Baada ya Kauli ya Rais Samia, Waliomtukana Dkt. Bashiru wamuombe radhi

Baada ya Kauli ya Rais Samia, Waliomtukana Dkt. Bashiru wamuombe radhi

kama mama kasema hivyo, basi kweli anaupiga mwingi..anazidi kukua kisiasa kwa kasi ya 5G.
 
Na Mh Rais asiishie kupinga hizi sifa za geresha za kumvisha kilemba cha ukoka ajiulize yale mabango ya wakulima ni kweli ni utashi wao au ni ya wanasiasa walio wawezesha ili kuficha mapungufu ya kiutendaji katika ugawaji wa mbolea. Je ni kweli mbolea inawafikia wakulima kwa uhakika au mabango na sifa vinatumika kumficha Mh Rais mapungufu yaliyoko katika utendaji.
Well Said
 
Ila kwa ucha Mungu wa mama Samia sometimes nafikiri hapendezwi na sifa ambazo zinaweza kumchonganisha na Mungu! Hata JPM kilikuwa kilema na mbengu mbaya kwake!

Mwl Nyerere alisifiwa mno binafsi sababu serikali ilikuwa changa sana na hapo lazima kujenga umoja kupitia kiongozi wenu kama dira. Sasa zama zetu hizi bado tunaishi na upepo ule ule? Tunapaswa kujengwa kulipenda Taifa sio mtu!
Umenena vyema !
 
Kashtuka na kagundua Bashiru si wa kisport sport, yahitaji umakini kumwendea Bashiru. Japo najua kaisema kinafiki naamini moyoni kakwazika sana na Bashiru, yafaa Bashiru akae chonjo
Wanasemaga wasiwasi ni Akili !! Kukaa chonjo ni muhimu. !!
 
Wao wangekuwa wanasifia sisi wananchi kwa kulipa kodi vizuri ili mambo ya serikali yaende vizuri.
Wakumbuke pia kwamba wananchi wasipolipa kodi vizuri, Serikali inakosa pesa kwenye hazina yake.
 
Wana-CCM kindakindaki na machawa ambao mlijikita katika kumshambulia Dkt. Bashiru kwa kauli yake kwa Taasisi ya Wakulima juu kumsifia sifia Rais badala ya kutimiza malengo yao ya kutetea wakulima wamepigwa stop.

Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.

Hii maana yake aliyosema Bashiru yalikuwa sahihi.

Je, hii aibu wanaibebaje hao wanafiki? Yuko wapi Lusinde au Msukuma waliomshambulia Bashiru? Yuko wapi Amos Makalla na wengine? AIBU KUBWA na walipaswa kusimama na kumuomba radhi Dkt. Bashiru.
Shida ilianzia kwa jpm ambaye alianzisha mpaka kipindi TBC Cha eti kishindo Cha jpm. Yule baba alikuwa anapenda masifa Sana yasiyomstahili kabisa na mwasisi wake alikuwa Dr Bashiru.
 
Wakuu wa mikoa wangejiunga jf wangejifunza mengi na wangekwenda na wakati. Wengi wako na mawazo ya awamu ya tano ya kusifu na kibudu.
 
Shida ilianzia kwa jpm ambaye alianzisha mpaka kipindi TBC Cha eti kishindo Cha jpm. Yule baba alikuwa anapenda masifa Sana yasiyomstahili kabisa na mwasisi wake alikuwa Dr Bashiru.
Kama mtangulizi wako alikosea sana haina maana na wewe ni halali kipitia njia zile zile !
 
Wana-CCM kindakindaki na machawa ambao mlijikita katika kumshambulia Dkt. Bashiru kwa kauli yake kwa Taasisi ya Wakulima juu kumsifia sifia Rais badala ya kutimiza malengo yao ya kutetea wakulima wamepigwa stop.

Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.

Hii maana yake aliyosema Bashiru yalikuwa sahihi.

Je, hii aibu wanaibebaje hao wanafiki? Yuko wapi Lusinde au Msukuma waliomshambulia Bashiru? Yuko wapi Amos Makalla na wengine? AIBU KUBWA na walipaswa kusimama na kumuomba radhi Dkt. Bashiru.
Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.[emoji23]
 
Nakwambia kesho akatokea kiongozi mwingine aina ya bashiru akazungumza na wafanyakazi! Kuwakumbusha kuwa TUCTA sio chama cha kumtetea mwajiri Bali kudai maslahi Bora ya wafanyakazi utaona Kila Aina ya panya watakavuojitokeza na hii huwa inafanywa na vijana wa uvccm ambao hawapo hata katika kada husika!
Mark my words

Umeongea ukwell hapa. Hii tabia ya kuwapa watu uongozi kwa ajili wanajua kusifu au kuwanyamazisha wasitoe hoja kinzani kwa serikali au kiongozi haina faida kwa Taifa.

Itafutwe namna nyengine ya uwezo wa muhusika kafanya nini na kukifanikisha katika majukumu aliyopewa huko nyuma. Hii itaondoa kwa sehemu kubwa tabia hizi za unafiki wa kujipendekeza kwa ajili eti kufikiriwa kupata cheo. Mh Rais kaonesha ujasiri kuwapa ukweli wao. Na huu ukweli utamuweka huru kweli kweli kwa kuwa atajipunguzia mzigo wa kuwabeba wakujipendekeza wasio na uwezo.
 
Back
Top Bottom