Simuoni Mwenye hadhi ya kuwa makamu wa Rais ndani ya CCM hii. Ni aibu kwa CCM inayojidai kuwa ni chama kikubwa lakini hata mmoja wa kushika nafasi ya Makamu wa Rais anakosekana.

Basi tuwasaidie, mpeni Lukuvi au Nchimbi. Achaneni na watukutu na wasio na msimamo kama Kabudi, Mwigulu, Kitila, N.k. Pia hakuna haja ya kuangalia sana udini, mpeni tu hata January Makamba.
 
Kwa vile kule Visiwani CCM wanakolabo na ACT basi apewe Zitto.
 
Najaribu utabiri wangu kuwa makamu wa Rais wetu atakuwa huyu hapa. Tangu nimfahamu, sikuwahi kusikia kakosea njia katika kutekeleza majukumu yake. Wala kusikia kinywa chake kikinena yawezayo kuwakwaza Wengine. Maoni yenu? Niambie japo kidogo kuhusu unavyomjua baba huyu. "Natabiri tu."
Mr Lukuvi.


 
Huyu hukumsikia kashifa za udini mkuu?
 
Huyo ana elimu ya darasa la saba tu..hafai.
 
Ni vizuri nafasi hizi za juu zikashikwa na watu wenye umri mkubwa kama Pinda
 
Mnadhani katiba inavunjwaga tu kwa mawazo ya kipuuzi kama haya ya kwako?
 
Safari hii nafasi ya Makamu wa Rais wa nchi yetu Tanzania bila kupepesa macho na kwa kuzingatia uzoefu,weledi na mgawanyo wa madaraka apewe Dr Wilbroad Slaa ambaye kwa sasa ndiye balozi wetu huko Sweden.
 
Imfikie Mstaafu Jakaya Kikwete popote alipo,
Salaam Baba habari ya MSOGA?
Nakuletea salaam nyingi toka kwa Wananzengo, Pole sana kwa Msiba wa Rais MAGUFULI, Hakika hatutasahau kazi na historia yake katika Taifa letu.

Ni wiki sasa Tangu tupate Msiba huu mkubwa kwa Taifa letu, wiki hii pia tunatarajia kumstiri mpendwa wetu Kijijini kwao Chato, Kazi ya Bwana haina Makosa japo bado ni ngumu kuzoea.

Wiki hii pia tumempata Rais Mpya, Mama Samia Suluhu Hassan, yote kheri tunamshukuru Mungu kwa kila jambo.

Wakati tunasubilia kuzika huko chato na maombolezo ya siku 21, yameanza kusikika maneno na hakika minong'ono kuwa WEWE Jakaya Kikwete sasa unajiandaa kurudi Ikulu kwa Mlango wa nyuma kupitia neno maarufu "USHAURI".

Hakuna mtu mwenye mashaka juu ya uwezo wako Baba Kikwete, hakuna mtu asiyejua kuwa wewe ndie tunayekutegemea kumshauri Rais wetu Mama Samia, Lakini chondechonde usimpotoshe akakosea ingali ASUBUHI kabla ya Matanga kuisha.

Mama Samia kwasasa baada ya kuapa na baada ya Mazishi anatakiwa kuitisha Bunge na kupeleka jina la Makamu wa Rais baada ya kushauriana na Chama chake (CCM).
Hapa pia anatakiwa kumchagua Waziri Mkuu Mpya ( japo watu bado wanampigia chapuo Majaliwa aendelee).

Minong'ono inayotanda kuwa wewe Baba Kikwete ndie unaepanga Safu hii na kumshauri Mama Samia atekeleze, Hofu ya wengi ni kuwa unaweza kumpotosha Mama yetu na likawa kosa la kwanza la kuwavunja Moyo Watanzania katika kipindi hiki kigumu cha kuhitaji Matumaini na kutiwa Moyo.

Chondechonde Baba Kikwete usimshauri vibaya Mama Samia afanye makosa Asubuhi maana atamaliza vibaya Jioni.

