chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,834
- 26,217
Ni wasira huyuhuyu tunayemfaham ndie mnataka awe Vice President au kuna mwingine?[emoji2]
Umenena vema. Wasiraaaaaa[emoji817], amechomwa mikuki mingi na ameivumila. Ila asiwe mwenye kulipa kisasi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni wasira huyuhuyu tunayemfaham ndie mnataka awe Vice President au kuna mwingine?[emoji2]
Umenena vema. Wasiraaaaaa[emoji817], amechomwa mikuki mingi na ameivumila. Ila asiwe mwenye kulipa kisasi
Heri ya Mangula kuliko mzee huyu aliyeifanya nchi shamba la bibi.Uwepo wake Mzee wetu huyu kipindi ni tunu, tunamwamini sana atasaidia
Na neno Wanyonge. Kunakuwaje na wanyonge ndani ya nchi huru? Wanatambulikaje au sifa zao ni zipii? Wamefikaje hapo?Amshauri arejeshe kaulimbiu ya maisha Bora kwa kila mtanzania, inaunganisha watu na kuwapa ari.
Na amshauri neno mabeberu likome kutumika kisiasa.
Imfikie Mstaafu Jakaya Kikwete popote alipo,
Salaam Baba habari ya MSOGA?
Nakuletea salaam nyingi toka kwa Wananzengo, Pole sana kwa Msiba wa Rais MAGUFULI, Hakika hatutasahau kazi na historia yake katika Taifa letu.
Ni wiki sasa Tangu tupate Msiba huu mkubwa kwa Taifa letu, wiki hii pia tunatarajia kumstiri mpendwa wetu Kijijini kwao Chato, Kazi ya Bwana haina Makosa japo bado ni ngumu kuzoea.
Wiki hii pia tumempata Rais Mpya, Mama Samia Suluhu Hassan, yote kheri tunamshukuru Mungu kwa kila jambo.
Wakati tunasubilia kuzika huko chato na maombolezo ya siku 21, yameanza kusikika maneno na hakika minong'ono kuwa WEWE Jakaya Kikwete sasa unajiandaa kurudi Ikulu kwa Mlango wa nyuma kupitia neno maarufu "USHAURI".
Hakuna mtu mwenye mashaka juu ya uwezo wako Baba Kikwete, hakuna mtu asiyejua kuwa wewe ndie tunayekutegemea kumshauri Rais wetu Mama Samia, Lakini chondechonde usimpotoshe akakosea ingali ASUBUHI kabla ya Matanga kuisha.
Mama Samia kwasasa baada ya kuapa na baada ya Mazishi anatakiwa kuitisha Bunge na kupeleka jina la Makamu wa Rais baada ya kushauriana na Chama chake (CCM).
Hapa pia anatakiwa kumchagua Waziri Mkuu Mpya ( japo watu bado wanampigia chapuo Majaliwa aendelee).
Minong'ono inayotanda kuwa wewe Baba Kikwete ndie unaepanga Safu hii na kumshauri Mama Samia atekeleze, Hofu ya wengi ni kuwa unaweza kumpotosha Mama yetu na likawa kosa la kwanza la kuwavunja Moyo Watanzania katika kipindi hiki kigumu cha kuhitaji Matumaini na kutiwa Moyo.
Chondechonde Baba Kikwete usimshauri vibaya Mama Samia afanye makosa Asubuhi maana atamaliza vibaya Jioni.
Yapo mambo hayajaandikwa katika Katiba yetu ya JMT lakini yanatekelezwa kwaajili ya mtangamano wa Taifa letu, Mfano anayetakiwa kuwa Makamu wetu wa Rais kwasasa LAZIMA awe Mkiristo tena anayetoka Tanzania Bara. Katika hili yapo Majina mengi yanatajwa ambayo yanahusishwa na wewe kupenyeza majina hayo kwa Rais Mama Samia kuwa hawa ndio wanaofaa, Mshauri vizuri Rais wetu usimpotoshe na usimuingizie Wana Mtandao watamvurugia uongozi na Itawakatisha Tamaa Watanzania ambao wanayapenda Maendeleo.
