kwa wale wanaume ambao huwa wanahudumia familia watashangaa, na wanawake wanao hudumiwa watashangaaa ila liko kundi kubwa la joyce kama mimi hapa, nimehangaika na mwanaume namlisha namvika yani kilakitu mimi, badae nikaona kama labda kipato chake kidogo hawezi kunihudumia nikampeleka shule amesoma kozi nzuri ya afya ambayo anaweza kufanya kazi hata private nimelipa ada miaka 3 nimeishi kwa kujibana sana na mwanangu kila mwezi namtumia matumizi na ada maana alisoma private chaajabu amemaliza chuo hataki kufanya kazi anataka niendelee kumlisha cha kushangaza niliuza kiwanja ili kusapot mambo ya ada na matumizi akiwa mwaka wamwisho yule mnunuaji akatoa hela nikamtumia ametumia zimeisha na shule kamaliza kuja waandikishane akakataa eti hiyo hela hajafanyia kitu hajanunua viatu, suti, na vitu vizuri sasa ili kuondoa lawama nikaenda vikoba nikakopa hela milioni moja nikampatia ndo akaandikishana ,hapo hakunipa hata senti moja na zimeisha yani nina hasira kuliko za joyce niko najipanga kumfungulia mashtaka ya kudai talaka simtaki, kibaya zaidi muhuni , mchoyo, muongo, mwizi. akikuta cmu hapo anapitia, hela anapitia afu mlokole anajiita mtumishi wa bawana , unashangaa hata akipata kidogo utasikia tu ah fulan alinisaidiaga alinipa hela kiasi fulan lkn mimi hajawahi nipa sioni umuhimu wake nimeona nipige chini. humu jamii forum niliwahi kuomba ushauri kipindi cha nyuma hakuna hata alonijibu vya maana