Yapo mambo hayajaandikwa katika Katiba yetu ya JMT lakini yanatekelezwa kwaajili ya mtangamano wa Taifa letu, Mfano anayetakiwa kuwa Makamu wetu wa Rais kwasasa LAZIMA awe Mkiristo tena anayetoka Tanzania Bara. Katika hili yapo Majina mengi yanatajwa ambayo yanahusishwa na wewe kupenyeza majina hayo kwa Rais Mama Samia kuwa hawa ndio wanaofaa, Mshauri vizuri Rais wetu usimpotoshe na usimuingizie Wana Mtandao watamvurugia uongozi na Itawakatisha Tamaa Watanzania ambao wanayapenda Maendeleo.

Baba Kikwete, Nakukumbusha Mwaka 1985 wakati Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere anaachia Madaraka na kumkabidhi Mzee Mwinyi (anayetoka Zanzibar) Mzee Ruksa alichagua Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mzee Msuya kumsaidia Mambo ya Tanzania Bara, Baadae alimchagua Mzee Warioba kumsaidia mambo ya Tanzania Bara, Baadae alimchagua Mzee Malechela kumsaidia Mambo ya Tanzania Bara na kwa Hakika mambo yalienda vizuri.

Umuhimu wa kumchagua Makamu wa Rais Mtu mzima mwenye uzoefu wa Nchi mwenye msimamo asiyeyumbishwa na anayeweza kumshauri vizuri Rais Samia Suluhu Hassan lazima lipewe kipaumbele na kuzingatiwa, Hapa ndipo penye Hekima kubwa bila mihemko, makundi na mitandao ya wasaka urais 2025 au 2030. Baba Jakaya uwe Makini maana lawama utazibeba wewe na utamfanya Rais ashindwe kumudu kazi yake vyema, mpatie nafasi apendekeze MTU mwenye uzoefu na uwezo wa kufanya kazi mwenye maadili na anayekubalika Tanzania BARA, Mkiristo anaweza kuunganisha viongozi wa dini na anayeza kumsaidia Rais katika Majukumu ya Urais muda wote.

Baba Kikwete najua kwasasa uko katika maombolezo lakini upatapo barua hii tafadhali pokea salaamu hizi na ujue kuwa watu wanajua kuwa ushauri wako unaweza kuwavunja Moyo Watanzania au kuwatia Moyo Watanzania katika kipindi hiki cha msiba mzito tulionao.

Yapo majina yanatajwa kuwa yanaweza kupewa kipaumbele kama Mizengo Pinda, Martine Shigela, Antony Mtaka, Palamagamba Kabudi, Stephen Wasira, Emmanuel Nchimbi na Wiliam Lukuvi. Pamoja na Wazoefu hawa kutajwatajwa lakini tunaomba Mama SAMIA aachwe ama ashauriwe vizuri kupata Makamu wa Rais anayekubalika kwa Watu, Bunge na Jeshi letu.

Baada ya Mchakato wa kuunda serikali kuisha, Umshauri Rais wetu Mama Samia kuweka safu nzuri ya Chama kuanzia Makamu Mkiti Imara, Katibu Mkuu Imara, Mwenezi Imara na Idara za chama zipate viongozi shupavu, Ikumbukwe kuwa Chama Imara huzaa Serikali Imara na Chama legelege huzaa Serikali legelege. Mkiti mpya wa Chama Mama Samia usimpotoshe akaunda safu za Kimtandao Hakika zitawakatisha Tamaa wanachama ambao wana IMANI KUBWA na chama chao.

Wasalaam Baba Kikwete.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Amshauri arejeshe kaulimbiu ya maisha Bora kwa kila mtanzania, inaunganisha watu na kuwapa ari.
Na amshauri neno mabeberu likome kutumika kisiasa.
 

Umenena vema. Wasiraaaaaa💯, amechomwa mikuki mingi na ameivumila. Ila asiwe mwenye kulipa kisasi
 
Uwepo wake Mzee wetu huyu kipindi ni tunu, tunamwamini sana atasaidia
 
Achana na Kikwete wewe NDEZI
Tunajua nia yenubovu kuwa unamvunja nguvu Kikwete kwani automatically ndiye atakayeshikiliavusukunai wa uenyekiti wa muda.
Mipangovyenu yote tunaijua ewe team Bashe
 
Nikurekebishe kidogo

Mzee Mwinyi alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri 1985 alimchagua Mzee Joseph Sinde Warioba kuwa ndio PM wake sio Msuya, Msuya alimchagua 1994 baada ya kuvunja Cabinet iliyokuwa na PM Malecela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…