Baada ya kubainika ufisadi wa kutisha, anataka kujifichia kwenye Mradi Bandari ya Bagamoyo?

Watakaoujadili ni wabunge gan labda?,labda bunge livunjwe uchaguzi urudiwe upya tena chini ya tume huru ya uchaguzi
 
Hivi huyo siejii ametoa pia na taarifa ya matibabu ya huyo spika kweli kipindi kile wakati anaumwa??

Manake napo pesa zilizotumika nasikia ni balaa
Huyo mgogo dhaifu kaona ahamishe magoli, atutoe kwenye madudu ya wizi, maana watu wanaweza kukumbushia aliyeweka record ya kuwa mgonjwa ghali nchini.

Everyday is Saturday............................... 😎
Na kweli tunahitaji
CAG atuweke wazi gharama za matibabu ya huyy spekear
 
Hakuna kiongozi ambae simuelewagi kama huyu, hana analolisimamia hana analoliamini, anajazwa.kila kitu. Sijui alikuwaje na hiyo nafasi.
 
Wanataka kuanzisha mradi mwingine halafu wapige. Nchi imejaa watumishi wa aina yake. Hawaogopi kusema uongo hadharani wala kupiga mali ya umma.
 

NDUGAI NA BUNGE LAKO MNA KILA SABABU YA KUWAJIBIKA KWA MAPUNGUFU YOTE YALIYOAINISHWA NA REPORT YA CAG KWANI KAZI YENU KAMA BUNGE NI KUISIMAMIA NA KUISHAURI SERIKALI , KAZI AMBAYO HAMKUITIMIZA KWA UFANISI!! NI LAZIMA MUWAJIBIKE.
 

Faida na hasara ni Mkataba Kiongozi, sio maneno ya Spika wa Bunge. Kumbukumbu zangu sijawahi kusikia huo Mkataba ukijadiliwa Bungeni.
Aache uhuni huyo jamaa, kama kapokea rushwa tujue pia. Kwa jicho la tatu, huu mradi kung’ang’aniwa kurudishwa sio bure. Ukizingatia kwa wahuni walewale ambao hawajawahi kuisimamia Serikali kikamilifu.
Sasa tunaanzaje kuwa na imani na watu hao wa calibre ya Spika wetu?
 
Ndugaye ang'olewe pale
 
NDUGAI NA BUNGE LAKO MNA KILA SABABU YA KUWAJIBIKA KWA MAPUNGUFU YOTE YALIYOAINISHWA NA REPORT YA CAG KWANI KAZI YENU KAMA BUNGE NI KUISIMAMIA NA KUISHAURI SERIKALI , KAZI AMBAYO HAMKUITIMIZA KWA UFANISI!! NI LAZIMA MUWAJIBIKE.
Ndugaye, ang'oke
 
Yaani huyu Ndungai ni wa kuchapwa viboko kabisa
 
Kama nchi yetu kila Chama ni cha majambazi, tufanye nini sasa?
 
Haitakiwi kuwalaumu viongozi wa kipindi cha Jiwe wengi walitetea matumbo yao, hawakutaka kuacha kazi na kwenda kujiajiri, ila walisema vijana wa graduate tujiajiri.
Kutetea matumbo yao je -hata spika? Kiongozi wa muhimili no way. Unatania
 
Ndugai ni spika wa bunge letu ana mamlaka ya kuomba mkataba ukajadiliwa bungeni na Watanzania wakausoma na kuuelewa ila kitendo cha kusema alienda China sijui balozi Kaituki aliwapeleka Shenzein ilipo hiyo kampuni na walipata presentation nzuri mimi binafsi sijamuelewa hao wachina angalieni Zambia wanavyoteseka kwa sababu ya kuwapa kila kitu haijatosha huko Zambia kumekua na polisi wa kichina wakilinda Mali walizochukua kwenye serikali sio watu hao huko Zimbabwe wanapata tabu na mikataba mibovu waliyoingia ya madini na makampuni kutoka China...
 
Msimamo wa Ndilugai toka mwanzo ni kuwa mradi wa bandari ya Bagamoyo ulikuwa mzuri na ulikuwa na faida kubwa kwa nchi. Lakini sijui kulikuwa na mazingira gani, ilimlazimu kubadili msimamo wake baada ya Rais kutoutaka huo mradi.

Kosa kubwa la awamu ya 5 ilikuwa ni kuminya uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari. Kama laiti uhuru wa maoni na wa vyombo vya habari ungelindwa kwa matakwa ya katiba, ni dhahiri watu wengi wangeweza kuuchambua huo mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, na kisha hata ambao tusiojua content ya huo mkataba, tungejua kwa uhakika kama mkataba ulikuwa mbaya au mzuri.

Serikali awamu ya 6, lindeni kwa nguvu zote uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari. Kunabfaida nyingi kufanya hivyo kuliko hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…