Baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu JamiiForums, nimeona nianze hivi

Mkuu hongera sana kwa hatua uliyo fika mungu yupo nawe kaka
 
Hii thread imekuwa ya manufaa sana kwa wanajukwaa wazo linazaa wazo jingine kiasi inaamsha ari ya kufanya kitu kujikwamua binafsi nimevutiwa mawazo humu na jana nilimtafuta mleta uzi na tuliongea kwa kirefu,Tueendelee kushirikiana sisi ambao hatujaanza hii safari tunategemea sana msaada hapa jamvini na vinginevyo.
 
Ujumbe,
Opportunities za kutengeneza pesa kwa uhalali ni nyingi sana, waache kutoa hizo opportunities kwa watu ambao ni wakwepa kodi kwa tamaa ya 10%. they should think bigger than that...
Uko sahihi kabisa mrembo.
 
Ujumbe,
Opportunities za kutengeneza pesa kwa uhalali ni nyingi sana, waache kutoa hizo opportunities kwa watu ambao ni wakwepa kodi kwa tamaa ya 10%. they should think bigger than that...

CC: mafisadi wote wachumia tumbo
 
Mkuu asante sana kwa kutuhabarisha habari njema, ila mkuu nilikuwa na shida kuhusu shamba huko, na heka huanzia tsh ngapi?

Karibu uje tufuge. Shamba linaanzia sh. Laki mbili Kwa heka.
 
Hongera sana Eberhard,
mi pia ni mdau, nilianza mwaka juzi kwa kununua mashamba, so far nimeshapanda mitiki huko mkoa wa pwani na pines huko iringa, miti yote inaendelea vizuri, nategemea 5 years from now nitaanza kuvuna. Pia nina mpango wa kuweka mifugo kama kuku na mbuzi na kulima mbogamboga by next year. Biashara ya upandaji miti ni nzuri sana hasa kwa wale waajiriwa kwani ahiitaji usimamizi wa karibu sana.
kwakweli inafurahisha sana kuona kumbe WATZ tunaweza tengeneza pesa nyingi tu bila kula rushwa. all the best

Mitiki ya mkoa wa pwani vipi?

Maana nilisikia huwa haifanyi vizuri sana huku pwani.
 
Ni kweli kabisa,leo ni moja ya siku ambazo nimejifunza kitu cha msingi,nakushukuru sana mkuu Eberhad,ubarikiwe sana..Mimi nasubiri tu huu mkataba na huyu mkoloni mweusi uishe,this Dec,2013 nami niingie huko kwa nguvu,ingawa nimeshanunua baadhi ya maeneo huko Mvomero.

Nataka nikasimamie kikamilifu
 
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.

Big up....TRA umewaachia manyoyaaa na Vumbiiiiiii
 
Eberhard umefanya jambo la kishujaa sana. Mimi binafsi nakupa hongera zangu na kukutia moyo kuwa plan yako ni njema sana kukupeleka kwenye bigger plan. Nakushauri uanze kufuga mmbwa kwenye hilo eneo kama ulinzi kwa kuwa wezi siku hizi wanarudisha sana maendeleo ya watu. Jitahidi utafanikiwa. Sky is the limit.
 
Last edited by a moderator:

Wewe ni mtu wa pili kunishauri. Nakuhaidi nitazingatia ushauri wako.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kumaliza degree yangu ya pili na kuona kuwa ajira kama ajira haiwezi kuwa mkombozi wangu kiuchumi niliamua nifatilie mawazo mbalimbali ya ujasiriamali. Nikafikiria ujasiriamali wa kiubunifu wa hali ya juu ndiyo utakuwa mkomnozi wangu kiuchumi. Nimeanza Kwa kununua shamba lenye ukubwa wa hekari 11 nje kidogo ya mji wa Morogoro ( Kwamakunganya-majichumvu). Imenigharimu 1.3 m kununua eneo hili lote.. Nililipia taratibu hata sasa bado nadaiwa sh 60 elfu nayotegemea kuimalizia after 2 weeks. Sehemu kubwa ya shamba langu nimepanda mitiki.

Baada ya kufatilia humu nikagundua kuwa mradi wa nguruwe na kuku wanalipa sana. Kwa kuwa imani yangu inaniruhusu nikaona ni laziima niifanya hii ya kitimoto pia. Hivyo nikaanza maandalizi ya kufuga nguruwe na kuku pia. Hivyo nilianza Kwa kuanzia kuchimba na kujengea tangi la maji chini. Ilimigharimu Kama miezi miwili tangu langu la maji kukamilika. Tangi langu la maji Lina uweze wa kujaza maji lita 30 elfu. .

Baada ya hapo nikaanza maandalizi ya ujenzi wa banda la nguruwe na la kuku. Baada ya mabanda yangu kukamiliaka nilisafiri hadi singida kufata kuku. Bei ya kuku singida inalidhisha sana. Ili upate kuku wa bei rahisi inakupasa uende kijijini ambako kuu huuzwa cheap. Hivyo nilisafiri hadi kijijini ambako nililinunua kuku 31 ambao ndiyo nimeanza nao.. Kwa upande wa nguruwe nimeanza na 12 ambao niliwanunua wakiwa na miezi mitano. Pia nimeweka kanga na mbuzi Kwa ushauri wa marafiki.

Ninashukuru Mungu ninaanza kuwaona kuku wameanza kutaga Kwa fujo. Pia ninamshukuru Mungu Kwa kuwa ninaona ninaanza kuwa muajili pole pole. Pia ninamshukuru Mungu ninaona mawazo ya kunyanyasika( kuajiliwa) yanaanza kupotea taratibu.
Kupitia uzi wangu huu nitakuwa nawataarifu maendeleo ya mifugo yangu Kama sehemu ya kuwatia moyo wajasiriamali wenzangu. Morogoro ni sehemu ambayo wajasiriamali mnaweza kutimiza ndoto zenu Kwa kuwa Ardhi inapatikana Kwa bei nafuu na ni Karibu na Dar kwenye soko kubwa la bidhaa mbalimbali.

saaaafi sana tuspende kuajiriwa tujiajiri wenyewe bwana
 
Nimepata maswali juu ya namna kilivyo kisima changu Cha maji. Ebu oneni kisima changu Cha maji.
 
hehehe

Una ujumbe gani kwa mafisadi?

Naona kuna Fisadi au Fisadi Mtoto ZeMarcopolo ameshatoa comment ya kinafiki hapo nyuma. Quote, "This is what we call KUELIMIKA. Excellent example."

Nafikiri ataenda kuwaambia mabosi wake wapi pa kuanza kukata kodi.
 
Back
Top Bottom