Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Uko sahihi kabisa, huyu Pslmp akubali mikataba yote tata ipelekwe bungeni. Kelele hazijaanza leo kwa huu wa Bagamoyo, yote yenye ukakasi ikajadiliwe tupate mwanga. Ununuzi wa ndege umepigiwa kelele sana, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, kelele tumezisikia, kwa nini huyu Pslmp anataka huu wa Bagamoyo tu?
 
Huyu ni sura halisi ya MCHUMIA TUMBO, ambaye anakwenda na "upepo"; na kwa akili yake, anadhani kesha jua na kufahamu "upepo" huu wa sasa hivi UNAVUMAJE? Ananchofanya ni kubahatisha tu, hivyo aangalie isije IKALA KWAKE!
Tuna hasara kubwa Sana Watanzania, huwezi kaa kimya miaka sita yote husemei Bandari, halafu leo tena baada ya Raisi kufariki ndipo uje kutuonyesha uzuri wa uwekezaji huo

Kwani isiwe 2015, ni Kweli yeye alikuja na ushauri huo baada ya kwenda China, akapendezwa na Ile ramani na bandari ya wawekezaji hao Kwa jinsi ilivyo kubwa na nzuri, lkn mkuu aliposoma Mkataba ule akasema, nanukuu, Ni mwenda wazimu pekee wa kuruhusu ujenzi wa Bandali hiyo baada ya hapo mkuu wa mhimili wa Bunge naye akaunganishia hapohapo, mjadala ukazimwa

Kwa nini leo auone ni Mradi Safi tena baada ya kifo cha Raisi alitekuwepo?? Je aliahidiwa Lupia kutoka Kwa wawekezaji hao??

Tunataka Mkataba wote usomwe bungeni Maana tunajua, sio Bunge loote likakosa mtu muungwana hata mmoja ingawa CCM siiamini tena!
 
Sawa mkuu, ulitaka kuhitimishaje
Kwenye chaguzi zijazo, tuache demokrasia ichukue mkondo wake. Uvurugaji wa uchaguzi wa 28 October 2020, hautasahalika katika historia ya chaguzi Tanzania. Hicho kilichopo bungeni ndicho JPM na wana CCM walikishangilia na kukiita ushindi wa kishindo na wakihistoria.
 
Si unajua Watanzania ni kama bendera na upepo!!
 
Ukweli ni kuwa ukifanya comparison analysis ukiwa objectively kabisa kati ya mikataba iliyoingiwa wakati wa JK na ile ya wakati wa JPM utaona mikataba karibia yote ya wakati wa JK ilikuwa ya kipigaji kuliko ya wakati wa JPM.
Umeshaona mikataba mingapi mkuu? K
 
Usemi huo hapo juu wa Hayati Rais Magufuli utasimamiwa na Watanzania wapenda haki kwa kupinga kwa nguvu zote huo mradi wa KIJINGA NA HOVYO, hata hao Wabunge sidhani kama wataunga mkono UPUUZI HUO. Ndugai na Wanamtandao wenzake hawana ubavu wa kuutetea mradi huo wa kjinga, alichofanya huyu ni KUJARIBU KUPIMA MAJI KWA MIGUU, yataondoka naye!
 
Walipenda kuimba wimbo uliopendwa na aliyewalipa. "Anayemlipa mpiga zumari, ndiye huchagua wimbo aupendao" By J K Nyerere.
 
Ndugai ana yake ya kujibu sioni kama anastahili kuwepo hadi mwisho wa mwaka huu.
 
Ndugai ana yake ya kujibu sioni kama anastahili kuwepo hadi mwisho wa mwaka huu.
Swali langu ni moja tu, Kwa nini alitaka amwongezee muda wa utawala?

Ni Kwa sababu alizuia Mradi wa bandari ya Bagamoyo.. ama nini hasa!!
 
Kwa hiyo hapa unataka kuniambia Professor Assad alikuwa sahihi???
Mkuu, alikuwa Sawa kabisaa

Ni mnafiki mno huyu jamaa, anayumba vibaya, utamsikia atavyofoka Leo na hizi nyuzi za kumponda kuruhusu wizi huu makubwa,
 
Ndugu zangu haya yaliyoibuliwa na CAG ni machache ya mengi ya yanayoendelea humu nchini kwa mfano nikizungumzia miradi ya maendelee hususani mradi wa reli ya SGR kuna madudu ya kufa MTU nikianza tuu na maswala ya rasilimali watu waturuki waliokuja hawajui kitu. Kuna makampuni Tanzu (sub) hazina usajili wowote kama vile CRB na bodi imekaa tuu wala hawafuatilii ukija kwa ma Engineer ndio kabisa wapo wakutosha hawajasajiliwa na bodi ERB na bodi IPO tuu ikumbukwe sio pesa tuu za registration tunapoteza ila pia hawajamaa wana jeopardize nafasi za wazawa na pia kuikosesha serikali mapato payee.

Quality ya kazi ni mbovu kupata kuona transformer mbovu zimefungwa tusubiri wakati wa operation tutaona mengi maana maintenance itakuwa ya garama sana maana vitu vilivyofungwa ni repair tuu kwa mfano km153 DATS-03 transformer mojawapo ilipo pale ni mbovu. Na mambo mengine ya ovyo kabisa nasikitika sana maana serikali yetu imeashindwa kuwa na watalamu wa kutosha kusimamia hivi vitu ili hali tupo watu wenye ujuzi na utaalamu wa kutosha tupo tuu mtaani.
 
Mkuu, alikuwa Sawa kabisaa

Ni mnafiki mno huyu jamaa, anayumba vibaya, utamsikia atavyofoka Leo na hizi nyuzi za kumponda kuruhusu wizi huu makubwa,
Mkuu mambo ni ya ovyo huko serikalini hamna haja ya kuwa na serikali kama MTU mwenye dhamana ya kuisimamia serikali unasema eti alishauriwa vibaya wewe ulikuwa wapi wakati unalipwa kwa kazi hiyo.
 

Tutaongea mambo meeengi then hakuna muafaka.

Hapa mkataba wa mradi uwekwe wazi tujue nani mwendawazimu ama kichaa kati ya wanao ukubali na yule alieukataa full stop.
 
Hata BUNGE sio la kuamini sababu limejaa wanafiki na wachumia tumbo. Wauweke hadharani raia kwa kushirikiana na TLS tuuchambue
Nadhani hii ndiyo njia sahihi ya kuondoa utata wa jobu aka kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…