto yaani nao inawabidi wajipange kitofauti.
 
Wewe kutoka Igunga unajua mifumo ya dunia lakini Trump Rais wa dunia haijui Hongera.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Eti mlugaluga huyo anaijua dunia zaidi ya Trump mtu ambaye alishakuwa rais wa Marekani yaani literally ameshawahi kuiongoza dunia kwa miaka minne na ana-control Oval office ambayo inaiburuza dunia plus advisers waliomzunguka na wanaomjulisha kila yale ya muhimu yanayoendelea around the globe. That shit is crazy frfr.
 
Hivi Ukraine aliichokoza vipi Urusi?
Kwa kivunja makubaliano kwamba hakutakuwa na expansion ya NATO at Russia's doorstep. Ila sababu ambayo Russia haiisemi sana ni ile ya mistreatment ya ethnic Russians(Russian speaking Ukrainians) iliyokuwa ikifanywa na utawala wa Zelenskyy mpaka kupelekea wao kupiga kura ya kutaka kujitenga kujiunga na Russia.
 
Unatakiwa kufahamu kwamba Watawala wengi sana wa Urusi ni kama vile Mashetani, wana Itikadi kali Sana za Ufashiati, kuua Watu kwao hawaoni kuwa ni tatizo. Kama umeshawahi kufika nchini Urusi au hata kuwahi kuishi na jamii za Watu kutoka Urusi nafikiri utakuwa unanielewa vizuri Sana.
Kwa kifupi ni kwamba Wananchi wengi Sana wa nchi hiyo ya Urusi wengi wao hawaridhiki kabisa na hali ya mambo jinsi yalivyo nchini mwao kutokana na kuwepo kwa Mazingira ya Utawala wa Kidikteta uliojikita mizizi katika nyanja zote kabisa za maisha ya Watu katika nchi hiyo. Hakuna kabisa Mazingira huru na ya Kidemokrasia, Wananchi wengi Sana wa Nchi hiyo wenye Vipato vya kutosha wamekuwa wakihama na kwenda kuishi katika nchi zingine, hususani kwenda katika nchi za Ulaya Magharibi.
Rejea kisa Cha Rais wa nchi hiyo ya Urusi ya zamani (USSR) Mikhail Gorbachev kufanya Uamuzi mgumu Sana wa kuisambaratisha nchi hiyo ya USSR ili kuwapunguzia Watu/Wananchi wengi zaidi kutoka kwenye janga kubwa sana la mateso kutoka kwa Utawala dhalimu chini ya KGB.
Acha propaganda za kitoto.
 
Zelensky ameishashindwa vita na Nchi imeshamegwa hao EU ni maboya waliomlaghai Zelensky na magobole ya misaada aibu inawakumba🤣🤣 lazima wajitoe kimasomaso sasa hivi Hangary anawacheka tu hao EU kwa kuangukia pua
Dogo lini imetangazwa vita imeisha na Ukraine imeshindwa?
 
Falitilia mkataba wa BUDAPEST KAMA UNATAKA KUJUA UNGESE WA PUTIN

Huo mkataba ulikuwa na masharti yapi?
 
Back
Top Bottom