Kumezuka kundi la watu kazi yao kubwa ni kumsifia Rais Samia hata pasipostahili, kundi hili kwa lugha sahihi ni machawa. Machawa hawa wapo kwa ajili ya kuishi kwa ujanja ujanja wa kumsifia Rais hata pasipostahili mpaka inakuwa kero kwa mhusika.
Kauli mbiu yao ni “Mama anaupiga mwingi." Juzi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa UWT taifa Rais Samia kachukizwa na sifa hizo hivyo, kwa taarifa yenu mama hataki!
Watanzania tunatakiwa kumpongeza Rais na siyo kumsifu siku zote, sifa na utukufu hupewa Mungu na siyo binadamu. Machawa wamekuwa wanampa sifa Rais za kinafiki na ndiyo maana Mama hataki sifa zenu.
Hongera sana Rais Samia kwa kuchukizwa na sifa za kinafiki, kumbuka hao hao wanaojifanya kukusifu ndiyo hao hao kesho watakusema vibaya, machawa ni wanafiki sana.
View attachment 2430489