Nikiwa na miaka 21 kuna mwanaume mtu mzima (39) amekuwa akionesha nia ya dhati ya kutaka kunioa.
Mm nilimpa masharti kuwa siko tayari kwa ndoa lkn akaning'ang'ania. Nikawa mtoto wa kike nikikohoa tu muamala unasoma, nikilia shida muamala unasoma na nikiwa na uhitaji wowote ule muamala unasoma.
Ni mwaka wa 3 sasa tangu anigande lkn sikuwahi hata kutoka naye out ya lunch wala dinner, achilia mbali utelezi ndiyo aliogopa hata kugusia. Kwasabb nilmwambia kama ana nia ya dhati ya kunioa asubiri ndoa.
Hivi sasa kanikomalia anataka akatoe posa lkn mm naona hatuendani maana yeye sasa ana 42 na mm 24. Nimebuni mbinu ya kumpiga chini pasipo maumivu.
Nimemwambia nikamtambulishe kwanza kwa wazazi kabla ya posa. Lkn nimekula dili na mama kuwa amkatae siku akija home. Tukifika tu home mama anune na awe mkali haswaa!
Kisha mama ataniandikia sms ya mchongo ya kumkataa. Halafu nitamuonesha ama kumtumia hiyo sms.
Mliosoma Cuba mpo?
Mbona akili zako zimejaa ubinafsi na uzandiki kabila hiyo unaoweza kusababisha majanga ya makusudi na ya kujitakia bila sababu?
Halafu inaonekana haujasoma na hauna elimu yoyote masikini!
Hapo mkubwa kibaiolojia ni wewe na mdogo kibaiolojia ni yeye.
Aliyestahili kumkwepa kwa uzee mwenzake ni yeye na si wewe.
Kwanini nimesema hayo?
Ni kwamba mwanamke ukifikia "menopause" unaelewa ni nini hutokea na kuendelea baada ya hapo?
Yote hayo huwatokea kina mama kuanzia umri miaka 47 hadi 50 tu ujue.
Kwa muktadha huo sasa, miaka hiyo yako24 kufikisha miaka 50 bado 26 tu.
Kwa mwanaume kama anaishi maisha ya staha, kuanza kupoteza uwezo wa "kupanda kwenye tuta" ni mika 80.
Sasa kwa miaka 42 aliyonayo jamaa, kufikia miaka 80 bado miaka 38, hapo nani atazeeka kabla ya mwenzake?
Maana yake ni kwamba, kibaiolojia wewe ni mkubwa na unamzidi jamaa umri wa miaka12 ya kuzeeka kabla yake.
Ambapo mgeoana, siku za usoni angelihitaji mwanamke mwingine wa "kumhifadhi" kuziba pengo kwa miaka yote hiyo 12 ambayo wewe ungelikuwa umezeeka "haujiwezi".
Umeona ambavyo kwamba haujui usichokijua kuhusu rehema za uumbaji wake maulana?
Roho za chuki na husda ndiyo mmeziweka mbele, utu hakuna.
Kama hauna mpango naye kwa nini usimkatae na kuweka msimamo wako mapema, kuna ulazima gani wa kuingiza utapeli na ulaghai wa kipumbafu pumbafu namna hiyo?