Zoezi la kupitisha jina la nafasi ya Makamu wa Rais limekua gumu sababu ya makundi yaliyoibuka baada ya msiba.

Haitakua rahisi tena kama awali kupata mtu atakaekua Makamu wa Rais.

Wengi wanaamini Makamu wa Rais wa sasa ndiye Rais ajae, na timu yenye nguvu ni hii iliyoshika kijiti kwa sasa.

Kati ya haya Majina mojawapo atakua Makamu na Rais ajae.
~January Makamba
~Nchimbi
~Lukuvi: ingawa huyu anaweza pia kuwa PM Baraza la Mawaziri likivunjwa
 
Natoa mwongozo 1. Kiongizi ambaye hatunzi kauli zake hafai 'a public figure has to keep his words' 2. Asiye na mihemuko ,Mwenye busara ,mwenye uwezo mzuri wa kufikiri.
 
Hakuna aijuaye kesho ,utaishije kwa kutegemea bahati?
 
Mimi naona mazingira ya uongozi wa Rais Samia Suluhu yananishawishi ni heri kamanda mstaafu Jenerali Mwamunyange afikiriwe umakamu wa Rais.Huyu ndiye "roho wa Bwana" ananionyesha sana. Kila nikisali anakuja huyu wa kwanza.

Mwingine ni dokta Wilbroad Peter Slaa. Yaani huyu apewe hata uwaziri mkuu ikishindikana umakamu.

Mwisho ni Philip Marmo, Mzee Mangula, Christopher Chiza, William Lukuvi na Job Ndugai na Anthony Mtaka.

Hivi kule TISS hakuna wazee wetu wastaafu waliobakiabakia?
 
Nianze kujitambulisha hapa kwamba mie ni mwananchi mzalendo tu Sina itikadi ya chama chochote Cha siasa na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote, ingawa umri wangu unakimbikia umri wa kustaafu.

Bila Shaka, hiyo inatuma ujumbe kwamba ,mie ni mtu objective na siyo subjective. Mimi naamini Sana katika mantic ya Mambo na niko more Principled.

Ungeniuliza Mimi, ni nani anafaa kuwa makamu wa Rais kwa merits zake ningekwambia ni Membe.
Ni msomi, statesman ( bila Shaka mnamuita kachero mbobezi), lakini hasa ni mtu muwazi na mzalendo.

Najua kwa sababu ya siasa zilizoghubika CCM mpya, alifukuzwa uanachama. Kwetu wengine tunaosoma Mambo katikati ya msitari, huoni sababu za kufukuzwa zenye mashiko na ukweli, Membe, haishi itikadi ya chama kingine competently zaidi ya CCM.
Utasema ACT, kwani kakaa ACT kwa muda gani? Is almost nothing.

Lakini kubwa hasa Membe aliondolewa CCM kwa kete ya chuki za kisiasa, naweza sema. Hivyo basi, mpaka ninapoandika, by assessment ,Membe is ideologically CCM, period!

Na kwa kuwa ana sifa muhimu za kuongoza kama nilivyoeleza hapo juu. Nawaomba CCM wamrudishie Membe uanachama wake by virtue of reconciliation and stability in the party. lakini waone hasa huyu ni mtu wao na kama wanavyojua, ana sifa zote za kuwa vp.

Kusameheana na maelewano ndo hatua ya juu kabisa ya ustaarabu na ubinadamu wetu. Na kwa sababu ni mtanzania na mzalendo, tutamuogopea nini?

ACT wako serikalini zanzibar na Mambo yanaenda, sembuse Membe ambaye UCCM wake( maana hajawahi toka kwa kutaka bali kwa mizengwe) kumpendekeza makamu? Think about that!

It can be done,let there be political willing and politics of national interests.

CCM mezeni matapishi wala hakuna ubaya maana ni matapishi yenu wenyewe.

Mleteni huyu jamaa Ili amalize maisha yake vizuri akiwa ametumia vipawa vyake vyote kwenye kiwango Cha juu Cha nafasi hiyo. Ni msomi, muitikadi, uelewa wa kimataifa, na bila kusahau ukachero ambayo ni sifa mama inayomueleza mzalendo asiyetiliwa Shaka.
Wasalaam.
 
Amekutuma? Muda wake ulishapita
 

Naunga hoja mkono majaliwa for VP ikiwa hivyo hatutaona sana pengo la JPM. Mawazo yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…