Hebu turudi kuleee enzi za kusoma hasi na chanya.
Hasi+hasi=?
Chanya+chanya=?
Hasi-chanya?=?
Sasa ipo hivi piga ua garagaza makamo wa raisi ni lazima atofautiane na raisi katika vigezo vifuatavyo.
1.Jinsi/jinsia
Hapo lazima awe wa kiume
2. Dini
Hapo lazima atofautiane Na samia. Ikiwa samia anaingia msikitini basi lazima makamu wake awe mtu wa kuingia kanisani na kinyumechake ndio ukweli wenyewe.
Sasa nimepitia mijadala mbalimbali naona ya kwamba January makamba anatajwa kushika nafasi hiyo hilo naomba asahau.
Kuna mtu anaitwa bashiru huyo nae asahau, vigezo hapo juu vinamtupilia mbali.
Majaliwa nae vilevile hata baada ya baraza kuvunjwa(ikitokea sio waziri mkuu) naye hawezi kuwa makamu.
Utaniuliza nimepekua katiba gani kuja na maelezo haya nami nitakujibu hakuna katiba niliyopekua na pengine hayo hayamo, ila uongozi wa kitanzania tangu anzi na enzi umeangukia ktk vigezo hapo juu.
Usiku mwema poleni niliowakera.
Nipo tayari kuja kuomba radhi endapo moja ya majina hapo juu yakipitishwa.