Lukuvi anafaa sana.
Lukuvi anauwezo mkubwa sana wa kufuatilia mambo.
Lukuvi atamrahisishia Rais wetu kuwashughulikia wezi waliojazana kila sekta huku wakijiita wazalendo.
Lakini pia yupo Dr. Slaa. Huyu ni mtu safi asiye na tuhuma wala uroho wa kujilimbikizia mali.
Mtendaji Mwingine anayeweza kumsaidia Mh. Rais Samia Suluhu ni AGREY MWANRY.
Huyu utendajo wake ni wa kutukuka bila kumwonea mtu. Anajua kuwabana wabadhirifu wa mali za umma kwa haki kabisa.
Kuna mwingine anayetajwa ,huyu ni Prof. Kabudi,; huyu ni mtu asiye na dira maalumu. Ni mlugaluga. Leo yupo hivi kesho vile. Mama achukue tahadhari sana kwa watu kama hawa , hawa ni wale waliokua wanajiona bila wao nchi haitaenda , utafikiri wao ndio Mungu.
Mungu aliyemuumba Magufuli ndiye aliyemuumba Pia mama Mh. Samia.
Anayebaki kumtukuza binadamu badala ya Muumba huyo tutamsamehe bure.
Nchi hii inahitaji mabadiliko katika fikra za kusaka uongozi.
Uongozi umekua ni fursa ya kujineemesha badala ya kutoa haki bila ubaguzi.
Ni Ukweli uliojificha kuwa kuna kamtandao kalikua kanajikita kwenye utawala kwa mgongo wa utendaji wa serikali huku kakiwapoteza na kuteka watu wote waliokua tishio kwao kisiasa na kiuchumi. Kamtandao hako ndiko kalikoitia dosari serikali yetu.
Ni kamtandao kalikojificha kwenye utekaji, uporaji wa fedha za watu kwa mgongo wa uhujumu uchumi , kutisha watu, ukabila ,udini na misingi ya ukanda. Haka kakundi kalikojificha chini ya kivuli cha kupigania chama na serikali kalikua na malengo maovu sana ka kuigawa nchi vipande vipande ili pawe na vinchi kama Rwanda bahati nzuri Mungu ametuletea Rais Jasiri Kabisa Mama yetu Samia Suluhu ,asiye na upendeleo wala maslahi binafsi ili aimarishe umoja wetu na utu wetu kama watanzania.
Nchi ilifikia mahali kutaja neno haki hata kwenye nyumba za Ibada ni kosa na viongozi wa dini wakawa wanahubiri maendeleo ya vitu na kusahau utu,haki, wema na usawa.
Viongozi wakawa wanasema hatutaki HAKI tunataka maendeleo.