Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Itapendeza ,kufumba macho ,kubadilisha baadhi ya vifungu , makamu atoke vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja kuvunja bunge , namanisha uchaguzi wa wabunge na madiwani urudiwe upya.

Lengo kuleta mshikamano wa kitaifa, hata huwe malaika kuongoza nchi ikiwa imagawanyika ni ngum Sana, wazee ,wastahafu kutoka CCM, hapa simameni imara kwa maslahi mapana ya taifa.
Hii nayo Ni point ya kuongezea Ila sasa shida gharama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mliowataja wote ni wabunge wa majimbo.na huyu mama hawezi kuvunja katiba kama mnavyofikiria wala msimlishe matango pori.Kabudi,Mpango Mwigulu wote ni wabunge wakae pembeni tu
 
Nasikia Wasukuma wanataka hiyo nafasi kwa udi na uvumba. Waziri wa ujenzi ndio chaguo lao ikishindikana basi hata Askofu Rashid au Makonda.
Tunaihitaji kwa udi na uvumba, haiwezekani tuishie njiani awamu yetu.
Kifuatacho 2025 ( Msukuma tena Dr Leonard Chamuriho ).
Basi hata Dr balozi Bashiru Ally Kakulwa tutampa maana tuna elements nae za kanda ya ziwa.
 
Mi nashauri Mh. Samia amtafute makamu wake ambaye ni mchumi mmbobezi ambaye amtamsaidia kuurudisha uchumi kwenye mstari, lakini mtu mwenye ufahamu wa diplomasia vizuri itamsaidia pia kuurudisha mahusiano na nchi marafiki na mwisho mtu walau mwenye uzoefu wa shughuli za serikali.

Possible candidates include former CAG, former Katibu mkuu kiiongozi Sefue,

Proffesor Mkenda, Mizengo Pinda.

Mheshimiwa aepuke kutea makada ambao wanaweka chama mbele na sio taifa
Ili kujenga umoja wa kitaifa Tundu A Lissu atafaa kuwa makamu wa rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kuondokewa na Rais wetu kipenzi. Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina.

Kutokana na hali ilivyo, automatically Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais ndo anakuwa Rais kamili kwa kipindi cha miaka minne iliyobaki.

Je, nani anayefaa kuwa Makamu wa Rais ukizingatia kuwa lazima atoke Bara kwani Mama Samia ametokea Zanzibar?

Mimi binafsi nahisi Mhesphimiwa January Makamba anafaa sana kuchukua hiyo nafasi ukizingatia ameshafanya kazi kwa karibu na Mama Samia kwa muda mrefu kipindi akiwa Waziri.

R.I.P Magufuli.
Paul Makonda,
 
Back
Top Bottom