Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Sijui ndio nimechanganyikiwa na hiki kifo cha ghafla cha Jembe letu,mpendwa wetu, kiongozi na mshauri wetu mkuu wa mambo ya Duniani,kuzimu & mbinguni.

Nimejikuta nawaza tu huenda nafasi ya makamu wa rais atapatiwa bwana Steven Wassirra akibebwa na uzoefu wake wa toka enzi za Nyerere
 
Sijui ndio nimechanganyikiwa na hiki kifo cha ghafla cha Jembe letu,mpendwa wetu, kiongozi na mshauri wetu mkuu wa mambo ya Duniani,kuzimu & mbinguni

Nimejikuta nawaza tu huenda nafasi ya makamu wa rais atapatiwa bwana Steven Wassirra akibebwa na uzoefu wake wa toka enzi za Nyerere
Utakuwa umepigwa kipapai wewe siyo bure.
 
Napendekeza Makamu wa Raisi awe January Makamba.
Hana makundi, ni mstaarabu, hana Jazba.
Mi nampendekeza huyo.
 
Kwani wakati ule wa teuzi za mawaziri,maRC MaDc etc ulipokuwa unapendelea upande mmoja si mlisema tuangalie uchapa kazi na sio DINI? Sasa leo nini tena,atakaeteuliwa yoyote atafaa cha msingi anauwezo wa kufanya kazi ipasavyo
Yangu enzi za nyerenyere aliweka usawa Kati ya dini hizi mbili. Kwa nafasi ya makamo na Rais. Huko kwenye dc na rc ni juhudi yako mwenyewe ya kujipendekeza
 
Wewe sio mtoa roho za watu! Kwani ni lazima Makamu wa Raisi awe mwanaume! Mhe. Samia ana uwezo wa kumpendekeza Makamu wa Raisi mwanamke na kwangu huu utakuwa uamuzi sahihi sana. Nchi hii ina wanawake shupavu na wenye mawazo ya kitaifa zaidi kuliko vyama vyetu. Tuna akina:

1. Asha-Rose Migiro
2. Anna Makinda
3. Prof. Bernadeta Killian
4. Anna Mghwira

Hawa ni baadhi ya wanawake wazalendo wanaoweza kutumikia nafasi ya Makamu wa Raisi wa JMT.
Natamani Rais awe na mawazo yako,sitamani Rais ambae watu wanaweza otea/kisia/bashiri Maamuzi yake

yani natamani kila aliewazwa asiwe huyo Rais aje na mtu wake anaemuamini yeye na ikibidi hata iwe kama ulivyo shauri.
 
January makamba is the best
Really?
Pale anapaswa kuwepo Mkristo, haiwezekani

-Rais Muislam
-Makamu wa Rais Muislam
-Waziri Mkuu Muislam
-Rais wa Zanzibar Muislam
-Makamu wa Rais Zanzibar Muislam
-Katibu Mkuu kiongozi bara Muislam
-Katibu Mkuu kiongozi zanzibar Muislam
-Mawaziri wote Zanzibar Waislam

Its better awe fair.
Huo ndiyo naita ujinga. Uongozi siyo dini. Anayefaa ni yule ambaye anaiweza hiyo kazi kuliko mwingine yoyote. Wapi uliona CV ya kazi ikiwa na dini kama sifa mojawapo? Kama dini ni sifa ya hiyo kazi, kwa nini wewe usiombe uteuliwa kwa vile ni mkristo!
 
Back
Top Bottom