Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Trump yeye akifanya harambee inajulikana kabisa kuwa kila atakayehudhuria atatoa kiasi fulani cha pesa na mara nyingi hawa huwa ni marafiki na matajiri ambao kwa namna moja au nyingine hufaidika na utawala wake kwa ku-influence policies zake ili ziendane na interests zao za kibiashara na kiuchumi huko majimboni kwao na kwingineko. Siamini kama mtu anaweza kutoa 10B na asitegemee cho chote in return.
Kwa nchi zetu za kiafrika Harambee kama hizi huwa zina faida sana kama zinafanywa ili kusaidia miradi ya kijamii mfano kujenga vituo vya afya nchi nzima. Hii ya matajiri kuchangia chama kinachotawala kidogo ina ukakasi. Mtu atoe bilioni 10 halafu kesho kweli umkamate eti sijui ana kilo kadhaa za unga laini wa muhogo au kakwepa kodi ya bilioni 50. Hii inaweka precedent mbaya hasa katika demokrasia yetu hii inayojikongoja na mihimili ambayo ni dhaifu kiutendaji.
Wazo zuri japo naamini lina madhara!