Baada ya Kauli ya Rais Samia, Waliomtukana Dkt. Bashiru wamuombe radhi

Baada ya Kauli ya Rais Samia, Waliomtukana Dkt. Bashiru wamuombe radhi

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Wana-CCM kindakindaki na machawa ambao mlijikita katika kumshambulia Dkt. Bashiru kwa kauli yake kwa Taasisi ya Wakulima juu kumsifia sifia Rais badala ya kutimiza malengo yao ya kutetea wakulima wamepigwa stop.

Akizungumza katika kufungua mkutano wa UWT Rais aliwaonya na kukataa mabango ya "TUNAKWENDA NA SAMIA" au "SAMIA ANAUPIGA MWINGI" na kusema sifa ni za Serikali sio mtu na waache mara moja.

Hii maana yake aliyosema Bashiru yalikuwa sahihi.

Je, hii aibu wanaibebaje hao wanafiki? Yuko wapi Lusinde au Msukuma waliomshambulia Bashiru? Yuko wapi Amos Makalla na wengine? AIBU KUBWA na walipaswa kusimama na kumuomba radhi Dkt. Bashiru.
 
Na Mh Rais asiishie kupinga hizi sifa za geresha za kumvisha kilemba cha ukoka ajiulize yale mabango ya wakulima ni kweli ni utashi wao au ni ya wanasiasa walio wawezesha ili kuficha mapungufu ya kiutendaji katika ugawaji wa mbolea.

Je ni kweli mbolea inawafikia wakulima kwa uhakika au mabango na sifa vinatumika kumficha Mh Rais mapungufu yaliyoko katika utendaji.
 
Kuisifia serikali ni bora zaidi kwa mustakabali wa chama chai kuliko kumsifia mtu mmoja kua anaupiga mwingi.

Mwisho wa siku huku chini kunakua hamna uwajibikaji kabisa, ukimsifia mkuu anakulinda.

Kama mama kaamua hivyo ni vyema sana, keshaona wanafki wengi mno na wanamzunguka sana kwa sifa za kijinga.
 
Back
Top Bottom