Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Sidhani kama watapenda kutoa mtu nje ya waliokuwa kwenye mchujo wa 2015.. 'Possibility' kubwa ni January Makamba kama VP.. na pia huenda ushawishi wa JK ukasaidia pia kwani ndiyo mwenye nguvu kwenye Kamati ya Marais Wastaafu..
Jamani JK asije akatuletea tena nanihii..
 
Ingawa katiba haikutaja dini, ila imetaka rais akitoka bara, basi makamu ni visiwani, na kinyume chake ni kweli. Kwa utamaduni wa CCM, hiyo ina maana pia kibarua cha waziri mkuu Majaliwa kimeshaota nyasi, kwakuwa rais atakuwa "mwislamu" basi waziri mkuu atakuwa "mkristo."
 
Mbona uko nyuma sana kimawazo mkuu kwan wanatumia msahaf na bible pale au roho mbaya tuu pale sio uislam pale katiba mkuu ayo mawazo dun
Huyo jamaa nimemshangaa utafikiri wanaenda kutuhubiria dini kitaifa. Sisi tunahitaji viongozi wa kutuongoza wenye maadili mema, busara na hekma wakifuata katiba na sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hayo mambo ya dini zao hazituhusu
 
Kigezo cha kwanza kwenye majina lazima awe mkristo ili kubalance haiwezekani wote wakawa waislamu haya tuanze upya kufikiria
Wakristo Roho zenu ngumu sana.mkae pembeni muangalie namna ya kuongoza nchi na waislam
 
Kwakuwa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inasema kabisa kwamba makamu wa Rais kwanza ni lazima asiwe katika kiti cha ubunge. Lazima awe mtu huru toka chama cha siasa, CCM kina hazina ya viongozi wengi wazuri na waliolelewa katika makuzi ya kiuongozi, hakuna haja ya kwenda kusubiri mtu ajiuzulu ubunge ndio umteue awe Makamu wa Rais halafu jimbo lisubiri uchaguzi mdogo kupoteza pesa na muda. Viongozi wangu Diplomatic leaders Emanuel Nchimbi na Mdogo wangu Anthony Mtaka wanafaa kabisa hiki kiti ndani ya chama.

Chama changu CCM pamoja na Mama yangu Samia Suluhu hawa vijana wawili wanatufaa sana kwa maandalizi ya baadaye. Wanaweza kuunganisha watanzania wakawa wamoja na uwezo wao wa kuwatuma kulitumikia taifa ni mkubwa.Kwa maoni yangu binafsi kabla ya Chama na maamuzi ya mama hawa wanafaa kabisa.

Naomba kushauri kama mwanachama hai anayetokea JF na pia anayeshiriki vikao mbali mbali vya chama.

Ahsanteni
 
Tunatakiwa tuangalie mtu ambaye ana msimamo, anaweza kusimamia mipango ya chama na serikali iliyopangwa kutekelezwa ndani ya miaka mitano ijayo, mtu mwenye kusimamia uchumi wa serikali na ambaye hatayumbishwa na mabeberu - wanaweza kumtoa kwenye mstari ashindwe kutekeleza malengo ya taifa ipasavyo! Kwa mtazamo wangu watu hawa wanafaa:-

1. Bashiru Ally Kakulwa
2. Andrew Chenge
3. Palamagamba Kabudi
4. Prof. Leonard Chamriho
 
Mtaka nchi itatajirika. Kwanza neno mtaka tu maana yake ni "mtu tajiri"
Maana anaspirit ya kijasiliamali.
Ni mtu wa M aende Leo. Kama amewahi kuwa Mkuu wa mkoa bora katikati ya uwepo wa baswite naamini anaweza kuwa Mkuu wa mikoa bora.

Huyo mwingine ni business as usual
 
Tumuache Mama mwenyewe achague mtu ambaye anaweza kufanya naye kazi. Kisheria Raisi ndiye anachagua makamu. Hii ni kazi na sio kuchagua watu ovyo tu
 
Nchimbi ni mwana-Siasa mzuri lakini Samiah hawezi kukubali kirahisi hasa ukizingatia Lowassa yupo ndani ya nyumba!!! Kufanya hivyo itakuwa ni kama kukaribisha vuguvugu la urais 2025 kabla ya wakati na hivyo kumfanya Samiah atawale kwa shida wakati bila shaka hata mwenyewe (Samia) angependa agombee hiyo 2025!
 
Back
Top Bottom