Mtoa mada umesahau kusema Mbeya walichokufanyia. Ninawasiwasi mtoa mada umeoa Mbeya kama hujaoa Mbeya basi kuna ndugu yako kaoa Mbeya na amebanwa haswa.
Binafsi nakupenda Mbeya kwasababu zifuatazo.
1. Mbeya kuna hali ya hewa nzuri ambayo hata mgeni kutoka ulaya lazima aipende.
2. Mbeya kuna vyakula vingi vitamu na vya kila aina na vya bei ndogo.
3. Mbeya kuna mazingira mazuri ya kusomea
4. Mbeya unakunywa maji ya kisima[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]Mbeya unafulia maji ya kisima.
5. Mbeya ukiagiza chakula hotelini maji ya kunywa unamiminiwa kutoka kwenye majagi maalumu. Na hayo maji yanachotwa kwenye ndoo tu.
Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.
Hii ndio imenipa akili ya kuanza mkakati wa kufungua kiwanda cha Kuchukua maji ya bahari ya Hindi na kuondoa chumvi, ili kupata maji safi na salama. Lakini pia kuna vimashine nitawauzia wakazi wa Dar es salaam waliochimba visima vyenye maji ya chumvi, vitakua vinatumia solar kutoa chumvi kwenye maji ya kisima. Sasa wakazi wataweza kupata maji ya kunywa, kufulia na kuoga majumbani mwao.