Angalia hii move kwa makini ndio utajua kwanini Magufuli aliwarudisha Lowassa na Rostam walioondoka CCM wakati wa utawala wa JK.

Hii issue kama ikitokea inaweza kuwa planned long time ago, siasa ni kama mathematics.
Na ndo maana Rostam amewezeshwa kufungua kiwanda cha ngozi Morogoro kwa kuleta wawekezaji.

He is the kingmaker.

Ila bado matokeo halisi yaweza kuwa tunapotezwa lengo.

Lakini Mafisadi hawana nafasi katika CCM mpya.
 
Na Nani aliyemwambia? Kwani walijua hili la kifo litatokea?
Uwe mwelewa.

Nikisema aliambiwa atulie namaanisha kwamba Nchimbi alionekana potential kwa baadae.

Ndo maana akaambiwa tutakuweka Mexico kwa muda.

Nchimbi alikuwa ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM hivyo anafaa kuwa kiunganishi.

Hayo ni maoni yangu.
 
Team Lowassa. Team Mafisi. Plus JK without Mkapa.

We are doomed!
 
Timu ya Bashe ndo ina maagizo maalum na nini cha kufanya.

Inaonekana hayo maagizo walipewa hali ilipozidi kuwa mbaya.

Pia baraza la USALAMA na Kitengo wapo kwa uangalizi zaidi.

Nilisema humu kwamba Mzee Malecela alitoa onyo mapema jana asubuhi.

Truth differs Reality!

Tunawaangalia......
 
Mwenyezi Mungu kwa nini umetuchukulia JPM? Tunakuomba sana utuleteee JPM mwingine siyo hawa wa "System." Msaidiea sana Mama Suluh Hassan aweze kusimama kwa nguvu kuhakikisha kuwa anateuliwa Makamu wa rais anayeendana na philosophy ya serikali aliyorithi.
 
Na Nani aliyemwambia? Kwani walijua hili la kifo litatokea?
ALIYEKUWA Mtabiri maarufu Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein aliitisha mkutano wa wahariri na waandishi wa habari mwaka 2006 na kuzungumzia utawala wa Rais Jakaya Kikwete ukiwa na umri wa mwaka mmoja tu.

Baada ya kuzungumza hayo nilipata nafasi ya kumuuliza. Je Tanzania baada ya Kikwete inaweza kupata rais mwanamke?

Shehe Yahya alinijibu:

“Baada ya vipindi viwili vya Rais Kikwete atakuja rais ambaye ni mweusi mchapa kazi lakini mchekeshaji sana, hata hivyo atatawaka kwa kipindi kifupi tu hapo ndipo Tanzania itapata rais mwanamke.”

Wahariri na waandishi waliguna kuonesha kutokubaliana naye wakiwemo wahariri wakongwe Hemedi Kimwaga, Yasini Sadiki, Magnus Mahenge na wengine ambao siwezi kuwakumbuka.

Shehe Yahya baada ya kuona tunambishia alichukua ubao kama ule wa darasani na mkononi alishika kutabu kilichoandikwa Astrology: Monthly numerology, akaanza kufanya hesabu kwa fomula anazojua yeye na akatuambia kwamba kwa Jakaya inaonesha atamaliza muda wake wa miaka kumi na lakini ajaye ataongoza kwa kipindi kifupi.

Tulimuuliza ataongoza kwa muda mfupi kwa sababu gani, alisema hayo mengine yeye hawezi kujua lakini akasisitiza kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa. Tulitawanyika pale kila mmoja akiwa anaona kama amepigwa ‘changa la macho’.

Lakini sasa nimeng’amua kwamba kumbe alikuwa akimtabiria mama Samia bila yeye mama kujua tulichokuwa tunafanya.

HAKIKA SHEHE YAHYA ALIKUWA MNAJIMU WA KWELI.

Kumbuka haya yanatokea baada ya miaka 15 ya utabiri wake na mtabiri akiwa katangulia mbele za haki. Sheh Yahya alifariki mwaka 2011. Mungu ampe raha ya milele na amnusuru na adhabu ya kaburini.

MHARIRI WA GAZETI LA UWAZI, ELVAN STAMBULI
 
Na ndo maana Rostam amewezeshwa kufungua kiwanda cha ngozi Morogoro kwa kuleta wawekezaji.

He is the kingmaker.

Ila bado matokeo halisi yaweza kuwa tunapotezwa lengo.

Lakini Mafisadi hawana nafasi katika CCM mpya.
Huyo Mama naskia anatishwa atapigiwa kura ya kutokuwa na imani nae wabunge wengi waliwekwa na Magufuli, she is scared.

Let's wait & see.
 
Huyo Mama naskia anatishwa atapigiwa kura ya kutokuwa na imani nae wabunge wengi waliwekwa na Magufuli, she is scared.

Let's wait & see.
Hakuna mbunge wa kumtisha mama wa taifa.Kwanza wabunge gani wana jeuri hiyo hawa waliopata kura nyingi kuliko idadi ya wapiga kura !.
 
Heshima sana wanajamvi,

Dalili zote zinaonyesha Emanuel Nchimbi ana nafasi kubwa ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Makamu wa Rais.

Ni hayo tu kwa leo
Hiyo itaturudishia lile jinamizi la Lowassa wa 2015.
Unakumbuka mtiti wa Nchimbi, Adam Kimbisa na Sophia Simba siku Lowassa alipoenguliwa kugombea urais?
 
Jana bashe alionekana amevaa barakoa kuhakikisha anajikinga ipasavyo.

He is a very smart young man upstairs na mzee alimpenda kwa hilo.

Chief, Bashe and Smartness don’t and will never rhyme!

Kuvaa barakoa jana, his smartness + Mzee alimpenda sana??!? Sijaelewa hapa!
 

Are you for real Chief?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…