Baba Kikwete, Nakukumbusha Mwaka 1985 wakati Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere anaachia Madaraka na kumkabidhi Mzee Mwinyi (anayetoka Zanzibar) Mzee Ruksa alichagua Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mzee Msuya kumsaidia Mambo ya Tanzania Bara, Baadae alimchagua Mzee Warioba kumsaidia mambo ya Tanzania Bara, Baadae alimchagua Mzee Malechela kumsaidia Mambo ya Tanzania Bara na kwa Hakika mambo yalienda vizuri.
Umuhimu wa kumchagua Makamu wa Rais Mtu mzima mwenye uzoefu wa Nchi mwenye msimamo asiyeyumbishwa na anayeweza kumshauri vizuri Rais Samia Suluhu Hassan lazima lipewe kipaumbele na kuzingatiwa, Hapa ndipo penye Hekima kubwa bila mihemko, makundi na mitandao ya wasaka urais 2025 au 2030. Baba Jakaya uwe Makini maana lawama utazibeba wewe na utamfanya Rais ashindwe kumudu kazi yake vyema, mpatie nafasi apendekeze MTU mwenye uzoefu na uwezo wa kufanya kazi mwenye maadili na anayekubalika Tanzania BARA, Mkiristo anaweza kuunganisha viongozi wa dini na anayeza kumsaidia Rais katika Majukumu ya Urais muda wote.
Baba Kikwete najua kwasasa uko katika maombolezo lakini upatapo barua hii tafadhali pokea salaamu hizi na ujue kuwa watu wanajua kuwa ushauri wako unaweza kuwavunja Moyo Watanzania au kuwatia Moyo Watanzania katika kipindi hiki cha msiba mzito tulionao.
Yapo majina yanatajwa kuwa yanaweza kupewa kipaumbele kama Mizengo Pinda, Martine Shigela, Antony Mtaka, Palamagamba Kabudi, Stephen Wasira, Emmanuel Nchimbi na Wiliam Lukuvi. Pamoja na Wazoefu hawa kutajwatajwa lakini tunaomba Mama SAMIA aachwe ama ashauriwe vizuri kupata Makamu wa Rais anayekubalika kwa Watu, Bunge na Jeshi letu.
Baada ya Mchakato wa kuunda serikali kuisha, Umshauri Rais wetu Mama Samia kuweka safu nzuri ya Chama kuanzia Makamu Mkiti Imara, Katibu Mkuu Imara, Mwenezi Imara na Idara za chama zipate viongozi shupavu, Ikumbukwe kuwa Chama Imara huzaa Serikali Imara na Chama legelege huzaa Serikali legelege. Mkiti mpya wa Chama Mama Samia usimpotoshe akaunda safu za Kimtandao Hakika zitawakatisha Tamaa wanachama ambao wana IMANI KUBWA na chama chao.
Wasalaam Baba Kikwete.
Mungu ibariki Tanzania.
Jombi Tanga ipo kaskazin siyo pwani,ipo pamoja na Kilimanjaro, Arusha,manyaraRais Pwani na makamu wa Rais iwe Pwani tena?
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.
Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndio anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.
Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?
R.I.P Magufuli.
We ni mtu wa ajabu saMnadhani katiba inavunjwaga tu kwa mawazo ya kipuuzi kama haya ya kwako?
Aisee wewe nashindwa nitumie neno gani ,itoshe kusema hoja haijibiwi KWA ma matusi,na kebehi,bali hujibiwa KWA hoja, so niseme unamapungungufu flani japo hujijui, na jilekebishe Mara moja kabla ya kumuomba mungu akufundishe KWA kiwango chake ,Mnadhani katiba inavunjwaga tu kwa mawazo ya kipuuzi kama haya ya kwako?
Mnadhani katiba inavunjwaga tu kwa mawazo ya kipuuzi kama haya ya kwako?
Bado mdogo kuwa VP. VP ni nafasi ya maveteran. Hata wanaosema EJN au Mbrazil kwa jina jipya na wanaosema awe Marope jr sioni kama ni watu wanaojua kutabiri mambo au nafasi za kisiasa.Ndio next VP?