Baada ya Kauli ya Rais Samia, Waliomtukana Dkt. Bashiru wamuombe radhi

Wana-CCM kindakindaki na machawa ambao mlijikita katika kumshambulia Dkt. Bashiru kwa kauli yake kwa Taasisi ya Wakulima juu kumsifia sifia Rais badala ya kutimiza malengo yao ya kutetea wakulima wamepigwa stop.

Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.

Hii maana yake aliyosema Bashiru yalikuwa sahihi.

Je, hii aibu wanaibebaje hao wanafiki? Yuko wapi Lusinde au Msukuma waliomshambulia Bashiru? Yuko wapi Amos Makalla na wengine? AIBU KUBWA na walipaswa kusimama na kumuomba radhi Dkt. Bashiru.
Mtu pekee angeweza kumsaidia huyu Mama ni Bashiru tu
 
Hi hotuba naiomba jamani.Maana mtu unasifiwa mpaka unajishangaa.
 
Wana-CCM kindakindaki na machawa ambao mlijikita katika kumshambulia Dkt. Bashiru kwa kauli yake kwa Taasisi ya Wakulima juu kumsifia sifia Rais badala ya kutimiza malengo yao ya kutetea wakulima wamepigwa stop.

Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.

Hii maana yake aliyosema Bashiru yalikuwa sahihi.

Je, hii aibu wanaibebaje hao wanafiki? Yuko wapi Lusinde au Msukuma waliomshambulia Bashiru? Yuko wapi Amos Makalla na wengine? AIBU KUBWA na walipaswa kusimama na kumuomba radhi Dkt. Bashiru.
Yuko wapi Kigwa mzee wa kutoa kafara wanawe ili awe waziri.
 
Kumezuka kundi la watu kazi yao kubwa ni kumsifia Rais Samia hata pasipostahili, kundi hili kwa lugha sahihi ni machawa. Machawa hawa wapo kwa ajili ya kuishi kwa ujanja ujanja wa kumsifia Rais hata pasipostahili mpaka inakuwa kero kwa mhusika.

Kauli mbiu yao ni “Mama anaupiga mwingi." Juzi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa UWT taifa Rais Samia kachukizwa na sifa hizo hivyo, kwa taarifa yenu mama hataki!

Watanzania tunatakiwa kumpongeza Rais na siyo kumsifu siku zote, sifa na utukufu hupewa Mungu na siyo binadamu. Machawa wamekuwa wanampa sifa Rais za kinafiki na ndiyo maana Mama hataki sifa zenu.

Hongera sana Rais Samia kwa kuchukizwa na sifa za kinafiki, kumbuka hao hao wanaojifanya kukusifu ndiyo hao hao kesho watakusema vibaya, machawa ni wanafiki sana.

cloudsfmtz_1669702635970964.jpg
 
Kiongozi yeyote anayeona Mbali Mapambio lazima yamkere wakati anaona bado tuna changamoto kwenye mambo mengi sana kumaliza nchini.

Ajira,Elimu, mzunguko wa Pesa na changamoto nyingine!

Britanicca
 
Wana-CCM kindakindaki na machawa ambao mlijikita katika kumshambulia Dkt. Bashiru kwa kauli yake kwa Taasisi ya Wakulima juu kumsifia sifia Rais badala ya kutimiza malengo yao ya kutetea wakulima wamepigwa stop.

Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.

Hii maana yake aliyosema Bashiru yalikuwa sahihi.

Je, hii aibu wanaibebaje hao wanafiki? Yuko wapi Lusinde au Msukuma waliomshambulia Bashiru? Yuko wapi Amos Makalla na wengine? AIBU KUBWA na walipaswa kusimama na kumuomba radhi Dkt. Bashiru.
Aisee...Bora amewambia ukweli....Maana utakuta Waziri amesimama anasema Mama ametupa pesa sijui bilioni ngapi kwa ajili ya mradi gani sijui......Sasa hapo huwa nashangaa; hizo ni pesa za Mama au ni pesa za serikali ambazo ni zetu wote?? Maana wote tumelipa kodi; na hata kama ni mkopo, basi tutalipa Wa-Tanzania wote. Angalau basi wangesema serikali chini ya usimamizi wa Mama imetoa pesa kiasi fulani.....hiyo ingekuwa sawa.
 
Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.
Tuliwaambia kimya cha huyo mama juu ya sifa wanazomrushia kina mshindo mkuu wakatushambulia weeee mpaka basi sasa bora amewaambia
 
Na Mh Rais asiishie kupinga hizi sifa za geresha za kumvisha kilemba cha ukoka ajiulize yale mabango ya wakulima ni kweli ni utashi wao au ni ya wanasiasa walio wawezesha ili kuficha mapungufu ya kiutendaji katika ugawaji wa mbolea. Je ni kweli mbolea inawafikia wakulima kwa uhakika au mabango na sifa vinatumika kumficha Mh Rais mapungufu yaliyoko katika utendaji.
Nakwambia kesho akatokea kiongozi mwingine aina ya bashiru akazungumza na wafanyakazi! Kuwakumbusha kuwa TUCTA sio chama cha kumtetea mwajiri Bali kudai maslahi Bora ya wafanyakazi utaona Kila Aina ya panya watakavuojitokeza na hii huwa inafanywa na vijana wa uvccm ambao hawapo hata katika kada husika!
Mark my words
 
Tuliwaambia kimya cha huyo mama juu ya sifa wanazomrushia kina mshindo mkuu wakatushambulia weeee mpaka basi sasa bora amewaambia
Tatizo lao hawana kumbukumbu mama alishawaonya Sana kuhusu kuacha uchawa tatizo ni mazuzu yasiyojielewa na ndio mana vichwa vyao havitunzi kumbukumbu hili nalo watasahau
 
Nakwambia kesho akatokea kiongozi mwingine aina ya bashiru akazungumza na wafanyakazi! Kuwakumbusha kuwa TUCTA sio chama cha kumtetea mwajiri Bali kudai maslahi Bora ya wafanyakazi utaona Kila Aina ya panya watakavuojitokeza na hii huwa inafanywa na vijana wa uvccm ambao hawapo hata katika kada husika!
Mark my words
Aliwahi kuwaambia KM wao juu ya madhara ya tabia hiyo
IMG-20221122-WA0007.jpg

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ila kwa ucha Mungu wa mama Samia sometimes nafikiri hapendezwi na sifa ambazo zinaweza kumchonganisha na Mungu! Hata JPM kilikuwa kilema na mbegu mbaya kwake!

Mwl Nyerere alisifiwa mno binafsi sababu serikali ilikuwa changa sana na hapo lazima kujenga umoja kupitia kiongozi wenu kama dira. Sasa zama zetu hizi bado tunaishi na upepo ule ule? Tunapaswa kujengwa kulipenda Taifa sio mtu!
 
Back
Top Bottom