#COVID19 Baada ya kumaliza Maombolezo ya kumuaga mpendwa wetu Magufuli, tujiandae na maambukizi mapya ya COVID-19

Uko sahihi maana 'Mdharau mwiba mguu huota tende'.
 
Tumaini pekee la kutupoza ni kwamba watu wengi ni vijana, wana afya nzuri na na tayari wana antibodies kutoka maambukizi ya awali.

Kama ukijichanganya humo mzee na una magonjwa, Covid-19 inakufyekelea mbali.
 
Kaa kwa kutulia bro! Kwani si umeshajikinga we na watoto wako inatosha au??????

Unataka nini sasa au nenda uwanjani halafu toa hoja yako ya kuvaa barakoa kitakachokupata uje hapa utoe mrejesho
 
Hakika[emoji122][emoji122]
 
Tunalazimishwa kuishi katika dilemma 'mkwamo'? wa "the slippery slope fallacy" kwa:

1. Kukataa ukweli kwamba covid-19 ipo duniani na bongoland.
Tumo ktk mteremko mkali kwenye gari lisilo na breki!

2. Tumepanda gari hilo kwa kupuuza maelekezo ya WHO kuhusu kupima, kutoa data, kujikinga, kuwapa watu chanjo.
Sasa inatubidi tutetee na kulinda msimamo (falsafa) wetu kwa gharama kubwa!
 
Inasikitisha sana ,waTZ tunaichukulia poa sana UVIKO.
 
Hst
 
Mikusanyiko kama hii ipo tangu mwaka jana
 
.
 
Kuna mjerumani mmoja alihojiwa akasema amekuja Tanzania kwa sababu ni pazuri hakuna lockdown, hakuna kuvaa barakoa kama kule kwao. Akamshukuru Magufuli. Na alikuwa amekuja kuaga na kusema Magufuli was very smart. Na akawa ana furahia watu kutokuvaa barakoa. Yupo na mtoto wake. Anasema walikuwa wamechoka kuvaa barakoa kule kwao na hataki hii chanjo. Link hiyo hapo chini.

 
Hatuombei vifo, maradhi na Mungu atupe wepesi Insha Allah. Ila kwa kuwa tunafanya makusudi, basi tutarajie majanga makubwa ya COVID 19 in three to four weeks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…