Baada ya Kifo cha Rais Magufuli: Nani anafaa kuwa Makamu wa Rais Tanzania?
Nchimbi ni mwana-Siasa mzuri lakini Samiah hawezi kukubali kirahisi hasa ukizingatia Lowassa yupo ndani ya nyumba!!! Kufanya hivyo itakuwa ni kama kukaribisha vuguvugu la urais 2025 kabla ya wakati na hivyo kumfanya Samiah atawale kwa shida wakati bila shaka hata mwenyewe (Samia) angependa agombee hiyo 2025!
Uanasiasa wake mzuri una tija gani kwa Taifa? Watanzania tunataka mtu mwenye maono na anayejitambua. Wanamtandao hatutaki hata kuwaona maana ubinafsi wao ndiyo umetufikisha hapa tulipo kama Taifa
 
Uanasiasa wake mzuri una tija gani kwa Taifa? Watanzania tunataka mtu mwenye maono na anayejitambua. Wanamtandao hatutaki hata kuwaona maana ubinafsi wao ndiyo umetufikisha hapa tulipo kama Taifa
Magufuli hakuwa mwana-Mtandao! Kutokuwa kwake mwana-Mtandao kumesaidia nini zaidi ya kuleta madhira kwa wananchi?!
 
Naona huijui Tanzania vizuri
Suala la dini, jinsia
Mtu wa Bara /Zanzibar huwa linazingatiwa

Kinacho zingatiwa ni umakamu wa Rais lazima atoke Tanzania visiwani (Zanzibar) na wala hakuna clause yoyote inayo sema lazima awe mwislaam, kinacho tafutwa pale ni uwezo wa kuchapa kazi si dini, ni coincident kwamba majority ya raia wa Zanzibar ni waslaam lakini akipatikana Mzanzibari ambaye ana sifa na ni mkristo Umakamu wa Rais wa Tanzania.

Nakubaliana nawe kwamba katika teuzi suala la gender balance linazingatiwa sana lakini sio Dini, after all Serikali haina Dini - wanao shabikia shabikia masuala ya teuzi zitakazo zingatia madhehebu ya kidini ni wenzetu Waislaam hata sijui kwa nini?
 
Tunatakiwa tuangalie mtu ambaye ana msimamo, anaweza kusimamia mipango ya chama na serikali iliyopangwa kutekelezwa ndani ya miaka mitano ijayo, mtu mwenye kusimamia uchumi wa serikali na ambaye hatayumbishwa na mabeberu - wanaweza kumtoa kwenye mstari ashindwe kutekeleza malengo ya taifa ipasavyo! Kwa mtazamo wangu watu hawa wanafaa:-

1. Bashiru Ally Kakulwa
2. Andrew Chenge
3. Palamagamba Kabudi
4. Prof. Leonard Chamriho
Kakulwa bado ni underdog, ilitakiwa japo awe alishakuwa wazir, ila bahati ipo upande wake hata hicho cheo cha katibu mkuu kiongozi, kinaweza kimpwaye

Chenge ana mawaa ya kumtosha na ambayo hayajajibika hasa kwny kujilimbukizia mali, yaani naamini akiona deal hataiacha na ataila kimyakimya. Nafikir asbr kwanza

Kabudi huyu kwa mda mchache, nimeona yupo tayar kufanya chochote mradi atetee maslahi yake binafsi ama nafasi alionayo ama ishukilia than kusimamia haki na ukweli halisi
 
Kinana, VP
Nape waziri mkuu.
Baraza la mawaziri lote vunjiliwa mbali.
 
Kwa sababu ni mngoni mwenzako? Hatuko tayari kurudia makosa. Taja sifa zake hapa. Kinyume na hapo, mshauri abakie huko huko! Hatutaki kabisa watu wanafiki nawachumia tumbo safari hii.
Uzoefu ndani ya Chama na Serikali, Elimu, umri unamruhusu hatuhitaji wazee tena, Mwanadiplomasia, anaifahamu system vizuri, yuko ngangari so atamsaidia mama vizuri, amekuwa nje ya siasa zetu kwa takribani miaka mitano, ni catholic, huwezi kuepuka ku balance hilo. Pia italeta sura ya utaifa kutoka maeneo anayotoka.

Huyu kama sio tu kuwa mhanga wa siasa za 2015 alikuwa ana nafasi kubwa ya kumrithi Kinana.

Labda na mtu mwingine lakini Mtaka bado japo anaonekama kuwa potential leader baadae
 
Tulikuaga na Jakaya na Shein, Jakaya na Gharib Bilali..

Kipi ulipunguza? Ambacho wakati wa Magufuli na Samia ulikiongeza?
Waziri mkuu alikua Lowasa na Pinda(Wakristo),nadhani jamaa anaongelea nafasi 3 za juu ni busara kuwe na mchanganyiko kama ilivyo kua Awamu zilizotangulia.
 
Magufuli hakuwa mwana-Mtandao! Kutokuwa kwake mwana-Mtandao kumesaidia nini zaidi ya kuleta madhira kwa wananchi?!
Magufuli alipendekezwa kamati kuu baada ya hao wana mtandao kulianzisha mara tu jina la mtu wao (Lowasa) kukatwa! Na huyo Nchimbi alishiriki kwenye ule mkwara ulio wasababishia kamati kuamua bora wakise wote!
 
Back
Top Bottom